Pages

Friday, March 4, 2016

SERIKALI YAVIPONGEZA VYOMBO VYA HABARI KWA KUHABARISHA JAMII VYEMA

1658-naibu waziri akiongea na hadhara
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura akizungumza na wadau wa habari wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na kampuni ya Mwananchi Communications Limited. Mheshimiwa Wambura alivishukuru vyombo vya habari kwa kuhabarisha watanzania kipindi cha uchaguzi na pia katika siku mia za kwanza za Rais wa awamu ya tano na Mhe.John Pombe Magufuli na kuwapongeza kwa kuonyesha weledi na ukomavu katika uandishi wa habari.
1615-naibu waziri akikaribishwa
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Anastazia Wambura akisalimiana na Mkurugenzi mkuu National Media Group  Bw. Joe Muganda wakati wa tafrija fupi iliyoandaliwa na kampuni ya Mwananchi Communications limited kwa ajili ya Bodi ya  Bodi ya Mwananchi,wateja wake na wadau wa Habari.
1635-mwambene akifurahia jambo
Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Bw.Assah Mwambene (kushoto) akifurahia jambo na Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Mwananchi Communications Limited Bakari Machumu wakati wa tafrija fupi iliyoandaliwa na kampuni ya hiyo kwa ajili ya Bodi ya  Mwananchi,wateja wake.
Na Daudi Manongi
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura amevipongeza Vyombo vya Habari kwa kuwahabarisha watanzania vyema katika mchakato wote wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na katika kipindi cha siku mia za kwanza za awamu ya tano ya utawala wa Mheshimiwa Dr. John Joseph Pombe Magufuli.

Naibu Waziri uyo ameyasema hayo alipokuwa akiongea na wadau wa Habari katika tafrija fupi iliyoandaliwa na kampuni ya Mwananchi Communications Limited.

“Hakika mmeonesha uwezo mkubwa, weledi na ukomavu mkubwa wa kisiasa na uzalendo kwa nchi yetu”.Alisema Bi.Wambura.

Mhe.Wambura pia alieleza kuwa Serikali ya awamu ya tano ina dhamira ya dhati kabisa ya kushirikiana na wadau wote vikiwemo Vyombo vya Habari, ambapo pia mchakato wa Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ambao ulishasomwa kwa mara ya kwanza bungeni bado Serikali inaendelea kupokea maoni ya wadau mbalimbali juu ya namna bora ya kuboresha Muswada huo.

Naibu Waziri uyo alikazia umuhimu wa upashaji habari na kusema ni jambo muhimu sana katika nchi yetu na kwaiyo Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo iko tayari kufanya kazi na wadau wote.

“Kama Serikali hatuwezi kuwakwepa wadau na ndio maana hata utaratibu wetu wa kushughulikia makosa kwenye Vyombo vya Habari umebadilika. Tumekuwa ni walezi zaidi badala ya kuwa viranja. Tunashauriana zaidi kuliko kutoa adhabu. Tunaelimisha zaidi kuliko kusubiliana”

Naibu Waziri uyo pia aliupongeza uongozi mpya wa jukwaa la wahariri na kuhaidi kuwapa ushirikiano wa karibu katika kutatua masuala mbalimbali ya Habari.

Kwa upande wake Mwenyekiti Mtendaji wa Bodi ya Magazeti ya Mwananchi Bw.Francis Nanai aliipongeza serikali kwa kuweka jitihada zaidi katika kuboresha mahusiano mazuri na vyombo vya Habari na pia kwa afrika mashariki Tanzania iko katika nafasi nzuri ukilinganisha na wenzetu katika suala la uhuru wa vyombo vya habari.
1664-wadau wa habari
Wadau wa habari wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura. Kutoka kushoto ni Bi.Teddy Mapunda na mwisho kulia ni Maria Sarungi.

RC DAR APIGA MARUFUKU UTOAJI VIBALI VYA MALORI YA MIZIGO YA ZAIDI YA TANI 10

Picha na 1
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Saidi Meck Sadiki akizungumza na wajumbe wa Bodi ya barabara ya mkoa wa Dar es Salaam kwenye kikao cha kwanza cha Bodi hiyo kwa mwaka 2016. Kulia ni Zungu Azzan, Mbunge wa Ilala na Kushoto ni Bw. Edward Otieno, Kaimu Katibu Tawala wa mkoa huo.
Na Aron Msigwa – MAELEZO
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Saidi Mecki Sadiki amepiga marufuku utoaji wa vibali vya malori ya mizigo na magari yenye uzito wa zaidi ya tani 10 kuingia katika barabara zote zinazosimamiwa na Manispaa za jiji la Dar es Salaam zilizojengwa kwa kiwango cha lami kufuatia barabara hizo kuharibika kwa kipindi kifupi kutokana uzito jambo linaloisababishia Serikali hasara.

Aidha, ameziagiza manispaa za jiji hilo kuweka alama za barabarani zinaonyesha zuio kwa magari yote yenye uzito wa zaidi ya tani 10 kupita kwenye barabara hizo ili wamiliki na madereva watakaokiuka agizo hilo wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Dar es Salaam kwenye kikao cha kwanza kwa mwaka 2016 Mhe. Sadiki Meck Sadiki amesema kuwa Manispaa za jiji hilo zinatenga fedha nyingi za kujenga barabara mpya na kufanya matengenezo ya zile zilizopo ambazo nyingi zinaharibiwa na malori ya mizigo.

Amefafanua kuwa matumizi hayo mabaya ya barabara kwa kiasi kikubwa yanachangiwa na ukiukwaji wa sheria za barabarani ambapo malori makubwa ya mizigo huegesha na kuziba maeneo ya waenda kwa miguu jambo linalowanyima haki wananchi kutumia maeneo yaiyotengwa kwa ajili yao.

Amesema baadhi ya magari yenye uzito wa tani 40 hudiriki kupita kwenye barabara za huduma (Service road), madaraja na wakati mwingine maeneo ya waenda kwa miguu jambo linalosababisha uvunjaji wa kingo za barabara na milingoti ya taa za barabarani na kuongeza kuwa vitendo hivyo vinaisababishia Serikali hasara kutokana na gharama ya matengenezo.

“Kuanzia leo katika mkoa wangu ni marufuku kutoa vibali vya magari yenye uzito wa zaidi ya tani 10 kuingia kwenye barabara zetu, tunataka barabara zetu zidumu, hatuwezi kuvumilia vitendo vya watu wachache wanaokiuka sheria za barabarani kuharibu barabara zetu, lazima tuchukue hatua Manispaa zinajitahidi kujenga bararaba lakini hazidumu” Amesisitiza Mhe. Sadiki.

Amesema barabara zinazosimamiwa na Manispaa za Dar es Salaam zina uwezo wa kuhimili uzito wa tani 10 na kubainisha kuwa kwa kipindi kirefu malori ya tani 40 yamekuwa yakipita kwenye barabara hizo na kuzifanya manispaa kunajenga barabara hizo kila mwaka.

Mhe. Sadiki amesema kuwa ipo haja ya mamlaka zinazohusika na miundombinu ya barabara katika jjiji la Dar es Salaam kwa kuwatumia wataalamu wa sheria kuanza kuangalia uwezekano wa wamiliki wa vyombo vinavyosababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara kulipa gharama za uharibifu huo.

Kuhusu ulinzi na Usalama watumiaji wa barabara za jiji amelitaka Jeshi la Polisi kuendelea kuchukua hatua na kufanya Operesheni dhidi ya madereva wa pikipiki (Bodaboda) na Bajaji wanaopitisha vyombo vyao vya usafiri kwenye njia za waenda kwa miguu na kusababisha usumbufu na ajali za mara kwa mara kwa wananchi wanaotumia njia hizo.

Pia amezitaka Manispaa za jiji hilo kushirikiana na Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Dar es Salaam kusimamia maeneo yote yanayotakiwa kujengwa miundombinu ya barabara ili yasivamiwe na wananchi pamoja na kuwachukulia hatua wananchi wanaofanya biashara katika maeneo yasiyoruhusiwa ya hifadhi za barabara na njia za waenda kwa miguu.

‘‘Ninaiagiza Manispaa ya Kinondoni kuondoa wafanyabishara wote walioko eneo la kituo cha kuzalishia umeme Ubungo, eneo lile ni hatari kwa usalama na maisha yao, kukaa pale ni kinyume cha sheria,’’ amesisitiza.

Aidha, amesema mwaka 2016 mkoa wa Dar es Salaam umetenga jumla ya Shilingi bilioni 343.5 ikilinganishwa na shilingi bilioni 266.6 zilizotengwa  mwaka 2015/2016 kutekeleza ujenzi na matengenezo ya barabara katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo lengo likiwa kupunguza msongamano wa magari.

Kuhusu Kikao hicho cha kwanza cha Bodi ya barabara ya mkoa wa Dar es Salaam kwa mwaka 2016 amesema pamoja mambo mengine kimepokea na kujadili tarrifa  utekelezwaji wa ujenzi wa miradi ya barabara kwa mwaka 2015/2016 pamoja na kupokea Mpango wa matengenezo ya barabara kwa mwaka 2016/2017.

Ametoa wito kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuzingatia usafi wa mazingira kwa kulinda miundombinu ya barabara na kuepuka kutupa taka kwenye  mifereji  ya kupitisha maji ili kuzuia mlipuko wa magonjwa ukiwemo ugonjwa wa kipindupindu.
Picha na 2
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw.Isaya Mngurumi akichangia jambo kuhusu uboreshaji wa miundombinu ya barabara katika Manispaa yake wakati wa Kikao cha kwanza cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Dar es Salaam.
Picha na 3
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema akichangia jambo wakati wa Kikao cha kwanza cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Dar es Salaam kwa mwaka 2016.
Picha na 4
Baadhi ya Wabunge wa jiji Dar es Salaam wakifuatilia kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mhe. Bonnah Kalua – Mbunge wa Segerea, Mhe. Faustine Ndugulile – Mbunge wa Kigamboni, Mhe. Azzan Zungu – Mbunge wa Ilala na Mhe. Abdallah Mtolea – Mbunge wa Temeke.

Thursday, March 3, 2016

DIWANI WA CCM AUMBULIWA MBELE YA MBUNGE, WANANCHI WAMZOMEA WAGOMEA MAAMUZI YAKE

Diwani wa kata ya Ng'ang'ange wilaya ya Kilolo Bw Namgalesi Lusumsuva akisisitiza jambo baada ya  kutoa maamuzi magumu ya kuteua majina  mawili ya mabinti ambao watakaimu nafasi ya afisa mtendaji wa kijiji cha Ng'ang'ange kabla ya wananchi kumpinga, kulia ni Mbunge wa jimbo la Kilolo Venance Mwamoto.

Mbunge Mwamoto akimpatia namba ya simu mmoja kati ya wasanii kijiji  cha Ng'ang'ange anayeomba kufika kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa albamu yake.
DIWANI  wa kata ya Ng'ang'ange  wilaya ya  kilolo mkoani Iringa Bw Namgales  Msuva (CCM) amejikuta katika  wakati mgumu  mbele ya  mbunge wa  jimbo la Kilolo Bw Venance Mwamoto baada wananchi  kumzomea kama  njia  ya  kupinga uteuzi  wake  usio  shirikishi wa makaimu wawili    watendaji wa  kata  ya Ng'ang'ange .

Wananchi hao    walifikia hatua   hiyo jana  wakati wa mkutano wa hadhara  wa mbunge  wao kuwashukuru  kwa  kumchagua  kuwa mbunge  wao katika  uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana .

Kabla  ya  diwani   huyo  kupingwa mbele ya  wananchi na mbunge  kuingilia kati kutuliza jazba  za  wananchi hao ,alikuwa  amewateua wasichana  wawili wakazi wa kijiji  cha Ng'ang'ange  akiwemo Felista Ngogo ambae alikuwa akikaimu nafasi hiyo na msaidizi  wake Flora Magoda  kuendelea  kukaimu nafasi hiyo .

Kwani  diwani   huyo alisema  kuwa  sababu ya  yeye  kufanya uteuzi huo ni  baada ya awali  kuteua  mtendaji wa muda ambae aliacha nafasi hiyo  baada ya  wananchi  kuonyesha  kumpuuza katika maagizo  mbali mbali aliyoyatoa.

Hivyo  alisema haiwezekani ofisi  hiyo  kukosa afisa mtendaji  wa kata kwa  zaidi ya miezi 6  hivi  sasa na yeye akiwa kama mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya kata  hiyo na diwani ameamua kufanya uteuzi wa maofisa hao  watendaji wawili badala ya mmoja ili  kuifanya kazi   hiyo.

" Mtendaji  katika  ofisi hii ya kata hayupo na  ofisi  imekuwa  ikifungwa muda  wote .....utendaji kata  si ajira halipwi chochote  sasa  mimi kama  diwani na mwenyekiti wa kata  natumia nafasi yangu kuwateua mabinti hawa  wawili ambao wataifanya kazi hii ya  kujitolea  kuanzia  leo nimeona  tunalala  sana .....natoa amri kuanzia  sasa mnanisikiliza " alisisitiza diwani  huyo

Huku  akitaka wananchi  ambao  wanatuhumiwa kwa ushirikina na pamoja na  vijana  wanaoshinda  vijiweni kufikishwa mbele ya  ofisi  yake ya kata  haraka   ili  kuchapwa  viboko.

Hatua   hiyo  ya  uteuzi wa maofisa  watendaji hao ilipelekea  mkutano  huo wa mbunge  kuvurugika kwa muda baada ya  wananchi hao kupinga ubabe wa diwani  wao  huyo kwa kufanya uteuzi pasipo kushirikisha baraza la  maendeleo ya  kata wala wahusika   wenyewe  kushirikishwa .

Wananchi hao  walisema  hawautambui uteuzi  wa maofisa  hao wa kata na  kuwa hao  aliowateua ni maofisa wa nyumbani kwake na  sio katika ofisi  hizo za serikali ngazi ya kata .

Mbali ya  wananchi  kuzomea  na  kumkataa diwani  huyo kwa maamuzi yake pia mabinti  hao  walijitokeza hadharani na  kukataa uteuzi huo kuwa hauna maslahi kwao na  wao  hawajashirikishwa kabla ya  kutangazwa hivyo hawapo tayari  kufanya kazi   hiyo kutokana  na  diwani  kutowashirikisha mapema .

Mbunge wa Kilolo Bw Mwamoto  alilazimika  kusimama na kusitisha uteuzi  huo kufuatia  maombi ya  wananchi  kumtaka  kuingilia kati maamuzi ya  diwani  huyo ambayo hayakushirikisha  kiongozi wala  mjumbe mwingine  yeyote  wa ngazi ya  kijiji  wala kata.

Bw  Mwamoto  alisema anasitisha  uteuzi huo  wa diwani  kwa  watendaji hao na  yeye kama  mbunge atawasiliana na ofisi ya mkurugenzi  mtendaji wa Halmashauri  ya  wilaya ya  Kilolo ili baada ya ajira  mpya  za  watendaji kutolewa basi kata  hiyo kupewa  kipaumbele na  kwa  sasa wakati  zoezi hilo  bado  kufanyika mwenyekiti wa  serikali ya kijiji  cha Ng'ang'ange ataendelea kukaimu nafasi ya utendaji  wa kata  pia.

Maamuzi hayo ya mbunge  Mwamoto  alionyesha  kuwafurahisha  wananchi  hao  wakiwemo wale wa upinzani  kutoka chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema ) ambao  walimpongeza mbunge kwea  busara  zake na  kuahidi  kuendelea  kutoa ushirikiano kwa mbunge   huyo na mwenyekiti  aliyeteuliwa kukaimu  utendaji wa kata.

Mbunge  wa  Kilolo Bw Venance Mwamoto wa kwanza  kulia akicheza ngoma ya njuga na  wasanii wa asili kijiji  cha Ng'ang'ange baada ya  kufika katika  mkutano wa hadhara.

UNCDF LAUNCHES REGIONAL CONSULTATIONS ON MUNICIPAL FINANCE

video-conference-1-702x336
In collaboration with the Financing for Development Office of the United Nations Department of Economic and Social Affairs and the Government of Tanzania, UNCDF launched a global series of expert group consultations on municipal finance in Dar es Salaam, Tanzania on 29 February – 1 March 2016.

The meeting brought together a unique set of practitioners, local government representatives, academics, policy makers and the private sector from African countries, as well as UN entities and other development partners. In an interactive format, experts exchanged their experiences and suggested policy measures on how municipal governments especially in the Least Developed Countries can access long-term finance to implement the ambitious 2030 Agenda for Sustainable Development.

“According to figures from the United Nations, 1.2 billion people live in over 650 secondary cities in developing countries. Yet most government finance and development aid is directed to central government agencies whilst private finance often avoids local governments”, said David Jackson, Director of Local Development Finance at UNCDF. The Africa expert consultation is the first in a series of regional consultations that aim to pave the way for increased and more effective international cooperation on subnational finance as called for Addis Abba Action Agenda and reaffirmed in the preparation of the Habitat III Conference later this year.

The discussion delved deep into lessons learned from fiscal, political and administrative decentralization experiences across African LDCs, many involving UNCDF support. There was a consensus view that enabling and empowering local authorities to unlock resources for long-term finances requires a holistic approach to municipal finance. Sound financial management and improved internal revenue generation including through effective property taxes, user fees, and land value capture can pave the way for better access to private and public domestic finance.

“Collaboration between banks and local government in Africa has to step up. Both actors have to meet in a middle area called trust where they share strategy, ambitions and solutions” said Ms. Zienzi Musamirapamwe, Head of Public Sector, Corporate and Investment at Barclays South Africa. Central government support and a conducive governance environment are equally important and intergovernmental fiscal transfers will remain a key source of local government finance.
UNCDF_GROUP PHOTO2
Participants noted that many municipalities in Africa have come a long way in getting their finances in order while promoting affordable access to essential services for all. Experts discussed the positive experiences of an increasing number of African cities such as Dakar and Kampala City, both of which have received investment grade ratings from well-known regional rating agencies. The progress of secondary African cities has also been reviewed and noted.

According to Khady Dia Sarr, Program Director, Dakar Municipal Finance Program, development is primarily local; and finance is one of the keys to development. “We have to strengthen local authorities in Africa to tap into capital markets to respond to the needs of populations.”

“Decentralization is essential, especially fiscal decentralization” said Youssouf Séga Konaté, Technical Adviser, Ministry of Decentralization of Mali. Experts also agreed that successful decentralization hinges on a carefully sequenced series of policy measures. It is a process that requires continuous assessment of what works and what doesn’t and policies can change down the road. The discussion also featured lively exchanges between local authorities and central government representatives, including on the appropriate level and types of fiscal transfers and the authority for municipalities to borrow. Participants agreed that good communication and buy-in from all stakeholders are crucial factors for success.

Mr. Shomary Mukhandi, Director, Regional Administration and Local Government – President’s Office in Tanzania, gathered from the discussions that there is a need to consider other feasible ways of financing local government infrastructure development projects to meet and reduce the fiscal gap between actual needs and available resources. “We have learnt some valuable lessons from participating in this key meeting. Pertinent issues have been raised in improving municipal finance that can be applied by local governments in Tanzania to stimulate and improve local economic growth.”

The consultation will result in a publication that summarizes major findings and provide some general guidelines for policy makers at the international, national and local levels of the Least Developed Countries. In addition, the published results will feed into the discussions leading to the Habitat III conference later this year, which should focus on how to implement the global agenda through cities.

MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KUFANYIKA MACHI 8

download (2)
Wizara ya Maendeleo ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto inawataarifu wananchi wote kuwa tarehe 8 Machi ya kila mwaka Tanzania huungana na nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Mataifa kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake, hutoa fursa kwa Serikali, wananchi, wadau, na wanawake wenyewe kupima utekelezaji wa maazimio, matamko na mikataba ya Kimataifa, Kikanda na Kitaifa inayohusu masuala ya maendeleo ya wanawake na usawa wa jinsia.

Siku ya wanawake Duniani husisitiza kujenga mshikamano wa wanawake wote duniani, kuhamasisha jamii kutafakari kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake ya kila mwaka; kuelimisha jamii kuhusu jitihada mbalimbali zilizofanywa na Serikali na asasi mbalimbali yakiwemo Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika kuwaendeleza wanawake; na kuhamasisha jamii kuhusu utekelezaji wa sera na mipango mbalimbali ya Serikali yenye lengo la kudumisha Amani, Usawa na Maendeleo.

Kaulimbiu ya  kitaifa ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mwaka 2016  inasema “50 – 50 Ifikapo 2030; Tuongeze Jitihada”. Kaulimbiu hii inasisitiza kuwa na mikakati thabiti yenye mwelekeo wa kufikia Agenda  2030 ya malengo inayohimiza kufikia asilimia 50 kwa 50 ya ushiriki wa wanawake na wasichana katika nyanja zote za maendeleo.

Kuanzia mwaka 2005 Serikali ilipitisha uamuzi kuwa, maadhimisho haya yafanyike Kitaifa kila baada ya miaka mitano kutoa muda wa utekelezaji wa maazimio na kupima mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitano. Mwaka 2015 Maadhimisho yalifanyika Kitaifa mkoani wa Morogoro. Kwa mwaka  2106, mikoa yote itaadhimisha siku hii katika maeneo yao kwa kuzingatia hali na mazingira ya mikoa husika. Kwa mfano mkoa wa Dar es salaam, utaadhimisha siku hii katika Manispaa ya Kinondoni. Wizara inatoa wito kwa mikoa yote kuhamasisha wananchi na wadau wote kushiriki maadhimisho ya siku hii adhimu na kuzingatia ujumbe wa kauli mbiu ya mwaka 2016.

Rai yangu kwa wadau wote ni kuwa, tuunge mkono jitihada za Serikali katika kutoa haki na ushiriki sawa katika fursa za uongozi wa kisiasa na kiuchumi; na kupima mafanikio yaliyofikiwa na kuweka mipango yenye matokeo makubwa, na kubainisha shuhuda za wanawake waliotoa mchango uliotukuka katika kuwezesha maendeleo ya wanawake wenywe na taifa kwa ujumla.

Nashauri wanahabari wote kuelimisha jamii kuhusu kaulimbiu ya Siku ya Wanawake kwa mwaka 2016 ili kila mwananchi aweze kutambua jukumu alionalo katika kufikia lengo la ushiriki sawa wa wanawake na wasichana katika uchumi; afya, elimu, ajira, sheria na siasa ifikapo mwaka 2030.

Nawatakia mafanikio mema katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mwaka huu.

Sihaba Nkinga
KATIBU MKUU

WANANCHI WACHOSHWA NA TAASISI YA VIZAZI NA VIFO (RITA) OFISI ZA PEMBA

download (13)

Na Masanja Mabula –Pemba
WANANCHI  wa Kisiwani Pemba wamesema kwamba wamechoshwa na vitendo nenda rudi nenda rudi katika Ofisi za vizazi na vifo kufuatailia vyeti vya kuzaliwa na pamoja na vyeti vya vifo ambavyo upatikanaji wake unasumbua.

Wananchi hao  wamelalamika juu ya ucheleweshwaji wa vyeti hivyo jambo ambalo limekuwa nikikwazo kikubwa  katika upatikanaji  wa  haki  zao za msingi.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti wamesema kuwa upatikanaji wa vyeti hivyo ni tatizo la muda mrefu hali ambayo imesababisha baadhi wa watoto kuanza skuli bila ya kuwa na cheti cha kuzaliwa .

Aisha  Kombo Hassan Mkaazi wa Ukutini Mkoani alisema kwamba ufuatiliaji  wa vyeti katika ofisi za Vizazi na Vifo za Wilaya, mbali na usumbufu anaoupata pia umekuwa ukiongeza gharama anazotumia katika gari za abiria.

"Hata ukikipata cheti utakuwa imetumia zaidi ya shilingi elfu ishirini, hii ni kutokana na gharama za kupanda katika gari za abiria mara kwa mara kwa kweli tunasumbuka sana," alifahamisha.

Naye Juma Ali Mohammed mkaazi wa Makangale, alisema kwamba wapo baadhi ya wananchi wamekosa vitambulisho vya mzanzibar mkaazi kutokana na kutokuwa na vyeti vya kuzaliwa.

Alisema wako vijana ambao wametmiza umri wa kupiga kura , lakini wameshindwa kupata fursa hiyo kutokana na kutkuwa na vyeti vya kuzaliwa ambavyo ndiyo vinavyopelekea kupata kitambulisho cha Mzanzibar .

Hali hiyo pia imelalamikiwa na Mwatime  Omar Issa Jojo Mchangamdogo ,  ambaye aliiomba  Serikali kuchukua hatua za makusudi kulipatia ufumbuzi suala hilo, ili wananchi wanaondokane na usumbufu wanaoupata kwa sasa.

Kwa upande wake Mdhamini  Ofisi ya Wakala Wa Usajili Wa Biashara Na Mali Vizazi Na Vifo Pemba Salehe Mohd Abdalla amesema  hali hiyo inatokana na ufinyu wa bajeti katika Ofisi hiyo .

Alisema kuwa tatizo hilo litapatiwa ufumbuzi hivi karibuni kwani Ofisi hiyo inatagemea kupata magamba elfu kumi (10000) kutoka Ofisi Kuu Unguja na watayagawanya kwa Ofisi za Wilaya  zote Pemba.

"Tunatarajia kupata magamba elfu kumi , na yakifika tu tunayapeleka katika Ofisi za Vizazi za Wilaya , naomba sana wananchi wawe wastahamilivu tatizo linafahamika," alieleza.

Aidha alifahamisha kuwa kutokana na ongezeko la vizazi, ofisi ya Pemba inahitaji kupata magamba angalau  mia tatu (300) kila mwezi ili kukidhi haja na mahitaji ya wananchi.

Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi umebaini kwamba baadhi ya Wilaya kuna wananchi wanadai vyeti vya kuzaliwa vya watoto wao kwa zaidi ya miaka mitano sasa bila ya mafanikio.
Chanzo:  Fullshangwe Blog

TWIGA STARS TAYARI KUWAVAA ZIMBABWE KESHO

Kikosi cha timu ya Taifa ya Wanawake ya Mpira wa Miguu (Twiga Stars), leo kimefanya mazoezi ya mwisho tayari kwa kuwakabili timu ya Taifa ya Wanawake kutoka Zimbabwe (Mighty Warriors) katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika kesho Ijumaa katika uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam.

Twiga Stars inayonolewa na kocha mzawa mwanamke, Nasra Juma imekamilisha ratiba yake leo asubuhi kwa kufanya mazoezi mepesi katika uwanja wa Karume ofisi za TFF, huku kocha wake Nasra akisema vijana wake wote wapo katika hali nzuri kuelekea kwenye mchezo huo.

Akiongea na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa TFF uliopo Karume, Nasra amesema ana waheshimu Zimbabwe wana timu nzuri, ndani ya miaka minne wameshacheza nao zaidi ya mara nne, mapungu yaliyojitokeza katika michezo iliyopita wamefanyi kazi na hivyo kesho ana imani watafanya vizuri.

Aidha kocha Nasra, amewaomba watanzania kujitokeza kwa wingi kesho Ijumaa katika uwanja wa Azam Complex Chamazi kuwapa sapoti Twiga Stars katika mchezo huo utakaonza majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Naye nahodha wa kikosi hicho Sophia Mwasikili, amesema wachezaji wote wapo katika hali nzuri, wana ana ari na morali ya hali ya juu kuelekea kwenye mchezo huo wa kesho, na kuwaomba watanzania kuwapa sapoti kwa kujitokeza kwa wingi kuja kuwashangilia uwanjani watakapokuwa wakipeperusha bendera ya Tanzania.

Wapinzani wa Twiga Stars, timu ya taifa ya Zimbabwe wanawasili leo jioni tayari kwa mchezo huo, huku waamuzi wa mchezo huo kutoka nchini Ethiopia wakiwa tayari wameshawasili leo mchana kwa shirika la ndege la Kenya (KQ).

HAPPY BIRTHDAY LULU SHABANI TOLLE

 
UONGOZI WA SHABANI TOLLE BLOG UNAKUTAKIA HERI YA SIKU YAKO YA KUZALIWA BI LULU S. TOLLE.  
MWENYEZI MUNGU AKUJAALIE AFYA NJEMA,  UMRI MREFU NA UTIMILIFU WA NDOTO ZAKO.  AMEN.

WAZIRI NAPE MGENI RASMI TAMASHA LA PASAKA JIJINI MWANZA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhNDkoUud6CFChe-0KRC2pgkqtxdYnge7MrKomIif7tejP67j17mKgmXEKM_gR7FWk7sliE5UPh4hMxLuh2RESmRI5jLXtsW59MQR1LQwmdk07tu6XBeolt963nYTbK1oxtcTXnwjEn9G3k/s1600/OTH_0565.jpg
Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama ambaye pia ni Mwenyekiti wa tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika hivi karibuni jijini Mwanza, akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari alipokuwa akizungumza nao ofisi kwake, Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Pasaka  linalotarajiwa kufanyika jijini Mwanza mnamo Machi 27.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maaandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama,amebainisha kuwa Waziri Nape amekubali kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo ambalo litaanzia Geita Machi 26 na kumalizia Kahama Machi 28.

Msama alisema kamati yake inaendelea na maandalizi ya kuelekea tamasha hilo ambalo litashirikisha waimbaji mbalimbali hapa nchini.“Maandalizi kuelekea Tamasha la Pasaka yanaendelea vema, hivyo wakazi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa wajiandae kupokea ujumbe wa neno la Mungu kupitia viongozi wa dini na waimbaji wa muziki wa Injili,” alisema Msama.

Msama alisema baadhi ya waimbaji waliothibitisha kushiriki tamasha hilo ambao ni pamoja na Rose Muhando, Bonny Mwaitege, Upendo Nkone, Jesca BM Honore, Christopher Mwahangila, Joshua Mlelwa, Sifael Mwabuka, Jenipher Mgendi, Kwaya ya AIC Makongoro na Kwaya ya Wakorintho Wapili.

Msama pia alidokeza kuhusiana na suala zima la viingilio,alisema kuwa viingilio hivyo vinaendana na tukio hilo ambalo mbali ya kumuimbia na kumtukuza Mungu pia lina dhamira ya kusaidia jamii yenye uhitaji maalum.

“Nawaomba wakazi wa mikoa Geita, Mwanza na Shinyanga kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha tamasha hilo,” alisema Msama.

Msama alisema kupitia viingilio vya tamasha hilo wanatarajia kutoa kipaumbele kwa wakazi wa mikoa itakayopitiwa na tamasha kwa kupatiwa  baiskeli zaidi ya 100 za walemavu, ambazo zitagawiwa mikoa mbalimbali.

WASAMBAZAJI WA FILAMU TANZANIA WAIPONGEZA SERIKALI

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgpvpxo_kPB-yMYUjdZaaxTS3rAT1yZ3Odcqn-DCTi8vn6ftUwK1_AELT-BGJWJQzot7It76dSunKYdkbrgIZdkLIUw4TBhyA2GWfrumIAiWynJnCrhSfVJXQAqS48N-734cwlx6_ahzqyG/s1600/e2900841-88d8-42f8-b81e-2ec3908afe27.jpe
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Bw. Saimon Mwakifamba (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa pongezi za Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) kwa Serikali ya awamu ya tano katika mkutano na waandishi wa habari. Picha na Jacquile Mrisho MAELEZO

Na Jacquiline Mrisho, MAELEZO
Chama cha Wasambazaji wa Filamu Tanzania kimeipongeza Serikali ya awamu ya tano kwa juhudi zake inazozifanya katika kupambana na uharamia kwenye sekta ya filamu Tanzania.

Hayo yamesemwa na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Bw. Saimon Mwakifamba alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu kuunga mkono juhudi madhubuti za Serikali za kudhibiti uharamia wa kazi za filamu haswa kwenye eneo la mauzo la sokoni Kariakoo.

“Kwa takribani miaka mitatu sasa tumekuwa na kilio cha wazi kwa Serikaliya Tanzania iliitusaidie kuwabana wahujumu wa mapato ya nchi unaofanyika kupitia njia za kiharamia zinazotumika kuuza kazi za filamu ndani na nje ya nchi.Kilio chetu kimesikilizwa natunaamini tija ya soko la filamu litaanza kuonekana ndani ya muda mfupi kuanzia sasa.”AlisemaMwakifamba.

Aidha, Mwakifamba amefafanua kuwa, idadi ya watu walioulizia kuwekeza katika usambazaj iimeongezeka kutokana na kazi ya usambazaji kufanyika kwa uhalali baada ya juhudi za Serikali za kupunguza uharamia unaofanyika kwenye usambazaji wafilamu.Pia,ametoa rai kwa Serikali kutolegeza kamba bali kuzidi kulidumisha zoezi hili la kudhibiti mianya yote ya uharamia ili wasambazaji watumie utaratibu unaotakiwa na Serikali katika usambazaji wa kazi za filamu.

Kwa kipindi kirefu sasa wasanii nchini wamekuwa wakipambana na unyonywaji wa kazi zao za filamu unaofanywa na wasambazaji wa filamu wasio halali ambao wanapunguza mapato ya wasanii na taifa kwa ujumla.
Chanzo: Michuzi Blog

SERIKALI KUJENGA MACHINJIO YA KISASA VINGUNGUTI

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiQQABj7j4DdDQOu5y0vxV5MgsQLS7Wy2cp0FBU4k1Ass5fcK36S6XsC6tnUIFUHHgoYTXye31W6M9bcgbspil6tGhQ7AOdqvpR9xLR9F8-yf487j0VoZ7pQ5UNHmdXVNEtauz_YfuY8cEV/s1600/1.JPG

Na Raymond Mushumbusi, MAELEZO
Serikali imejipanga kujenga machinjio ya kisasa katika eneo la Vingunguti  Jijini Dar es Salaam ili kuondoa changamoto zilizopo machinjioni hapo ikiwa ni pamoja na kulinda afya za wachinjaji na walaji wa nyama.
 
Akiongelea mipango hiyo kwa njia ya simu Msemaji wa Manispaa ya Ilala Bi.Tabu Shahibu amesema Halmashauri iko katika mchakato wa kutangaza zabuni kwa makampuni yatakayoweza kujenga machinjio hayo kwa kiwango kinachotakiwa.

"Tupo katika harakati za kutafuta mkandarasi wa kujenga machinjio na hivi karibuni tutatangaza zabuni kwa ajili ya ujenzi huo."

"Napenda kuwahakikishia kwamba tutafanya jitihada zote za kumpata mkandarasi mapema ili tuanze mapema ujenzi huu wa machinjio mapya na kuondokana na changamoto zinazokabili machinjio yaliyopo," lisema Bi Tabu.

Aidha, Bi Tabu Shaibu amesema kuwa kabla ya kujenga machinjio mapya wanaendelea na ujenzi wa mabanda ya machinjio, njia za kushushia ng’ombe, bucha na kupanua eneo la machinjio na wameshapima na kufanya tathimini ya gharama ambazo zitatumika katika marekebisho hayo.

Mpango huu umekuja mara baada ya ya agizo la mawaziri, akiwemo Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Nchemba, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Hamis Kigwangalla na Waziri wa Nchi ofisi ya Raisi TAMISEMI MHE. George Simbachawene walipotembelea machinjio ya Vingunguti Januari 2 mwaka huu.

Machinjio ya Vingunguti yalianza kutumika tangu miaka ya 1950 ikiwa inahudumia idadi ya watumiaji wa mazao ya wanyama waliokuwa kwa wakati ule. Machinjio hayondio bado  yanatumika hadi sasa wakati idadi ya watumiaji wa mazao ya nyama wameongezeka  hivyo kukumbana na changamoto mbalimbali. Ili kukabiliana na changamoto hiyo Serikali imepanga kuyarekebisha yaliyopo na kujenga mapya na ya kisasa.
Chanzo: Michuzi Blog

Monday, February 29, 2016

TOLLE MEDIA BLOG INAKUTAKIA HAPI BATHI DAY BUTWA!!


 Rachel Maona wa UK alivyo sheherekea hapi bathi day ya butwa, Rachel ni mdogo wa Shabani Tolle mmoja wa wakurugenzi wa IPSHA MEDIA PRODUCTIONS AND PROMOTIONS wamiliki wa TOLLE MEDIA BLOG " Uongozi na wafanyakazi wote wa Blog hii inamtakia maisha marefu na yenye fanaka tele jomba BUTWA"

UPANUZI WA BARABARA YA ARUSHA KUWA NA NJIA SITA UNAENDELEA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhF_Ox0347ikJdtd1bAThXph5KpkARXxRW8u5gLBfmyM6voVVWKbYKbOX2T9oIvEN5KmSRkY5-sZhe_pcZq-sGoSdzsJZemoUBvzvlV645qyDVdJxGlEj1qGW5Ihd_612v0iu9nkalO9_EE/s1600/20160229012645.jpg
Picha ya juu na chini ni muonekano wa barabara ya Moshi-Arusha inayoendelea na upanuzi wake kuwa njia sita, kama inavyoonekana.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgkydK1KI9nzwQhpA2D5HOB3mTaFxnZYerlBGiFTAbXYuCJayliGe7xlvtiBhCVfUM9kqNfxC00dPNLXumz1DqbzPA4OemmgP29VW9ej0DZSIYf8VX5vkkv8MLV9VTTdPyb0xudoyiV4Vnq/s1600/20160229012654.jpg

INTERNATIONAL WOMEN'S DAY 2016

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgLOl0iwQldDUPgSzKkz_UfnrZx4FOLCaQxeCK8NrzV2gsf6bLjbHW4EnFXqX-xQUcZF0RcOpBlrp7BGzJIaKOcr9aiVHpOeukuqvfIqQkql7UM27qq9RO8Yka9Q9SrmXUMA1wK87lg8h0F/s1600/IWD+-+Empower+Women+FLYER+29.02.16.jpg

BEI ZA KUBADILISHA FEDHA LEO (EXCHANGE RATE)

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj9nTD6nbWhmfjQNfJs6xqqPhL0jRzSeaRmSCMDjfd7YiEWmxUBZROvQuTQoCryM9aDH3BrM__EPHHBVPwYkJCwRSgvRYdO_CPO1MEX-3w_baUA4RN8HqAsriUK2Wktn7bgkxj6rN6yrS3H/s1600/20160229001305.jpg

BREAKING NEWS: MABWENI YA SHULE YA SEKONDARI IYUNGA, MBEYA YATEKETEA KWA MOTO

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi5P42h0rmtQHwS4fJUWxBXMI1gmhLhy15wgdfUIqBcHMpSGUj7wFmsQbvrFsNWHp-LGLE7vb0TadMIxJmXUI_7akOzdbEa1WNT5l0zsVWUAiMYG2AsGf2-W4oHiyYAwlw2ad7WjM1HmPL8/s1600/20160229011740.jpg
Askari wa kikosi cha zimamoto jijini Mbeya akiendelea na jitihada za kuuzima moto unaoendelea kuwaka na kuteketeza mabweni ya shule ya Sekondari Iyunga.  Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika hadi sasa.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgys8Acyl-h-mo1FrBI8POGTSX80I5ig0qc3D_nvoWe6sSkjc3MkSMqYlsHJw4hUr6miD0Uazz5RMx5UwAihE_lyRVQL85Zp1rrFGDEtex1_NSP0pcF_GI579ACAzrW4Or4TtydFp0r_XPa/s1600/20160229011747.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhaVkFec4_qqWYPIoF6kC80li10EKtmorW5XCFOAjXekPv-Kr62lCtgmLPwTvgF0vgaKcyBOjBZmn_zFDnfbXHxVNQiRU8bMA3aWrktje8QE_i_fTKMRHRHWWS8yVSY45OolPx6wJTv4KdC/s1600/20160229011753.jpg
Kikosi cha zimamoto cha jijini Mbeya kikiendelea na jitihada za kuuzima moto huo.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhr94bAPoFX9oGetb6gefVOpFOYlJAc83aARTaIpRc62YwslL0fv6bPUeaTDHkXeWz8Qp_8c7vxfzVNjhzMCubxq74gNtIZmKgAvEoYWgjTukMstz8_z9fRZogdA8BTq5bmOcqLPpPGEcb9/s1600/20160229011802.jpg
Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo iliyopo jijini Mbeya wakiwa nje ya shule wakiangalia baadhi ya vitu vyao vilivyofanikiwa kuokolewa.
Chanzo: Michuzi Blog

HOFU YA MABADILIKO MAKUBWA POLISI

http://mtanzania.co.tz/wp-content/uploads/2016/02/IGP-Mangu.jpg
HOFU ya mabadiliko makubwa imetanda ndani ya jeshi la polisi, huku ikielezwa kuwa huenda yakamgusa Mkuu wa jeshi hilo, IGP Ernest Mangu, MTANZANIA imebaini.

Habari za uhakika ambazo gazeti hili limezipata Dar es Salaam kutoka kwenye vyanzo vyake zilieleza kwamba IGP Mangu ni miongoni mwa maofisa wa ngazi za juu wa jeshi hilo ambao huenda wakakumbana na mabadiliko hayo.

“Mabadiliko makubwa yanakuja na mmoja waoanayeguswa ni bosi wetu, IGPMangu.

Unajua ndani ya jeshi hili kuna mambo yanaonekana hayaendi vizuri hasa matukio ya ujambazi ambayo yamekuwa yakiendelea kila kukicha katikamaeneo mbalimbali nchini.

“Hata juzi umeona IGP Mangu kafanya mabadiliko ya makamanda wa polisi wa mikoa na wakuu wa vikosi kwa nia ya kuboresha utendaji ambao unaonekana kulegalega,” kilisema chanzo chetu.

Mtoa habari huyo alisema pamoja na hatua hiyo ya IGP Mangu, bado kuna baadhi ya viongozi wa juu nchini ambao wamekuwa hawaridhishwi na matukio kadhaa ikiwamo kurejea kwa kasi matukio ya ujambazi nchini.

Kutokana na hali hiyo kwa wiki ya pili sasa, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, amekuwa akifanya vikao na wakuu na watendaji kadhaa wa Jeshi la Polisi pamoja na wa idara zilizoko chini ya wizara hiyo.

Suala jingine linaloelezwa ni kulegalega kwa utendaji wa Jeshi la Polisi, hali ambayo imesababisha Waziri Kitwanga aombe msaada wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kudhibiti vitendo vya uhalifu ukiwamo ujambazi.

“Ni aibu na fedheha kubwa… kazi ya Jeshi la Polisi ni kulinda usalama wa raia na mali zao, lakini baada ya majambazi kuvamia benki ya Access kule Mbagala, JWTZ wameombwa washiriki kukomesha vitendo hivi… ni fedheha kwa jeshi la polisi.

“JWTZ kazi yao kubwa ni kulinda mipaka ya nchi wakati wote lakini sasa hatua ya kuanza kupambana na majambazi ni wazi polisi wameshindwa kazi ambayo ndiyo jukumu lao la msingi,” kilisema chanzo chetu.

IGP Mangu aliteuliwa kushika wadhifa huo Desembav30 mwaka 2013 na Rais mstaafu wa serikali ya awamu ya nne, Jakaya Kikwete.

Alichukua nafasi ya mkuu wa jeshi hilo aliyestaafu utumishi wa umma, IGP Said Mwema.

Kabla ya uteuzi huo, Mangu alikuwa Mkurugenzi wa Inteligensia ya Jinai katika jeshi hilo.

KAULI YA WAZIRI
Kutokana na taaarifa za mabadiliko hayo, MTANZANIA ilimtafuta Waziri Kitwanga ambaye alisema ameshtushwa na watu wanaosambaza taarifa za kuondolewa IGP Mangu, wakati yeye mwenyewe au Rais ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dk. John Magufuli, hana taarifa hizo.

“IGP haondolewi kwenye nafasi yake, Rais Magufuli ana imani naye kutokana na
utendaji kazi wake mzuri…sijui kwa nini watu wanasambaza taarifa za uongo maana maneno haya nimeyasikia, naomba uandike haya ninayoyasema.

“Mimi waziri mwenye dhamana ya Mambo ya Ndani sina taarifa yoyote juu ya kuondolewa IGP, Rais ana imani naye, lazima angenishirikisha katika suala hili nyeti, tungejadiliana ili kuona nini cha kufanya ila hayo ni maneno ya kusikia tu," alisema.

“Kutokana na utendaji kazi wake ndiyo maana tumekuwa tukishirikiana vizuri kuboresha jeshi letu, ndiyo sababu hata juzi mmeona tumefanya mabadiliko makubwa ya makamanda wa polisi wa mikoa na wakuu wa vikosi…sasa hili linatoka wapi?” alihoji Waziri Kitwanga.

Alisema mpaka sasa Rais Magufuli hajafikiria kufanya mabadiliko kwenye nafasi hiyo.

“Unajua Rais ana uamuzi wa mwisho. Kama waziri au IGP ameshindwa kutekeleza wajibu wake sawasaswa atamuondoa, hata kama ni mimi nitaondolewa kwa mamlaka ya uteuzi…lakini mpaka sasa majukumu tuliyokabidhiwa yanaendelea vizuri,” alisema Waziri Kitwanga.

IGP
Juzi IGP Mangu alifanya mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa na vikosi. Katika mabadiliko hayo alimteua Kamishina Msaidizi wa Polisi, Mihayo Msikhela kuwa Mkuu wa Kikosi cha Kupambana na Dawa za Kulevya.

Kabla ya Msikhela kuteuliwa kushika nafasi hiyo ya Godfrey Nzowa, alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga.

Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam juzi na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba, ilisema mabadiliko hayo ni ya kawaida kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za jeshi hilo.

Pia IGP Mangu alimhamisha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Polisi, Leonard Paul, kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga.
Chanzo: Nipashe

UNFPA YAITAJA TANZANIA KUWA MOJA YA NCHI TATU ZINAZOONGOZA KWA NDOA ZA UTOTONI


Imeelezwa kuwa Tanzania ni moja ya nchi ambayo bado inakabiliwa na changamoto ya ndoa za utotoni ambazo husabishwa na mila potufu, elimu duni na  umaskini unaopelekea wazazi kuwa na tamaa za kupata mali ili waweze kukidhi haja zao pamoja na sheria kandamizi.

Kwa mujibu wa takwimu kutoka Shirika la watu duniani (UNFPA) imeonyesha kuwa Tanzania ni nchi ya tatu inayoongoza kwa ndoa za utotoni duniani kwa kuwa na kiwango cha juu ukilinganisha na nchi zingine duniani.

Akielezea kuhusu ripoti hiyo, ofisini kwake,Mwanasheria wa TAMWA Bi. Loyce Gondwe alisema kuwa mikoa inayoongoza kwa ndoa za utotoni ni Shinyanga, Tabora, Mara, Dodoma, Lindi, Mbeya, Morogoro, Singida, Manyara, Mtwara, Pwani, Arusha, Kilimanjaro, Kigoma, Dar Es salaam na Iringa.

Bi.Gondwe, alisema kuwa kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kifungu cha 13 kimeruhusu mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 14 kuolewa kwa ridhaa ya mahakama na miaka 15 kwa ridhaa ya wazazi na mtoto wa kiume aliyefikisha umri wa miaka 18 anaweza kuoa.

Ameendelea kusema kuwa licha ya kuwepo kwa sheria ya mtoto ya mwaka 2009, inayotafsiri kwamba mtoto ni mtu yeyote mwenye umri chini ya miaka 18 bado sheria ya ndoa ya mwaka 1971 inawaruhusu watoto wa kike chini ya miaka 18 kuolewa na hivyo sheria ya ndoa kukinzana na sheria zingine.

Hata hivyo, alisema licha ya Tanzania kuridhia mikataba mbalimbali ya kimataifa inayopinga na kuzuia ndoa za utotoni, kama Mkataba wa Haki za watoto wa mwaka 1989, ambao unamtafsiri mtoto kama yeyote mwenye umri chini ya miaka 18 na Tamko la Haki za Binadamu ulimwenguni la mwaka 1948, Ibara ya 16(2) bado tatizo la ndoa za utotoni limeendelea kuwepo.

Naye mratibu wa kituo cha usuluhishi TAMWA, Bi. Gladness Munuo alisema kuwa ndoa za utotoni zina madhara mengi kwa mtoto ikiwemo kumyima haki yake ya msingi ya kupata elimu na hivyo kumpotezea ndoto zake za kimaisha.

Bi. Munuo alisema Ndoa za utotoni zinaweza kuleta madhara ya kiafya kwa mtoto ikiwemo magonjwa ya fistula, ulemavu wa kudumu kwa sababu viungo haviko tayari kushiriki tendo la ndoa na kushika mimba.

Aliendelea kusema kuwa mtoto mdogo anapoingia kwenye ndoa anakumbana na changamoto kubwa zingine za ndoa, kwa mfano migogoro ya ndoa kama vile kupigwa, kufukuzwa, ulevi, utelekezwaji ambavyo hupelekea madhara makubwa kwa mtoto katika maisha yake.

Hata hivyo alitoa wito kwa serikali, jamii, watu binafsi na  taasisi mbalimbali kulinda haki za watoto  ikiwemo kuchukua hatua ya kutoa taarifa sehemu husika ili suala hilo liweze kuchukuliwa hatua na kutatuliwa.
Chanzo: Mo Blog

MADUDU TENA BANDARINI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea bandari ya Mtwara juzi. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea bandari ya Mtwara juzi.  Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amekagua bandari ya Mtwara na kunusa ufisadi katika utoaji wa zabuni ya ujenzi wa gati mpya tatu.

Amekinyooshea kitengo cha manunuzi bandarini hapo, akisema kimekuwa chanzo cha upotevu wa fedha za serikali kutokana na ujanja wa watu wachache.

Waziri Mkuu aliigusa pia Bodi ya Korosho akisema yako majipu yanayohitaji kutumbuliwa kutokana na kukwamisha mizigo kupitia bandari ya Mtwara, badala yake inapitishwa kupitia bandari ya Dar es Salaam.

UTATA WA WAZABUNI
Majaliwa ambaye juzi alitembelea eneo la ujenzi wa gati hizo, alisema mzabuni ameshashinda, lakini yapo madai kwamba watu wa manunuzi kupitia Mamlaka ya Manunuzi ya Umma Tanzania (PPRA) ndiyo wanakwamisha zabuni hiyo.

Alisisitiza, “Natambua kwamba kuna mpango wa kujenga gati nne ambapo moja kati ya hizo itajengwa na TPA (Mamlaka ya Bandari) lakini hizi tatu zilitangazwa na kupata mzabuni ambaye ni kampuni ya Hyundai kutoka Japan. Lakini hii kampuni imekuwa ikizungushwa bila sababu. Tutafuatilia kubaini tatizo liko wapi.”

“Sasa hivi tuna uwezo wa kupaki meli moja tu, lakini gati zikikamilika tutaweza kuwa na meli tatu kwa mpigo, cha msingi tusimamie maamuzi yetu kwamba lazima wafanyabiashara wa korosho watumie bandari hii kusafirisha mizigo yao na si kuipeleka kwingine,” alisema.

KITENGO CHA MANUNUZI
Waziri Mkuu alimtaka Mkuu wa Bandari ya Mtwara, Prosper Kimaro kuwa makini na watu wa kitengo cha manunuzi katika bandari hiyo, akisema kimekuwa chanzo cha upotevu wa fedha za Serikali kutokana na ujanja wa watu wachache.

“Hapa si kuna mtu alitaka kuiba Sh milioni 300 kwa kufoji (kughushi) saini za wakubwa wake?” Alihoji Waziri Mkuu, swali ambalo lilijibiwa na Kimaro akikiri juu ya hilo na kusema, uongozi uliingilia kati kabla wizi huo haujakamilishwa.

BODI YA KOROSHO
“Kwenye Bodi ya Korosho nako kuna majipu yanahitaji kutumbuliwa. RCC (Baraza la Ushauri la Mkoa) ilishakaa na kupitisha uamuzi kuwa mizigo yote ipitie bandari ya Mtwara lakini kuna watu ndani ya Bodi hiyo wanatoa vibali vya kusafirisha mizigo kupitia bandari ya Dar es Salaam,” alisema Waziri Mkuu.

Aliomba wabunge wa Mkoa wa Mtwara washirikiane kusimamia ujenzi wa gati uanze mara moja, ili ajira kwa wananchi mkoani humo zipatikane.

“Ujenzi ukikamilika siyo tu ajira zitaongezeka bali hata meli nyingi zitaleta mizigo katika bandari hii na mapato ya mkoa yataongezeka”, alisema.

Fidia kisiwa cha Mgao Kuhusu fidia kwa wakazi wa vijiji vya Kisiwa na Mgao ambao wamekubali kuhama ili kupisha upanuzi wa bandari hiyo, Waziri Mkuu aliwahakikishia wabunge hao pamoja na uongozi wa bandari kwamba Sh bilioni 13.8 zimekwishatengwa na Wizara na zitatolewa mapema mwezi ujao.

Alitumia fursa hiyo kusisitiza udhibiti wa bandari bubu ambazo zinatumiwa kuingiza sukari na mchele na kuikosesha Serikali mapato.

“Mkuu wa Mkoa, nilikwishatoa agizo kama hilo wakati nimeenda kukagua bandari ya Tanga. Kaa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa nanyi pia muweke mbinu za kudhibiti upenyo huu wa kuingiza bidhaa za magendo kwa sababu hawa ndiyo wanaokwepa kulipa kodi ya Serikali,” alisisitiza.

Awali, Mkuu wa bandari ya Mtwara, Kimaro wakati akitoa taarifa ya utendaji wa bandari mbele ya Waziri Mkuu, alisema ilianzishwa mwaka 1950 na imekuwa ikikabiliwa na ufinyu wa gati ya kuegesha meli, vifaa vya kupakulia na kupakia mizigo.

Alisema hivi sasa wamekwishapata winchi ya bandarini yenye uwezo wa kubeba tani 100 na wako kwenye mpango wa kujenga gati moja.

MAJIPU BANDARINI
Waziri Mkuu, Majaliwa ameshafanya ziara kwenye Bandari za Dar es Salaam, Tanga na sasa Mtwara ambako amebaini mambo mengi hayaendi vizuri hali ambayo amekuwa akilazimika kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kuwajibisha watendaji.

Chini ya mkakati wa Serikali ya awamu ya tano ya kutumbua majipu, Rais John Magufuli alivunja bodi simamizi ya bandari siku chache baada ya kupatikana kwa kontena ambazo hayakuwa yamelipiwa ushuru Bandari ya Dar es Salaam.

Kampuni 43 ziligunduliwa kuhusika katika makontena hayo. Mwenyekiti wa Bodi, Profesa Joseph Msambichaka sanjari na Mkurugenzi Mkuu wa Bandari, Awadhi Massawe walivuliwa nyadhifa zao .

Pia Katibu mkuu wa wizara ya uchukuzi, Dk Shaban Mwinjaka aliondolewa kwenye wadhifa huo. Waziri Mkuu, Majaliwa alipofanya ziara ya kushitukiza katika bandari ya Dar es Salaam, aligundua kontena 329 zilipitishwa bila kulipiwa kodi kinyume na utaratibu wa bandarini.

Aidha, Waziri Mkuu, hivi karibuni alifanya ziara ya kushitukiza katika Bandari ya Tanga ambako pamoja na masuala mengine, alikuta tishali tatu zikiwa chakavu bila ya injini wakati serikali ilitoa fedha za ununuzi wa matishali ya kisasa.

Baada ya kubaini jipu hilo, alimwagiza Meneja wa Bandari ya Tanga, Henry Arika kutoa maelezo kwa maandishi ya nani alihusika na ununuzi wa matishali hayo badala ya zile mbili zilizopaswa kuwapo ambazo Serikali ilitoa dola za Marekani milioni 10.

Arika alijitetea kwamba tishari hizo ziliwasili nchini miaka minne iliyopita iliyopita lakini zilianza kufanya kazi rasmi mwaka jana na kwamba yeye hana muda mrefu katika bandari hiyo
.
Chanzo: Habari Leo

NAIBU SPIKA AKAANGWA KWA MAFUTA YAKE


Mbeya/Dar.  Naibu Spika, Dk Tulia Ackson amesema kazi za Mbunge si kupiga kelele bungeni ili aonekane kwenye luninga, bali ni ushiriki wake katika kazi za maendeleo kwenye jimbo lake.

Lakini kauli hiyo imepingwa vikali na baadhi ya wabunge wa upinzani ambao wamesema ukosefu wa uzoefu ndiyo uliomfanya atamke hayo.

Dk Ackson ambaye ameingia kwa mara ya kwanza kwenye chombo hicho kwa kuteuliwa na Rais na baadaye kushinda uchaguzi wa Naibu Spika baada ya kupitishwa na CCM, alitoa kauli hiyo juzi usiku jijini Mbeya wakati wa hafla ya kumpongeza kwa kuchaguliwa kushika nafasi hiyo iliyoandaliwa na wadau wa maendeleo wa mikoa ya Mbeya na Songwe.

Aliwataka wananchi kuacha kuwafurahia wabunge wanaozungumza kwenye Bunge bila kuonesha vitendo kwenye majimbo yao.

Alisema hata kama Mbunge hapati fursa ya kuzungumza chochote bungeni, hilo lisiwape shida badala yake waangalie anavyofanya kazi kwenye jimbo.

"Angalieni wabunge wenu wanafanya nini majimboni ukilinganisha na kuonekana kwenye TV, na pia pimeni mambo anayozungumza kama yana faida kwa jamii au la," alisema.

WABUNGE WAMJIBU
Lakini kauli hiyo ilijibiwa vikali na wabunge.  Mbunge wa Kaliua (CUF), Magdalena Sakaya alisema kauli ya Naibu Spika imemkera na ni hatari kutolewa na kiongozi kama yeye.

Sakaya, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF, alisema Dk Acksno anafahamu kwamba kazi za Mbunge ni kuisimamia na kuishauri serikali na kutunga sheria na wanatakiwa kuisimamia serikali ili kuhakikisha bajeti iliyopitishwa inatekelezwa.

"Utafanyaje kazi hizo bila kuzungumza bungeni?  Anataka kutueleza kwamba tunauza sura kwenye televisheni?  Tunamsubiri huyo amenikasirisha sana," alisema.

Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa alisema "Naibu Spika ni Mbunge wa kuteuliwa.  Hajawahi kuchaguliwa kuwakilisha wananchi ndiyo maana anatoa ujumbe unaopotosha wananchi."

Mbunge wa viti maalumu (Chadema), Suzan Lyimo alisema wabunge wanatakiwa kuzungumza wakati wowote ili kuibana Serikali, lakini vikao vikiisha wanakwenda majimboni.

Mbunge wa Kilwa Kusini (CUF), Suleiman Said Bungara alisema moja ya kazi za wabunge ni kuisimamia na kuishauri Serikali.
Chanzo: Mwananchi

UTANI WA MPIRA WASABABISHA KIFO CHA MWANAFUNZI

Mbeya.  Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari ya Kinyara wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya, Deogratius Mwanangwa amefariki dunia kwa madai ya kusukumwa na mwanafunzi mwenzake na kuanguka kutoka kwenye kitanda cha juu 'deka.'

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku wakiwa bwenini.

Alisema wanafunzi hao walikuwa wakibishana kuhusu Simba na Yanga.

Msangi alisema Mwanangwa aliwahishwa hospitali ya Igogwe kwa matibabu lakini alifariki dunia.

Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Oyeti Mwakosya alisema mwanafunzi huyo alifikishwa hospitali akiwa amepoteza maisha.

Dk. Mwakosya alisema uchunguzi ulibaini kuwa kifo chake kilitokana na mtikisiko wa ubongo.
Chanzo: Mwananchi

POLISI APIGWA RISASI SIKU YAKE YA KWANZA KAZINI

Polisi mmoja wa kike nchini Marekani amepigwa risasi na kuuawa katika siku yake ya kwanza kazini.

Askari huyo bi Ashley Guindon alikula kiapo mapema siku hiyo hiyo kisha akaelekezwa na wakubwa wake kwenda nyumbani kwa mama mmoja kutatua mzozo wa kinyumbani katika kitongoji Washington, DC.

Bi Ashley akiandamana na wenzake wawili walikwenda Woodbridge, Virginia, kilomita 32 kusini mwa Washington lakini walipofika huko walifyatuliwa risasi na kwa bahati mbaya Ashley hakubahatika.

Wenzake wawili pia walijeruhiwa vibaya na wamelazwa hospitalini.
Mshukiwa wa mauaji hayo ni mlengaji shabaha katika jeshi la Marekani aliwazidi maarifa maafisa hao wachanga.

Mwanajeshi huyo alikamatwa baadaye na vitengo maalum vya polisi.

Mwanjeshi huyo alikuwa amempiga risasi na kumuua mkewe papo hapo kabla ya Ashley na wenzake kutokea.

Hakukuwa na mtoto nyumbani wakati wa ufyatulianaji huo wa risasi.

Afisa mkuu wa kituo "Tunasikitika kuwatangazia kifo cha afisa wa polisi wa kituo cha Prince William County bi. Ashley Guindon, aliaga dunia kufuatia ufyatulianaji risasi katika mtaa wa Lashmere Ct akiwa kazini".
Chanzo:  BBC Swahili

AL-SHABAB YAWAUA 24 WAKITAZAMA MAN U-ARSENAL

al shabaab
Watu 24 wameuawa mjini Baidoa Kusini mwa Somalia wakitazama mechi baina ya Manchester United na Arsenal baada ya shambulizi lililotekelezwa na Al-Shabab.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa milipuko miwili mikubwa ilitokea, katika mkahawa huo uliokuwa umejaa mashabiki wa mechi kati ya Manchester United na Arsenal.

Miongoni mwa wale waliouawa ni pamoja na Afisa wa serikali ya jiji hilo.

Mji wa Baidoa ulitekwa na wapiganaji wa Kiislamu wa Al-Shabaab mwaka wa 2008, lakini walitimuliwa mwaka 2012.

Mji huo ulioko takriban kilomita 200 kutoka mji mkuu Mogadishu ni mji wa hivi punde zaidi kushambuliwa na wanamgambo hao wa kiislamu.

Shambulizi la kwanza lilitokea katika mgahawa maarufu unaopendwa na wageni na viongozi wa kisiasa ambao ulishambuliwa kwa gari lililokuwa limetegwa bomu.
Walionusurika waliokolewa na wanajeshi wa muungano wa Afrika AMISOM.

Shambulizi hili limetokea muda mchache tu baada ya kukamilika kwa warsha ya viongozi wa mataifa yanayochangia wanajeshi wake katika jeshi la muungano wa Afrika AMISOM.

Siku ya Ijumaa watu wengine zaidi ya 20 waliuawa katika mgahawa mwengine kufuatia shambulizi la Al-Shabaab
.
Chanzo: BBC Swahili