![]() |
Dkt. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Uchukuzi |
Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa agizo kwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) kuwafukuza kazi na kuliagiza jeshi la Polisi nchini kuwaunganisha na wengine kwenye kesi mahakamani ili kujibu mashitaka ya jinai, wale wote waliohusika katika kuwasaidia Agness Gerald na mwenziye Melissa Edward kupitisha dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine "TIK" au "Meth" au "USAN" kilogramu 180 kuelekea Afrika Kusini Julai 5 mwaka huu, ambako walikamatwa katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Oliver Tambo nchini humo.
Waziri Mwakyembe ametoa agizo hilo jana, ofisini kwake, mbele ya waandishi wa habari wakati alipowaita ili kuufahamisha umma kuhusu hatua zilizochukuliwa na Wizara yake kuhusu suala la dawa za kulevya.
Waliofukuzwa ni Koplo Ernest, Yusuph, Jackson, Juliana Tadei na Mohamed ambao walihusika katika kuwasaidia Agnes Gerald (Masogange) na mwenzake Mellisa kupitisha dawa za kulevya kuelekea Afrika Kusini ambako walikamatwa.
![]() |
Agness Gerald a.k.a. Masogange |
No comments:
Post a Comment