Pages

Saturday, August 17, 2013

YANGA YAILAZA AZAM BAO 1 - 0 MECHI ZA NGAO YA JAMII LEO



BAO pekee la kiungo Salum Abdul Telela jioni hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeipa Yanga SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC na kutwaa Ngao ya Jamii.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Oden Mbaga, aliyesaidiwa na Hamisi Chang’walu na Omar Kambangwa wote wa Dar es Salaam, hadi mapumziko Yanga SC walikuwa mbele kwa bao 1-0.

Yanga ilipata bao hilo mapema tu dakika ya pili, mfungaji kiungo Salum Abdula Telela aliyeunganisha pasi ya Didier Kavumbangu.

Kipindi cha pili, Yanga SC waliendelea kucheza vizuri na kukosa mabao zaidi, huku sifa zaidi akistahili kipa chipukizi Aishi Manula.

Dakika ya 67 Telela alikarbia kufunga tena baada ya kuunganishia nje krosi nzuri ya Haruna Niyonzima.

Dakika ya 81 Niyonzima alikaribia kufunga mwenyewe kwa mpira wa adhabu, lakini shuti lake liligonga mwamba wa juu na kudondokea chini kabla ya beki Aggrey Morris kuondosha katika hatari.

Kikosi cha Yanga SC leo kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’/Deo Munishi ‘Dida’ dk15, Juma Abdul, David Luhende, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan/Mbuyu Twite dk15, Athumani Iddi ‘Chuji’, Simon Msuva, Salum Telela, Jerry Tegete/Hussein Javu68, Didier Kavumbangu na Haruna Niyonzima.

Azam FC; Aishi Manula, Erasto Nyoni/Joackins Atudo dk46, Waziri Salum, David Mwantika, Aggrey Morris, Himid Mao, Kipre Tchetche, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, John Bocco ‘Adebayor’/Gaudence Mwaikimba dk74, Kipre Balou/Ibrahim Mwaipopo dk62 na Khamis Mcha. 

SOURCE: BIN ZUBERI BLOG

FAMILIA ZA JAMII MASIKINI ZAFURAHIA MRADI WA KUKU CHINI YA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA KIMAREKANI LA HEIFER INTERNATIONAL

Mfugaji wa kuku wa asili Bw.  Nicodemus Nzenga mkazi wa kijiji cha  Maluwe akionyesha vifaranga ambavyo vimetotolewa na kuku wa asili ambao anawafuga kupitia mradi wa kuku wa shirika la kimataifa la Kimarekani la Heifer International.
   
Mtaalamu wa mifugo wa halmashauri ya wilaya ya Kilosa  Bw. Nicodemus Nzenga (kulia) akimwelekeza jambo mfugaji wa kuku wa asili mkazi wa kijiji cha  Maluwe Bw. Abdalla Salum.  Mradi huo umefadhiliwa na Shirika la kimataifa la Kimarekani la Heifer International.
     
Bi Asha Ramadhani mfugaji wa kuku wa asili wa kijiji cha Zombo wilayani Kilosa mkoani Morogoro, akiwa amemkamata mmoja wa kuku anaowafuga kupitia mradi wa ufugaji kuku unaofadhiliwa na Shirika la kimataifa la Kimarekani la Heifer International.


FAMILIA ZA JAMII MASIKINI ZINAZOISHI KATIKA VIJIJI VYA MALUWE NA ZOMBO VILIVYOPO KATIKA WILAYA YA KILOSA MKOANI MOROGORO ZIMESEMA KUWA MRADI WA KUKU WA ASILI CHINI YA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA KIMAREKANI LA HEIFER PAMOJA NA MAFUNZO WALIYO YAPATA YA UFUGAJI WA KUKU HAO KWA MBINU ZA KISASA  UNAWEZA KUWASAIDIA KUWATOA KATIKA WIMBI LA UMASIKI LINALO WAKABILI KWA MUDA MREFU SASA.

WAKAZI HAO WAKIZUNGUMZA KWA NYAKATI TOFAUTI KATIKA VIJIJI HIVYO WAMESEMA KUWA HALI YA MAISHA YAO NI DUNI NA WANATEGEMEA KILIMO PEKEE AMBACHO KWA MUDA MREFU HAKIJASAIDIA KATIKA KUINUA PATO LAO NA HIVYO KUENDELEA KUBAKI MASIKINI AMBAPO WAMEFAFANUA KWAMBA WANA IMANI KUPITIA MRADI HUO WA UFUGAJI WA KUKU WA ASILI KWA MBINU ZA KISASA KUTAWEZA KUWASAIDIA KUBADILISHA MAISHA YAO KUTOKANA NA MAUZO YA KUKU HAO.

BWANA NICODEMUS NZENGA AMBAYE NI MTAALAMU WA MIFUGO KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA KILOSA NA MRATIBU WA MIRADI YA HEIFER WILAYANI HAPO AMEPONGEZA JITIHADA ZINAZOFANYWA NA SHIRIKA HILO AMBAPO AMEELEZEA KUWA CHANGAMOTO BADO NI KUBWA KUTOKANA NA UHITAJI MKUBWA UNAOTOKANA NA KUWEPO KWA FAMILIA NYINGI ZENYE SHIDA AMBAPO SHIRIKA HILO LIMEKUWA LIKISAIDIA JAMII MASIKINI 285 KUTOKA VIJIJI 14 TU KATI YA 161 VILIVYOPO KATIKA WILAYA HIYO.

DORICE MOLLEL NDIYE REDD'S MISS ILALA 2013

Redds Miss Ilala  Dorice Mollel (katikati) akiwa na washindi wenzake, kulia ni mshindi wa pili Alice Isaac na kushoto mshindi wa tatu Clara Bayo.




************************

Miss Tabata  Dorice Mollel (22) usiku wa kuamkia jana aliwashinda warembo wengine 13 katika shindano la kumtafuta Redd's Miss Ilala 2013 lililofanyika katika ukumbi wa Golden Jubilee Tower, Dar es Salaam na kufanikiwa kumrithi Noela Michael ambaye alishinda taji hilo mwaka jana, pia akitokea Tabata.

Dorice alizawadiwa shilingi 1.5 milioni/-, na mshindi wa pili Alice Isaac (Dar City Centre) alipata shilingi 1 milioni /-.

Mshindi wa tatu katika shindamo hilo ni Clara Bayo (Dar City Centre) ambaye  alizawadiwa  Sh. 700,000/-. Mshindi wanne Pendo Lema (Tabata) alizawadiwa Sh. 400,000/- na wa tano  Shamim Mohamed alipata Sh. 300,000/-.

Mrembo Juanita Kabunga kutoka Tabata alizawadiwa Sh. 500,000/- baada ya kushinda Miss Talent na Kabula Kibogoti pia kutoka Tabata alishinda taji la Miss Rio and Spa na kuzawadiwa Sh. 200,000/- na ajira ya kudumu kwenye kampuni hiyo.

Warembo waliosalia kila moja alipata kifuta jasho cha Sh. 200,000/- ambao ni Clara Paul, Anna Johnson, Irene Mwelolo, Rehema Mpanda,  Martha Gewe, Diana Joachim, Natasha Mohamed,  Kazumbe Mussa, Kabula Kibogoti na Juanita Kabunga.

MKUTANO WA MWAKA WA WANAHISA WA KAMPUNI YA GESI TANZANIA (TOL) WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM


Bodi ya wakurugenzi wa kampuni  ya TOL Gases Limited wakiwa katika mkutano na wanahisa wa kampuni hiyo uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya TOL Gases Limited Bw. Harold Temu akihojiwa na mwandishi wa habari wa ITV Emanuel Buhohela katika mkutano huo ambao umefanyika jana jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washiriki wa Mkutano mkuu wa mwaka wa Wanahisa wa Kampuni ya utengenezaji wa Gesi ya TOL wakijiandikisha tayari kwa mkutano wa Wanahisa ambao umefanyika jijini Dar es Salaam jana katika ukumbi wa Quality Centre.
 Baadhi ya Wanahisa wa Kampuni hiyo wakipitia makabrasha tayari kwa kuanza mkutano huo.
 Wafanyakazi wa ngazi za juu wa shirika hilo wakiwa katika mkutano huo ambao umefanyika jijini Dar es Salaam na kushirikisha idadi kubwa ya Wanahisa wa Kampuni hiyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya TOL, Harold Temu(kushoto) akijadili jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa TOL, Daniel Warungu kabla ya kuanza kwa mkutano wa Wanahisa jijini Dar es Salaam jana.


MKAKATI unaolenga kuboresha utendaji wa Kampuni ya Gesi ya TOL, umeanza kuwa na mafanikio.

Akifungua mkutano wa mwaka wa wanahisa jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Bodi ya TOL, Harold Temu, amesema kuwa uzalishaji na mapato ya kampuni hiyo yameongezeka katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, kutokana na mipango imara waliyoiweka.

“Hii ni dalili nzuri, kwani kampuni iko kwenye mwelekeo sahihi katika eneo la uzalishaji na mapato yanakwenda vizuri, kwani yameongezeka kwa asilimia 26 hadi asilimia 30 kwa kipindi cha miaka miwili," alisema Temu.

“Faida baada ya kodi imeongezeka mara saba hadi kufikia shilingi milioni 952 kwa mwaka kutoka shilingi milioni 120 za mwaka 2011,” alisema Temu.

Kwa mujibu wa Temu, sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa kuimarisha utendaji wa kampuni hiyo, TOL imekamilisha ujenzi na uzinduzi wa mtambo wa kisasa wa kutengeneza gesi aina ya Oksijeni wilayani Rungwe, mkoani Mbeya.

Alisema uwepo wa mtambo huo, utaongeza uwezo wa kampuni wa uzalishaji kwa asilimia 200 na hivyo kuiwezesha kampuni kukidhi mahitaji yote ya gesi hiyo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TOL, Daniel Warungu, alisema kampuni hiyo iko katika mkakati wa kumiliki mtambo mkubwa wa kuzalisha tani 31 za gesi na kwamba mtambo huo ni mkubwa kuliko mitambo yote katika nchi za Afrika Mashariki na Kati.

“Hatua za kujinufaisha na uwezo mkubwa wa mtambo huo zimefikia mahali pazuri na muda mfupi ujao wateja wetu watanufaika kutokana na uwezo mkubwa wa mtambo wetu,” alisema Warungu.

Alilalamikia pia uwepo wa kampuni feki za gesi ambazo alisema zinatishia kuharibu imani iliyojengeka kwa wananchi juu ya gesi ya TOL.

ASKOFU MSAIDIZI, MCH. GEORGE FUPE KUZINDUA HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA LA KKKT USHARIKA WA MISUGUSUGU (KIBAHA) KESHO AGOSTI 18

"LETENI ZAKA KAMILI GHALANI, ILI KIWEMO CHAKULA KATIKA NYUMBA YANGU, MKANIJARIBU KWA NJIA HIYO, ASEMA BWANA WA MAJESHI; MJUE KAMA SITAWAFUNGULIA MADIRISHA YA MBINGUNI, NA KUWAMWAGIENI BARAKA, HATA ISIWEPO NAFASI YA KUTOSHA, AU LA, NAMI KWA AJILI YENU NITAMKEMEA YEYE ALAYE, WALA HATAHARIBU MAZAO YA ARDHI YENU; WALA MZABIBU WENU HAUTAPUKUTISHA MATUNDA YAKE KABLA YA WAKATI WAKE KATIKA MASHAMBA, ASEMA BWANA WA MAJESHI ." (MALAKI 3:10-11)

Zifuatazo ni picha mbalimbali za kanisa hilo lilivyo kwa sasa:

Sehemu ya lango kuu la kuingia kanisani.





Sehemu ya madhabahu ya kanisa hilo.

Kanisa hili la KKKT usharika wa Misugusugu lipo barabarani upande wa kushoto kama unatoka Dar es Salaam kwenda Morogoro. Uzinduzi wa harambee ya kuchangia ujenzi utafanywa na Msaidizi wa Askofu, Mch. George Fupe, kesho tarehe 18 Agosti 2013 kuanzia saa 2.00 asubuhi.  Wote mnakaribishwa kuchangia ujenzi wa nyumba ya Bwana.

Mtolee Bwana kwa kuchangia ujenzi wa kanisa hili.  Kwa mchango wasiliana na:
1.  Mwinjilisti Samwel Mwakalobo, Simu Na. 0786/0767-325726
2.  Aggrey Mwendamseke (Mzee wa Kanisa) Simu Na. 0754/0782/0715 - 307194

DR. JOYCE NDALICHAKO ELECTED NEW PRESIDENT FOR AFRICA'S EAA


THE Executive Secretary for the National Examination Council of Tanzania (NECTA), Dr Joyce Ndalichako, has been elected new President for the Association for Educational Assessment in Africa (AEAA).

Dr. Ndalichako was chosen during the just ended 31st AEAA conference organised by NECTA.

The NECTA Executive Secretary who previously has been serving as the Vice-President of the AEAA will be in-charge of the Pan African education body for one year.

“During my tenure I will make sure that education assessors on the continent are well trained under the ‘capacity building’ initiative and would like to encourage Tanzanians to make good use of the country’s position at AEAA to also pursue further training,” stated Dr Ndalichako.

She pointed out that since Tanzania has only one examination body, exam assessors in the country needed other platforms from which they can get developed technically and academically, even if it means to seek assistances from international organisations as the AEAA.

The new president also expressed gratitude to members of the association as well as the delegation at the 31st conference for electing her on the highest position.

Education experts from all over the continent were meeting here for five-day 31st Annual Conference of the AEAA running under the theme: Enhancing Assessment Practices for Quality Education.

The Second Vice-President in the Revolutionary Government of Zanzibar, Amb. Seif Ali Iddi opened the conference on Monday; calling for African countries to evaluate the success of education delivery.

There is a need to innovate assessment practices which provide reliable results reflecting the candidate’s attainment of the intended learning objectives.

Countries that participated in the conference include Mozambique, Gambia, Kenya, Uganda, Zambia, South-Africa and the host Tanzania, as well as overseas participants from the United States (US), United Kingdom (UK), Germany and China.

Tanzania is hosting the AEAA conference for the fifth time having played the same role previously in 1983, 1987, 1992 and 2002, before hosting the event again this year (2013) in Arusha.

Next year, the 32nd conference will be held in Lusaka, Zambia.  This year's conference addressed, among other topics, the role of classroom assessment practices in improving quality of education; enhance teachers' capacity in assessments, for improving the quality of education and the impact of Information and Communication Technology in educational assessment.

The week-long meeting also dealt with the relationship between continuous assessment and final examination scores: Implications on quality of education, dynamics of languages in assessment and learning outcome and the challenges associated with assessment of soft skills for quality education. The participants also debated about innovations in assessment practices and their implications in improving quality of education, as well as the impact of security breach on quality of examination and assessment.

Founded in 1982, the AEAA, with main offices in Lusaka, Zambia, operates along the main guiding policy of 'Harmonisation of Educational Assessment on the African continent.'

The major objectives for the AEAA include; promoting co-operation amongst examining and assessment bodies in Africa; encourage relevant examining and assessment activities among members and sponsoring international participation in the field of educational testing and examining.

Source: dailynews.co.tz

MWAKYEMBE AWATIMUA WALIOMSAIDIA AGNESS MASOGANGE KUPITISHA MADAWA YA KULEVYA KATIKA UWANJA WA NDEGE WA JNIA, DSM


Dkt. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Uchukuzi
 
 Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa agizo kwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) kuwafukuza kazi na kuliagiza jeshi la Polisi nchini kuwaunganisha na wengine kwenye kesi mahakamani ili kujibu mashitaka ya jinai, wale wote waliohusika katika kuwasaidia Agness Gerald na mwenziye Melissa Edward kupitisha dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine "TIK" au "Meth" au "USAN" kilogramu 180 kuelekea Afrika Kusini Julai 5 mwaka huu, ambako walikamatwa katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Oliver Tambo nchini humo.

Waziri Mwakyembe ametoa agizo hilo jana, ofisini kwake, mbele ya waandishi wa habari wakati alipowaita ili kuufahamisha umma kuhusu hatua zilizochukuliwa na Wizara yake kuhusu suala la dawa za kulevya.

Waliofukuzwa ni Koplo Ernest, Yusuph, Jackson, Juliana Tadei na Mohamed ambao walihusika katika kuwasaidia Agnes Gerald (Masogange) na mwenzake Mellisa kupitisha dawa za kulevya kuelekea Afrika Kusini ambako walikamatwa.


Agness Gerald a.k.a. Masogange

MALIPO YA WAKAZI WA MLOGANZILA KUKAMILIKA SEPTEMBA, 2013 - PINDA



WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema atasimamia suala la fidia kwa wakazi 91 waliobakia kulipwa katika eneo la Mloganzila nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ili liweze kuisha mwezi ujao na malipo yaandaliwe mara baada ya taratibu zote kukamilika.

Alikuwa akizungumza katika mkutano wa dharura jana jioni (Ijumaa, Agosti 16, 2013) uliosababishwa na wakazi wa Mloganzila na vitongoji vyake ambao wanadai fidia ili wapishe mradi mkubwa wa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Tiba na Hospitali unaotarajiwa kuanza karibuni.

Kwa mujibu wa ratiba yake, Waziri Mkuu alikuwa ameenda Mloganzila kukagua eneo la mradi huo na kupata maelezo kwa watendaji kuhusu kusuasua kwa mradi huo.

Alisema kwa utaratibu wa kawaida wa makusanyo ya Serikali, suala hilo linaweza kufanyika mwezi Oktoba na malipo yao yataanza kupatikana Novemba mwaka huu lakini kwa vile amesikiliza hoja zao, atafuatilia na kuhakikisha malipo hayo yanawahi kidogo.

“Kwa tarehe ya leo, hata nifanye nini hatuwezi kuwahi kukamilisha malipo haya mwisho wa mwezi huu (Agosti). Na hii ni kwa mujibu wa taratibu za kifedha. Nitafuatilia ili mpewe kipaumbele katika makusanyo ya mwezi ujao,” alisema.

Kwa mujibu wa tathmini iliyofanyika mwaka 2008 na kurudiwa mwaka 2011, wakazi hao wanatakiwa kulipwa sh. milioni 980.6/-. Wakazi wengine 2,533 walikwishafanyiwa tathmini na kulipwa fidia ya sh. bilioni 9.55/-.

Katika mkutano huo baadhi ya wakazi waliopewa nafasi kuelezea kero zao, walilalamikia kuhusu viwango vidogo vya fidia walizopewa, kutolipwa fidia kwa baadhi ya wakazi ambao walikwisha kufanyiwa tathmini, na malipo yaliyotolewa kutolingana na ukubwa wa maeneo yao waliyokuwa wakiishi.

Akijibu hoja hizo, Waziri Mkuu Pinda alisema chanzo cha mgogoro huo ni baadhi ya wakazi kudai walipwe fidia ya ardhi wakati eneo hilo si lao bali lilikuwa ni mali ya kiwanda cha kusindika nyama cha Tanganyika Packers lililokuwa likitumika kunenepesha mifugo kabla haijapelekwa kiwandani.

“Tatizo hapa ni matumizi mabaya ya ardhi. Waliopewa eneo hawakuliendeleza, waliliacha wazi kwa muda mrefu na tena hawakulizungushia uzio. Hali hii ilileta vishawishi kwa watu kuanza kujipenyeza kushoto na kulia,” alisema.

Alisema anakubaliana na madai ya wakazi 91 kutolipwa fidia zao lakini wale 2,533 lazima wakubali kwamba tayari walikwishalipwa fidia ya maendelezo ya eneo walilokuwa wakiishi.

Akizungumzia kuhusu mradi wa chuo na hospitali ya Mloganzila, Waziri Mkuu Pinda aliitaja mipango ya haraka ya kuendeleza eneo hilo kuwa ni kutengeneza barabara ya kilometa 12 itakayounganisha eneo kuu la chuo hicho. ”Huduma nyingine ambazo ni lazima zipatikane haraka ni maji na umeme. Ili mradi uende kwa kasi, ni lazima hizi huduma zipatikane mapema,” alisema.

Aliwapongeza wakazi hao kwa uamuzi wao wa kukubali kupisha mradi wa ujenzi wa chuo hicho uendelee kwa vile wanatambua kwamba una maslahi kwa Taifa. ”Nimefurahi kusikia kwamba mnataka mradi huu uendelee kwa vile mnatambua umuhimu wake,” aliongeza.

Mara baada ya mkutano huo, Waziri Mkuu alipokea maelezo kuhusu maandalizi ya ujenzi wa mradi huo kutoka kwa watendaji wa taasisi za Serikali kama TANROADS, TANESCO, Wizara ya Maji, Wizara ya Elimu na Kamishna wa Ardhi.

Katika mkutano huo, Waziri Mkuu alifuatana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid. Wengine ni Wakuu wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM

Friday, August 16, 2013

KAMATI YA UCHAGUZI KUJADILI SIMBA, YANGA





                           TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
                                            Agosti 16, 2013

 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemwandikia Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ili kufanya uamuzi wenye manufaa kwa washabiki wa mpira wa miguu baada ya tarehe ya uchaguzi aliyotangaza kuingiliana na mechi ya watani wa jadi (Simba na Yanga) ya Ligi Kuu ya Vodacom.

Sekretarieti ya TFF imepokea maoni kutoka kwa wapenzi mbalimbali wa mpira wa miguu wakiomba matukio hayo mawili (Uchaguzi wa TFF na mechi ya Simba na Yanga) yafanyike katika siku tofauti.

Wakati Kamati ya Uchaguzi inatangaza uchaguzi kufanyika Oktoba 20 mwaka huu tayari ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom ilikuwa imeshatoka, na ikionesha kuwa timu ambazo zina historia ya kipekee katika mpira wa miguu zitacheza siku hiyo.

Sekretarieti imelazimika kumwandikia Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi kwa vile yeye na kamati yake ndiye wenye mamlaka ya kuitisha Mkutano wa Uchaguzi. Huko nyuma TFF imeshafanya mikutano huku kukiwa na mechi za timu ya Taifa (Taifa Stars), jambo ambalo liliwezekana kutokana na mikutano hiyo kuwa na ajenda moja tu.

Tayari Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Hamidu Mbwezeleni ameitisha kikao cha kamati yake kujadili barua hiyo ya sekretarieti.

COCA COLA YATOA MIPIRA 100, FULANA 800
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa shukrani kwa kampuni ya Coca Cola kwa kukabidhi fulana 800 na mipira 100 kwa ajili ya ngazi ya mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 15 ngazi ya mikoa yanayoanza Septemba Mosi mwaka huu.

Coca Cola ndiyo inayodhamini mashindano hayo yaliyoanzia ngazi ya wilaya ambapo mwaka huu yatachezwa kwa kanda na baadaye fainali itakayochezwa kuanzia Septemba 7-14 mwaka huu jijini Dar es Salaam ikishirikisha mikoa 16 itakayokuwa imefanya vizuri katika ngazi ya kanda.
Kila mkoa utapata fulana 25 na mipira mitatu ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya timu zao kwa ajili ya michuano hiyo ngazi ya kanda itakayomazika Septemba 6 mwaka huu.

Kanda hizo ni Mwanza itakayokuwa na timu za mikoa ya Geita, Kagera, Kigoma, Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Tabora. Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Singida inaunda Kanda ya Arusha.

Zanzibar itakuwa na Kaskazini Pemba, Kusini Pemba na mikoa miwili ya Unguja wakati Kanda ya Dar es Salaam ina Ilala, Kinondoni, Lindi, Mtwara, Temeke na mkoa mmoja wa Unguja.

Kanda ya Mbeya inaundwa na Iringa, Katavi, Mbeya, Njombe, Rukwa na Ruvuma wakati Dodoma, Morogoro, Pwani na Tanga zinaunda Kanda ya Morogoro.

Mwanza itatoa timu nne kucheza hatua ya fainali wakati kanda nyingine za Arusha timu mbili, Zanzibar (2), Mbeya (3) na Kanda ya Morogoro itaingiza timu mbili.

Wakati huo huo, semina ya makocha 32 wa timu za mikoa zitakazoshiriki michuano ya U15 FIFA Copa Coca-Cola iliyokuwa ikiendeshwa na mkufunzi Govinder Thondoo kutoka Mauritius inafungwa leo (Agosti 16 mwaka huu) saa 9 alasiri kwenye ukumbi wa Msimbazi Center, Dar es Salaam.

RAMBIRAMBI MSIBA WA MWANDISHI GRACEMO BAMBAZA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha aliyekuwa mwandishi wa habari za michezo wa Radio ABM ya Dodoma, Gracemo Bambaza kilichotokea Agosti 14 mwaka huu katika Hospitali ya Ocean Road, Dar es Salaam.

Msiba huo ni mkubwa katika sekta ya habari na mpira wa miguu kwani Bambaza kwa kipindi chote akiwa mwandishi alikuwa akifanya kazi nasi, hivyo mchango wake katika mpira wa miguu tutaukumbuka daima.

Bambaza aliyezaliwa mwaka 1973 na ambaye pia aliwahi kufanya kazi katika vituo vya redio vya Wapo cha Dar es Salaam na Pride cha Mtwara amesafirishwa jana (Agosti 15 mwaka huu) kwenda Karagwe mkoani Kagera kwa ajili ya mazishi.

TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Bambaza, ABM Radio na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

Mungu aiweke roho ya marehemu Bambaza mahali pema peponi. Amina

TIKETI MECHI YA YANGA, AZAM KUUZWA ASUBUHI
Tiketi kwa ajili ya mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Yanga na Azam itakayochezwa kesho (Agosti 17 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam zitaanza kuuzwa saa 3 asubuhi.

Vituo vitakavyouza tiketi hizo Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Dar Live Mbagala na BMM Barber Shop iliyoko Sinza Madukani.

Katika vituo hivyo tiketi zitauzwa katika magari maalumu. Magari yote yanayouza tiketi yatahamia uwanjani saa 7 kamili mchana.

Viingilio katika mechi hiyo ni sh. 7,000 kwa viti vya rangi ya kijani na bluu wakati viti vya rangi ya chungwa ni sh. 10,000. Watakaiongia viti vya VIP C watalipa sh. 15,000, viti vya VIP B ni sh. 20,000 wakati VIP A watalipa sh. 30,000.

                                   Boniface Wambura
                                          Ofisa Habari
                  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

KIBONZO CHA LEO................!!


NGASA KUCHEZEA YANGA BAADA YA KIFUNGO CHA MECHI SITA


  
KAMATI YAPITIA USAJILI, NGASA KUCHEZEA YANGA
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imepitia usajili wa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom na kumuidhinisha Mrisho Ngasa kuchezea timu ya Yanga baada ya kukamilisha usajili wake.

Hata hivyo, Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa imebaini kuwa Ngasa alisaini mkataba mwingine Simba (katika kipindi ambacho alikuwa na mkataba na Azam) ambapo anatakiwa kurejesha fedha alizopokea (sh. milioni 30) pamoja na fidia ya asilimia 50 (sh. milioni 15) ya fedha hizo kwa Simba.

Kamati pia imemfungia mechi sita za mashindano (kuanzia mechi ya Ngao ya Jamii), na anatakiwa awe amelipa fedha hizo ndani ya kipindi hicho cha kukosa mechi hizo. Akishindwa, hataruhusiwa kucheza hadi atakapolipa fedha hizo.

Vilevile Kamati imepitia pingamizi zote zilizowasilishwa kuhusu usajili wa wachezaji, kukatiza mikataba ya wachezaji na kuzitaka klabu husika ziwe zimetatua masuala hayo hadi Alhamisi (Agosti 22 mwaka huu).

Kwa upande wa wachezaji wa kigeni, Kamati imeagiza wasiruhusiwe kucheza hadi watakapopata Hati za Uhamisho wa Kimataifa (ITC) pamoja na vibali vya kufanya kazi nchini (work permits).

Kamati hiyo itakutana tena Ijumaa (Agosti 23 mwaka huu) ili kupata ripoti za pingamizi ilizoagiza ziwe zimefanyiwa kazi hadi Agosti 22 mwaka huu na kutoa uamuzi kwa pande ambazo hazikuafikiana.

UCHAGUZI TFF SASA KUFANYIKA OKTOBA 27
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kuzingatia mamlaka iliyonayo katika kifungu cha 10(6) cha Kanuni za Uchaguzi za TFF inasogeza mbele tarehe ya uchaguzi wa TFF kutoka Oktoba 20 mpaka Oktoba 26 na 27 mwaka huu.

Sababu za kusogeza mbele uchaguzi ni kutokana na ukweli kuwa Oktoba 20 mwaka huu uongozi wa TFF utakuwa na shughuli nyingi za maandalizi ya mechi ya Simba na Yanga, na hivyo haitawezekana kusimamia shughuli za Mkutano Mkuu wa Uchaguzi kwa wakati mmoja na mchezo huo.

Siku ya mwisho ya kampeni itakuwa Oktoba 25 mwaka huu. Ukiondoa  mabadiliko hayo ya tarehe ya uchaguzi wa viongozi wa TFF, ratiba ya mchakato wa uchaguzi na itabaki kama ilivyotangazwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF katika mkutano wake na waandishi wa habari Agosti 24 mwaka huu.

Pia Kamati imeamua kuwa uchaguzi wa Bodi ya Ligi utabakia kuwa Oktoba 18 mwaka huu kama ilivyopangwa awali.

Kamati imesema inaamini wahusika wote watapokea vizuri mabadiliko hayo na inasikitika kwa usumbufu utakaosababishwa na mabadiliko hayo.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

HAPPY BIRTHDAY UNCLE AGGREY MWENDAMSEKE

May you live to blow 100+ candles. 
HAPPY BIRTHDAY.

Thursday, August 15, 2013

YANGA NA AZAM KUVAANA MECHI YA NGAO YA JAMII J’MOSI



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Agosti 15, 2013

YANGA, AZAM KUVAANA NGAO YA JAMII J’MOSI

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom, Yanga na makamu bingwa Azam wanavaana keshokutwa (Jumamosi) kwenye mechi ya Ngao ya Jamii(Community Shield) kuashiria uzinduzi wa msimu mpya wa 2013/2014.

Mechi hiyo inayotarajiwa kuwa kivutio kwa wapenzi wa mpira wa miguu nchini itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni ambapo mshindi atakabidhiwa ngao.

Iwapo dakika 90 za mechi hiyo hazitatoa mshindi, timu hizo zitatenganishwa kwa mikwaju ya penalti huku asilimia 10 ya mapato ya mechi hiyo yakiendakwa kituo cha kulelea watoto cha SOS.

Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 7,000 kwa viti vya rangi ya kijani na bluu wakati viti vya rangi ya chungwa ni sh. 10,000. Watakaiongia viti vya VIPC watalipa sh. 15,000, viti vya VIP B ni sh. 20,000 wakati VIP A watalipa sh. 30,000.


LIGI DARAJA LA KWANZA KUANZA SEPT 14

Michuano ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inayoshirikisha timu 24 zilizogawanywa katika makundi matatu msimu huu (2013/2014) itaanza kutimua vumbi Septemba 14 mwaka huu.

Kila timu itakayoongoza kundi lake katika ligi itakayochezwa kwa mikondo miwili (nyumbani na ugenini) ndiyo itakayopanda daraja kucheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2014/2015.

Mechi za ufunguzi kwa kundi A zitakuwa kati ya Tessema vs Green Warriors(Uwanja wa Karume, Dar es Salaam) wakati Septemba 15 mwaka huu ni Transit Camp vs Polisi Dar (Uwanja wa Mabatini, Pwani), Ndanda vs Friends Rangers (Uwanja wa Nangwanda, Mtwara) wakati Villa Squad vs African Lyon itachezwa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
 
Kundi B ni Burkina Faso vs Polisi Moro (Uwanja wa Jamhuri, Morogoro), Mkamba Rangers vs Lipuli (Uwanja wa CCM Mkamba, Morogoro), Majimaji vs Mlale JKT (Uwanja wa Majimaji, Songea) wakati Septemba 15 mwaka huu Kimondo SC vs Kurugenzi (Uwanja wa Sokoine, Mbeya).

Mechi za ufunguzi kundi C ni Polisi Mara vs Polisi Dodoma (Uwanja wa Karume,Musoma), Kanembwa JKT vs Polisi Tabora (Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma), Stand United vs Mwadui (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga), na Pamba vs Toto Africans (Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza).

Mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo utamalizika Oktoba 26 mwaka huu wakati wa pili utamalizika Machi 22 mwakani.(Ratiba imeambatanishwa)

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) 

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU MATUMIZI YA MIFUKO YA PLASTIKI NCHINI - DKT. TEREZYA HUVISA

Picha ya juu na chini ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Mamaku wa Rais Mazingira, Dkt. Terezya Huvisa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo kuhusu tamko la serikali la kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki hapa nchi.
(Picha na Ofisi ya Makamu ya wa Rais.)



SERIKALI imepiga marufuku uingizaji, utengenezaji, uuzaji na utumiaji wa mifuko ya plastiki kutokana na mifuko hiyo kusababisha uchafu na madhara kwa binadamu.

Hayo yameelezwa leo na Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais(mazingira) Dkt. Terezya Huvisa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Dkt. Huvisa ameeleza kuwa Serikali imeamua kuchukua hatua hiyo ili kupunguza ama kuondoa kabisa tatizo la kusambaa kwa taka za mifuko ya plastiki ambayo baada ya matumizi yake huishia kwenye uchafuzi wa mazingira.

Aidha, dkt. Huvisa amesisitiza kuwa zuio hilo linahusu mifuko yote ya plastiki ya kubebea bidhaa toka madukani, sokoni na majumbani isipokuwa mifuko yenye unene wa maikron 100 inayooza (bio-digradable) na vifungashio vya bidhaa mbalimbali kama vile vifaa vya mahospitalini.

"Marufuku hii inapaswa kuzingatiwa na wenye viwanda, wenye maduka na wananchi wote kwa ujumla ili kutokomeza kuenea kwa taka zinazotokana na mifuko ya plastiki kwenye mazingira." amesema Dkt. Huvisa.

Vile vile Dkt. Huvisa amesema kuwa jitihada zinatakiwa zifanywe ili kuhakikisha kuwa marufuku hii inazingatiwa na kwamba misako ya watu wanaofanya biashara ya mifuko hii itafanyika katika maeneo yote ndani ya nchi yetu, na watakaokiuka watachukuliwa hatua, ikiwa ni pamoja na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Imeelezwa kuwa madhara yanayosababishwa na mifuko ya plastiki ni pamoja na uharibifu wa udongo unaotokana na kuunguzwa na plastiki hizo na hivyo kusababisha madhara ya kiafya kwa binadamu na wanyama, kutooza kirahisi kwa njia za kiasili (non-biogradable), kuzagaa katika mito, maziwa, bahari na nchi kavu hivyo kuhatarisha maisha ya viumbe hai wanaoishi katika mazingira hayo.

KIBONZO CHA LEO..........!!


BENKI YA CRDB YAZINDUA MPANGO WA UTOAJI MIKOPO YA NYUMBA UITWAO 'JIJENGE'


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki  ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza wakati wa uzinduzi wa mikopo ya nyumba ijulikanayo kwa jina ya ‘JIJENGE’ itakakayoanza kutolewa na benki hiyo. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.

Meneja wa benki ya CRDB anayeshughulikia mikopo ya nyumba 'JIJENGE',' Silas Katemi akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mikopo hiyo.

Baadhi ya Maofisa wa benki ya CRDB wakiwa na wageni waalikwa katika hafla hiyo.

MKUTANO WA MPANGO WA "MATOKEO MAKUBWA SASA" KATIKA SEKTA YA ELIMU WAFANYIKA JIJINI DSM

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mhe Shukuru Kawambwa (aliyesimama) akitoa hotuba wakati akifungua mkutano wa wakaguzi wakuu wa Shule kanda na Wilaya hapa nchini.  Lengo la mkutano huo ni kuandaa uzinduzi wa mpango wa “Matokeo Makubwa Sasa” katika sekta ya Elimu. Kushoto ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo. Mkutano huo umefanyika jana Agosti 14,2013 kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.

Wakuu wa shule za sekondari na shule za msingi wakiwa kwenye mkutano huo wa kuandaa uzinduzi wa mpango wa “Matokeo Makubwa Sasa” katika sekta ya Elimu uliofanyika  Agosti 14, 2013 kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.

Wakuu wa shule za sekondari na shule za msingi wakiwa kwenye mkutano huo wa kuandaa uzinduzi wa mpango wa “Matokeo Makubwa Sasa” katika sekta ya Elimu uliofanyika  Agosti 14, 2013 kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Wakuu wa shule za sekondari na shule za msingi wakiwa kwenye mkutano huo jana wa kuandaa uzinduzi wa mpango wa “Matokeo Makubwa Sasa” katika sekta ya Elimu, wakipata vitabu vya mwongozo wa utoaji wa huduma za kielimu kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi.

Wednesday, August 14, 2013

SERIKALI YATAHADHARISHWA KUTOKEA KWA MIFARAKANO KATI YA WAFUGAJI NA MAKABILA YA WAFUGAJI AMBAYO YAMEVAMIA KATIKA KIJIJI CHA ULAYA MBUYUNI

 Bi Sharifa Mustafa mkazi wa Ulaya Mbuyuni wilayani Kilosa mkoani Morogoro akionyesha Ng'ombe wake ambaye amepatiwa na shirika la kimataifa la Heifer kwa lengo la kujikwamua kiuchumi  

Dakta Zengo Mikomagwa Mshauri wa mifugo Heifer International akizungumza na waandishi katika kijiji cha Ulaya Mbuyuni wilayani Kilosa mkoani Morogoro kuhusu miradi inayoendeshwa na shirika hilo hapa nchini.


Wanakikundi wa Mshikamano ambao wamebahatika kupata Ng'ombe wa maziwa kutoka shirika la kimataifa la Heifer International(PICHA ZOTE NA IPSHA MEDIA).

SERIKALI IMETAHADHARISHWA KUTOKEA KWA MIFARAKANO KATI YA WAFUGAJI NA MAKABILA YA WAFUGAJI AMBAYO YAMEVAMIA KATIKA KIJIJI CHA ULAYA MBUYUNI KILICHOPO WILAYANI KILOSA MKOANI MOROGO AMBAPO MIFUGO HIYO IMEKUWA IKIARIBU MAZAO YAO NA VYAZO VYA MAJI JAMBO AMBALO HAWATO WEZA KULIVUMIA LIENDELEE.

WAKIZUNGUMZA KIJIJINI HAPO WAKAZI WA ENEO HILO AMBAO WAPO KATIKA MRADI WA UFUGAJI WA NG'OMBE WA KISASA CHINI YA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA HEIFER INTERNATIONAL WAMESEMA KUWA KUTOKANA NA MIFUGO YA WAVAMIZI AMBAO WANAFUGA NG'OMBE WA KIENYEJI NA HIVYO KUSABABISHA UHARIBIFU MKUBWA HATA WAO WAKO HATARINI KUKOSA MAJANI YA MALISHO YA NG'OMBE WAO AMBAO HAWATOKI MABANDANI NA HIVYO KUIOMBA SERIKALI KUCHUKUA HATUA ZA HARAKA ZA KUWAONDOA WAVAMIZI HAO KATIKA KIJIJI CHAO ILI WASIENDELEE KUFANYA UHARIBIFU HUO.

AWALI AKIZUNGUMZIA TATIZO LA MALISHO YA MIFUGO MSHAURI WA MASUALA YA MIFUGO KUTOKA SHIRIKA LA HEIFER AMESEMA KUWA SHIRIKA LAKE LIMEKUWA LIKIFANYA JITIHADA MBALIMBALI ZA KUHAKIKISHA KUWA MIFUGO WANAYO WAPATIA WAFUGAJI HAO AMBAO PIA NI WAKULIMA INAPATA MALISHO BORA AMBAPO WAMEANZA KUWAPATIA MAFUNZO YA MRADI WA SUKUMA VUTA AMBAO  UNAWAWEZESHA WAFUGAJI HAO KULIMA MAZAO YAO NA MAJANI YA MALISHO KATIKA SHAMBA MOJA.

POLISI WAMKAMATA ALIYEMUUA BILIONEA ERASTO MSUYA



ARUSHA
Polisi wamefanikiwa kumtia mbaroni mfanyabiashara tajiri wa madini ya Tanzanite huko Mirerani anayetajwa kuwa ndiye aliyepanga na kukodi watu waliomuua bilionea Erasto Msuya.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zimedai kuwa mfanyabiashara huyo alikamatwa mwishoni mwa wiki na jana na juzi alikuwa akihojiwa na makachero.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, mfanyabiashara huyo ndiye aliyetoa fedha za kununulia pikipiki mbili zilizotumika katika mpango huo na pia alitoa fedha kwa ajili ya kununua simu mpya na laini mpya.

“Tumewakamata watu wametupa mwanga mzuri na huyo mfanyabiashara ndiye aliyetoa fedha za kununua pikipiki na siku moja kabla ya tukio zilihifadhiwa nyumbani kwake,” alidokeza polisi mmoja.

Habari hizo zimedai kuwa polisi pia imewahoji mawakala wa kampuni za simu ambao walitumiwa kusajili laini mpya za simu zilizotumika kumpigia marehemu na kutumika kupanga mauaji hayo.

Pikipiki hizo mbili, zilinunuliwa siku moja kabla ya tukio zikahifadhiwa nyumbani kwa mfanyabiashara huyo hadi siku iliyofuata ambapo aliwakabidhi wauaji na zote zimekamatwa.

Mahojiano kati ya mfanyabiashara huyo na Polisi yamekuwa yakifanyika kwa siri na katika kituo cha polisi (jina tunalo) na kwamba mambo ni mazuri.

Source: mwananchi.co.tz

TFF KUFANYA UCHAGUZI WA KAMATI MPYA YA UTENDAJI OKTOBA 18



Boniface Wambura

Na Boniface Wambura, TFF

KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetoa tangazo la uchaguzi wa Kamati ya mpya ya Utendaji ambao utafanyika Oktoba 20 mwaka huu. Pia Kamati hiyo imetoa tangazo za uchaguzi wa Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPL Board) ambao utafanyika Oktoba 18 mwaka huu.

Akitangaza mchakato huo wa uchaguzi leo (Agosti 14 mwaka huu) jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Hamidu Mbwezeleni amesema nafasi zitakazogombewa kwa upande wa TFF ni Rais, Makamu wa Rais na wajumbe 13 wa Kamati ya Utendaji wakiwakilisha kanda mbalimbali.

Fomu kwa wagombea zitatolewa kuanzia Agosti 16 mwaka huu kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 10 kamili jioni kwenye ofizi za TFF. Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni Agosti 20 mwaka huu. Fomu kwa nafasi ya Rais ni sh. 500,000, Makamu wa Rais ni sh. 300,000 wakati wajumbe ni sh. 200,000.

Mbwezeleni amesema kwa wale ambao walilipia fomu katika mchakato uliofutwa na wanakusudia kugombea nafasi zilezile walizolipia, hawatalipia tena ada ya fomu husika bali watatakiwa kuambatanisha risiti za malipo wakati wa kurudisha fomu za maombi hayo ili kuthibitisha malipo yao.

Kwa upande wa uchaguzi wa TPL Board, fomu zitaanza kutolewa Agosti 16 hadi 20 mwaka huu, na nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti ambapo ada ni sh. 200,000 wakati wajumbe wa Bodi ada ni sh. 100,000.

KAMATI YA SHERIA TFF KUPITIA USAJILI IJUMAA


Bw. Alex Mgongolwa
 
Na Boniface Wambura, TFF

KAMATI ya Sheria na Hadhi za Wachezaji iliyokuwa ikutane jana (Agosti 13 mwaka huu) na leo (Agosti 14 mwaka huu) kupitia usajili wa wachezaji kwa klabu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza sasa itakutana keshokutwa (Agosti 16 mwaka huu) saa 4 asubuhi.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Alex Mgongolwa amepanga tarehe hiyo mpya baada ya kikao cha jana kushindwa kupata akidi. Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ina wajumbe saba, na ili kikao kiweze kufanyika ni lazima wapatikane wajumbe kuanzia wanne.

MWISHO WA KUPOKEA MAONI YA MABARAZA YA KATIBA YA ASASI, TAASISI NA MAKUNDI YA WATU WENYE MALENGO YANAYOFANANA NI TAREHE 31 AGOSTI, 2013


Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mkuu mstaafu Augustino Ramadhani (aliyesimama) akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara katika mkutano ulioitishwa na Tume ili kuijadili na kuitolea maoni Rasimu ya Katiba Mpya wakati wa mkutano uliofanyika Wilayani humo hivi karibuni. Kulia ni Mjumbe wa Tume, Bw. Yahya Msulwa.

Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bi. Salma Maulid (kulia) akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi mkoani Kilimanjaro katika mkutano ulioitishwa Tume wa kuijadili na kuitolea maoni Rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume hiyo. Kushoto ni Mjumbe wa Tume, Profesa Mwesiga Baregu.
************************* 
TUME ya Mabadiliko ya Katiba inapenda kuwakumbusha wananchi kuwa mwisho wa kupokea maoni kuhusu Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa asasi, taasisi, na makundi ya watu yenye malengo yanayofanana ni siku ya Jumamosi, tarehe 31 Agosti 2013.

Tarehe 31 Agosti, 2013 ilipangwa na kutangazwa katika Mwongozo Kuhusu Mabaraza ya Katiba ya Asasi, Taasisi na Makundi ya Watu Wenye Malengo Yanayofanana uliotolewa na Tume na ulianza kutumika tarehe 01 Juni 2013.

UTARATIBU WA KUWASILISHA MAONI
Kwa mujibu wa Aya Na. 4.0 ya mwongozo huo, Asasi, Taasisi na Makundi ya Watu wenye Malengo yanayofanana yanatakiwa kuwasilisha kwa Tume maoni hayo kwa njia ya randama, barua, andiko au muhtasari wa makubaliano, n.k.

Hivyo basi Asasi, Taasisi au Makundi ya watu wenye Malengo yanayofanana yanaweza kupeleka maoni yao moja kwa moja katika ofisi za Tume zilizopo jijini Dar es Salaam, Mtaa wa Ohio au Zanzibar, Mtaa wa Kikwajuni, Gofu Jengo la Mfuko wa Barabara. Aidha, wanaweza kutuma maoni hayo kwa kutumia barua pepe ambayo ni katibu@katiba.go.tz au anuani zifuatazo:

1.Tume ya Mabadiliko ya Katiba, S.L.P. 1681, Dar es Salaam; au
2.Tume ya Mabadiliko ya Katiba, S.L.P. 2775, Zanzibar.

Muda wa Kuwasilisha Hautaongezwa
Tume inapenda kusisitiza kuwa muda wa kupokea maoni kuhusu Rasimu ya Katiba hautaongezwa na kuwa Asasi, Taasisi na Makundi ya watu wenye Malengo yanayofanana kuzingatia tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maoni iliyopangwa na Tume.

RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AKABIDHIWA JEZI NAMBA 10 YA BARCELONA NA TBL


 Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bi. Kushilla Thomas akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete jezi iliyosainiwa na wachezaji wote wa timu ya FC Barcelona Ikulu jijini Dar es salaam jana ikiwa ni kutambua mchango wake katika kuendeleza soka na ikiwa ishara ya kutambua ushirikiano wa kihistoria kati ya Castle Lager na FC Barcelona uliosainiwa hivi karibuni huko Camp Nou Hispania. Wanaotazama ni Meneja Mauzo wa TBL Kanda ya Kusini James Bokella (wa kwanza kulia) na Meneja Masoko wa TBL Bi. Natalia Celani (wa pili kulia). Na kushoto ni Meneja wa Castle Lager, Kabula Nshimo na Aggrey Marealle, Mkurugenzi wa Executive Solutions washauri wa mahusiano wa TBL. 
 Wakiwa katika picha ya kumbukumbu mara baada ya makabidhiano.

 Jezi hii sasa iliwekwa katika Fremu maalum ambayo itawekwa ukutani.

MFUKO WA PENSHENI WA PPF WAELEZEA MAFANIKIO YAKE

  Meneja Uratibu Ofisi za Kanda toka Mfuko wa Pensheni wa PPF Mbarouk Magawa akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya namna mwanachama anavyoweza kupata taarifa mbalimbali za michango yake.
 Meneja Uwekezaji toka Mfuko wa Pensheni wa PPF Selestine Some akielezea mafanikio mbalimbali ambayo mfuko umepata tangu kuanzishwa kwake miaka 35 iliyopita 

Afisa Uhusiano toka Mfuko wa Pensheni wa PPF Lulu Mengele (kushoto) akiwaeleza waandishi wa habari  mafanikio ya mfuko na aina za mafao ambazo  mfuko inatoa kwa wanachama wake, kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Zamaradi Kawawa.



Mfuko wa Pensheni wa PPF  ni Mfuko mkongwe hapa nchini, ulianzishwa mwaka 1978 kwa Sheria ya Mfuko wa Pensheni wa PPF Sura na. 372 kwa madhumuni ya kutoa mafao ya pensheni na mafao mengine yanayoendena na hayo kwa wafanyakazi wote walio katika sekta rasmi na zisizo rasmi.

majukumu ya mfuko

PPF ina majukumu yafuatayo:-

i)     kuandikisha wanachama,

ii)   kukusanya michango,

iii)  kuwekeza michango inayokusanywa na

iv) kulipa mafao ya pensheni na mafao mengine yanayoendana na hayo kwa wanachama wake.

WIGO WA UANACHAMA

Mfuko unaandikisha wanachama kutoka katika sekta zote za uchumi mashirika ya umma, makampuni binafsi, waliojiajiri wenyewe na sekta isiyo rasmi

Mafao ya PPF: Mfuko wa PPF una mafao saba

baadhi ya mafao ambayo Mfuko unatoa ni

Mafao ya Pensheni ambapo hutolewa pale ambapo mwanachama anapokuwa amechangia kwa kipindi cha miaka 10 au zaidi na amefikia umri kustaafu yaani miaka 55 mpaka 60.Na awe ameondoka kwenye ajira.
Mpaka sasa PPF ina wastaafu  wapatao 25,896 na tunalipa kila mwezi Billioni 3.7

Hii ni kwa mafao ya uzeeni tu mnaweza kuona jinsi tunavyosaidia kuondoa umaskini na kukuza uchumi wa nchi.

Mafao ya Ugonjwa
 Hutolewa pale ambapo mwanachama wa PPF anapokuwa ameondoka kazini kwa sababu za ugonjwa na imedhibitishwa na Daktari kwamba kweli hawezi kufanya kazi tena

Mafao ya Elimu:
Hutolewa pale ambapo mwanachama wa PPF anapokuwa amefariki dunia baada ya kuchangia kwa muda wa miaka 3 au zaidi.

Fao hili hutolewa kwa watoto wa mwanachama wasiozidi 4 kwa kulipia gharama ya elimu ya chekechea mpaka kidato cha nne.

Kwa kutambua umuhimu wa elimu kuanzia mwakani 2014 Mfuko unaongeza muda wa kuwasomesha watoto mpaka kidato cha sita.

Tunalipa mmoja kwa mmoja kwenye shule za watoto wanachama