![]() |
Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama ambaye pia ni Mwenyekiti wa tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika hivi karibuni jijini Mwanza, akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari alipokuwa akizungumza nao ofisi kwake, Kinondoni jijini Dar es Salaam leo. |
WAZIRI
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye anatarajiwa kuwa
mgeni rasmi kwenye Tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika jijini
Mwanza mnamo Machi 27.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maaandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama,amebainisha kuwa Waziri Nape amekubali kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo ambalo litaanzia Geita Machi 26 na kumalizia Kahama Machi 28.
Msama alisema kamati yake inaendelea na maandalizi ya kuelekea tamasha hilo ambalo litashirikisha waimbaji mbalimbali hapa nchini.“Maandalizi kuelekea Tamasha la Pasaka yanaendelea vema, hivyo wakazi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa wajiandae kupokea ujumbe wa neno la Mungu kupitia viongozi wa dini na waimbaji wa muziki wa Injili,” alisema Msama.
Msama alisema baadhi ya waimbaji waliothibitisha kushiriki tamasha hilo ambao ni pamoja na Rose Muhando, Bonny Mwaitege, Upendo Nkone, Jesca BM Honore, Christopher Mwahangila, Joshua Mlelwa, Sifael Mwabuka, Jenipher Mgendi, Kwaya ya AIC Makongoro na Kwaya ya Wakorintho Wapili.
Msama pia alidokeza kuhusiana na suala zima la viingilio,alisema kuwa viingilio hivyo vinaendana na tukio hilo ambalo mbali ya kumuimbia na kumtukuza Mungu pia lina dhamira ya kusaidia jamii yenye uhitaji maalum.
“Nawaomba wakazi wa mikoa Geita, Mwanza na Shinyanga kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha tamasha hilo,” alisema Msama.
Msama alisema kupitia viingilio vya tamasha hilo wanatarajia kutoa kipaumbele kwa wakazi wa mikoa itakayopitiwa na tamasha kwa kupatiwa baiskeli zaidi ya 100 za walemavu, ambazo zitagawiwa mikoa mbalimbali.

No comments:
Post a Comment