Mbeya. Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari ya Kinyara wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya, Deogratius Mwanangwa amefariki dunia kwa madai ya kusukumwa na mwanafunzi mwenzake na kuanguka kutoka kwenye kitanda cha juu 'deka.'
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku wakiwa bwenini.
Alisema wanafunzi hao walikuwa wakibishana kuhusu Simba na Yanga.
Msangi alisema Mwanangwa aliwahishwa hospitali ya Igogwe kwa matibabu lakini alifariki dunia.
Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Oyeti Mwakosya alisema mwanafunzi huyo alifikishwa hospitali akiwa amepoteza maisha.
Dk. Mwakosya alisema uchunguzi ulibaini kuwa kifo chake kilitokana na mtikisiko wa ubongo.Chanzo: Mwananchi

No comments:
Post a Comment