Pages

Saturday, August 17, 2013

MKUTANO WA MWAKA WA WANAHISA WA KAMPUNI YA GESI TANZANIA (TOL) WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM


Bodi ya wakurugenzi wa kampuni  ya TOL Gases Limited wakiwa katika mkutano na wanahisa wa kampuni hiyo uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya TOL Gases Limited Bw. Harold Temu akihojiwa na mwandishi wa habari wa ITV Emanuel Buhohela katika mkutano huo ambao umefanyika jana jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washiriki wa Mkutano mkuu wa mwaka wa Wanahisa wa Kampuni ya utengenezaji wa Gesi ya TOL wakijiandikisha tayari kwa mkutano wa Wanahisa ambao umefanyika jijini Dar es Salaam jana katika ukumbi wa Quality Centre.
 Baadhi ya Wanahisa wa Kampuni hiyo wakipitia makabrasha tayari kwa kuanza mkutano huo.
 Wafanyakazi wa ngazi za juu wa shirika hilo wakiwa katika mkutano huo ambao umefanyika jijini Dar es Salaam na kushirikisha idadi kubwa ya Wanahisa wa Kampuni hiyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya TOL, Harold Temu(kushoto) akijadili jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa TOL, Daniel Warungu kabla ya kuanza kwa mkutano wa Wanahisa jijini Dar es Salaam jana.


MKAKATI unaolenga kuboresha utendaji wa Kampuni ya Gesi ya TOL, umeanza kuwa na mafanikio.

Akifungua mkutano wa mwaka wa wanahisa jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Bodi ya TOL, Harold Temu, amesema kuwa uzalishaji na mapato ya kampuni hiyo yameongezeka katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, kutokana na mipango imara waliyoiweka.

“Hii ni dalili nzuri, kwani kampuni iko kwenye mwelekeo sahihi katika eneo la uzalishaji na mapato yanakwenda vizuri, kwani yameongezeka kwa asilimia 26 hadi asilimia 30 kwa kipindi cha miaka miwili," alisema Temu.

“Faida baada ya kodi imeongezeka mara saba hadi kufikia shilingi milioni 952 kwa mwaka kutoka shilingi milioni 120 za mwaka 2011,” alisema Temu.

Kwa mujibu wa Temu, sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa kuimarisha utendaji wa kampuni hiyo, TOL imekamilisha ujenzi na uzinduzi wa mtambo wa kisasa wa kutengeneza gesi aina ya Oksijeni wilayani Rungwe, mkoani Mbeya.

Alisema uwepo wa mtambo huo, utaongeza uwezo wa kampuni wa uzalishaji kwa asilimia 200 na hivyo kuiwezesha kampuni kukidhi mahitaji yote ya gesi hiyo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TOL, Daniel Warungu, alisema kampuni hiyo iko katika mkakati wa kumiliki mtambo mkubwa wa kuzalisha tani 31 za gesi na kwamba mtambo huo ni mkubwa kuliko mitambo yote katika nchi za Afrika Mashariki na Kati.

“Hatua za kujinufaisha na uwezo mkubwa wa mtambo huo zimefikia mahali pazuri na muda mfupi ujao wateja wetu watanufaika kutokana na uwezo mkubwa wa mtambo wetu,” alisema Warungu.

Alilalamikia pia uwepo wa kampuni feki za gesi ambazo alisema zinatishia kuharibu imani iliyojengeka kwa wananchi juu ya gesi ya TOL.

No comments: