Pages

Thursday, August 15, 2013

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU MATUMIZI YA MIFUKO YA PLASTIKI NCHINI - DKT. TEREZYA HUVISA

Picha ya juu na chini ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Mamaku wa Rais Mazingira, Dkt. Terezya Huvisa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo kuhusu tamko la serikali la kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki hapa nchi.
(Picha na Ofisi ya Makamu ya wa Rais.)



SERIKALI imepiga marufuku uingizaji, utengenezaji, uuzaji na utumiaji wa mifuko ya plastiki kutokana na mifuko hiyo kusababisha uchafu na madhara kwa binadamu.

Hayo yameelezwa leo na Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais(mazingira) Dkt. Terezya Huvisa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Dkt. Huvisa ameeleza kuwa Serikali imeamua kuchukua hatua hiyo ili kupunguza ama kuondoa kabisa tatizo la kusambaa kwa taka za mifuko ya plastiki ambayo baada ya matumizi yake huishia kwenye uchafuzi wa mazingira.

Aidha, dkt. Huvisa amesisitiza kuwa zuio hilo linahusu mifuko yote ya plastiki ya kubebea bidhaa toka madukani, sokoni na majumbani isipokuwa mifuko yenye unene wa maikron 100 inayooza (bio-digradable) na vifungashio vya bidhaa mbalimbali kama vile vifaa vya mahospitalini.

"Marufuku hii inapaswa kuzingatiwa na wenye viwanda, wenye maduka na wananchi wote kwa ujumla ili kutokomeza kuenea kwa taka zinazotokana na mifuko ya plastiki kwenye mazingira." amesema Dkt. Huvisa.

Vile vile Dkt. Huvisa amesema kuwa jitihada zinatakiwa zifanywe ili kuhakikisha kuwa marufuku hii inazingatiwa na kwamba misako ya watu wanaofanya biashara ya mifuko hii itafanyika katika maeneo yote ndani ya nchi yetu, na watakaokiuka watachukuliwa hatua, ikiwa ni pamoja na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Imeelezwa kuwa madhara yanayosababishwa na mifuko ya plastiki ni pamoja na uharibifu wa udongo unaotokana na kuunguzwa na plastiki hizo na hivyo kusababisha madhara ya kiafya kwa binadamu na wanyama, kutooza kirahisi kwa njia za kiasili (non-biogradable), kuzagaa katika mito, maziwa, bahari na nchi kavu hivyo kuhatarisha maisha ya viumbe hai wanaoishi katika mazingira hayo.

No comments: