Meneja Uratibu Ofisi za Kanda toka Mfuko wa Pensheni wa PPF Mbarouk Magawa akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya namna mwanachama anavyoweza kupata taarifa mbalimbali za michango yake.
Meneja Uwekezaji toka Mfuko wa Pensheni wa PPF Selestine Some akielezea mafanikio mbalimbali ambayo mfuko umepata tangu kuanzishwa kwake miaka 35 iliyopita
Afisa Uhusiano toka Mfuko wa Pensheni wa PPF Lulu Mengele (kushoto) akiwaeleza waandishi wa habari mafanikio ya mfuko na aina za mafao ambazo mfuko inatoa kwa wanachama wake, kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Zamaradi Kawawa.
Mfuko wa Pensheni wa PPF ni Mfuko mkongwe hapa nchini, ulianzishwa mwaka 1978 kwa Sheria ya Mfuko wa Pensheni wa PPF Sura na. 372 kwa madhumuni ya kutoa mafao ya pensheni na mafao mengine yanayoendena na hayo kwa wafanyakazi wote walio katika sekta rasmi na zisizo rasmi.
majukumu ya mfuko
PPF ina majukumu yafuatayo:-
i) kuandikisha wanachama,
ii) kukusanya michango,
iii) kuwekeza michango inayokusanywa na
iv) kulipa mafao ya pensheni na mafao mengine yanayoendana na hayo kwa wanachama wake.
WIGO WA UANACHAMA
Mfuko unaandikisha wanachama kutoka katika sekta zote za uchumi mashirika ya umma, makampuni binafsi, waliojiajiri wenyewe na sekta isiyo rasmi
Mafao ya PPF: Mfuko wa PPF una mafao saba
baadhi ya mafao ambayo Mfuko unatoa ni
Mafao ya Pensheni ambapo hutolewa pale ambapo mwanachama anapokuwa amechangia kwa kipindi cha miaka 10 au zaidi na amefikia umri kustaafu yaani miaka 55 mpaka 60.Na awe ameondoka kwenye ajira.
Mpaka sasa PPF ina wastaafu wapatao 25,896 na tunalipa kila mwezi Billioni 3.7
Hii ni kwa mafao ya uzeeni tu mnaweza kuona jinsi tunavyosaidia kuondoa umaskini na kukuza uchumi wa nchi.
Mafao ya Ugonjwa
Hutolewa pale ambapo mwanachama wa PPF anapokuwa ameondoka kazini kwa sababu za ugonjwa na imedhibitishwa na Daktari kwamba kweli hawezi kufanya kazi tena
Mafao ya Elimu:
Hutolewa pale ambapo mwanachama wa PPF anapokuwa amefariki dunia baada ya kuchangia kwa muda wa miaka 3 au zaidi.
Fao hili hutolewa kwa watoto wa mwanachama wasiozidi 4 kwa kulipia gharama ya elimu ya chekechea mpaka kidato cha nne.
Kwa kutambua umuhimu wa elimu kuanzia mwakani 2014 Mfuko unaongeza muda wa kuwasomesha watoto mpaka kidato cha sita.
Tunalipa mmoja kwa mmoja kwenye shule za watoto wanachama
No comments:
Post a Comment