Diwani wa kata ya Ng'ang'ange wilaya ya Kilolo Bw Namgalesi Lusumsuva akisisitiza jambo baada ya kutoa maamuzi magumu ya kuteua majina mawili ya mabinti ambao watakaimu nafasi ya afisa mtendaji wa kijiji cha Ng'ang'ange kabla ya wananchi kumpinga, kulia ni Mbunge wa jimbo la Kilolo Venance Mwamoto. |
Mbunge Mwamoto akimpatia namba ya simu mmoja kati ya wasanii kijiji cha Ng'ang'ange anayeomba kufika kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa albamu yake. |
DIWANI wa kata ya Ng'ang'ange wilaya ya kilolo mkoani Iringa Bw Namgales Msuva (CCM) amejikuta katika wakati mgumu mbele ya mbunge wa jimbo la Kilolo Bw Venance Mwamoto baada wananchi kumzomea kama njia ya kupinga uteuzi wake usio shirikishi wa makaimu wawili watendaji wa kata ya Ng'ang'ange .
Wananchi hao walifikia hatua hiyo jana wakati wa mkutano wa hadhara wa mbunge wao kuwashukuru kwa kumchagua kuwa mbunge wao katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana .
Kabla ya diwani huyo kupingwa mbele ya wananchi na mbunge kuingilia kati kutuliza jazba za wananchi hao ,alikuwa amewateua wasichana wawili wakazi wa kijiji cha Ng'ang'ange akiwemo Felista Ngogo ambae alikuwa akikaimu nafasi hiyo na msaidizi wake Flora Magoda kuendelea kukaimu nafasi hiyo .
Kwani diwani huyo alisema kuwa sababu ya yeye kufanya uteuzi huo ni baada ya awali kuteua mtendaji wa muda ambae aliacha nafasi hiyo baada ya wananchi kuonyesha kumpuuza katika maagizo mbali mbali aliyoyatoa.
Hivyo alisema haiwezekani ofisi hiyo kukosa afisa mtendaji wa kata kwa zaidi ya miezi 6 hivi sasa na yeye akiwa kama mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya kata hiyo na diwani ameamua kufanya uteuzi wa maofisa hao watendaji wawili badala ya mmoja ili kuifanya kazi hiyo.
" Mtendaji katika ofisi hii ya kata hayupo na ofisi imekuwa ikifungwa muda wote .....utendaji kata si ajira halipwi chochote sasa mimi kama diwani na mwenyekiti wa kata natumia nafasi yangu kuwateua mabinti hawa wawili ambao wataifanya kazi hii ya kujitolea kuanzia leo nimeona tunalala sana .....natoa amri kuanzia sasa mnanisikiliza " alisisitiza diwani huyo
Huku akitaka wananchi ambao wanatuhumiwa kwa ushirikina na pamoja na vijana wanaoshinda vijiweni kufikishwa mbele ya ofisi yake ya kata haraka ili kuchapwa viboko.
Hatua hiyo ya uteuzi wa maofisa watendaji hao ilipelekea mkutano huo wa mbunge kuvurugika kwa muda baada ya wananchi hao kupinga ubabe wa diwani wao huyo kwa kufanya uteuzi pasipo kushirikisha baraza la maendeleo ya kata wala wahusika wenyewe kushirikishwa .
Wananchi hao walisema hawautambui uteuzi wa maofisa hao wa kata na kuwa hao aliowateua ni maofisa wa nyumbani kwake na sio katika ofisi hizo za serikali ngazi ya kata .
Mbali ya wananchi kuzomea na kumkataa diwani huyo kwa maamuzi yake pia mabinti hao walijitokeza hadharani na kukataa uteuzi huo kuwa hauna maslahi kwao na wao hawajashirikishwa kabla ya kutangazwa hivyo hawapo tayari kufanya kazi hiyo kutokana na diwani kutowashirikisha mapema .
Mbunge wa Kilolo Bw Mwamoto alilazimika kusimama na kusitisha uteuzi huo kufuatia maombi ya wananchi kumtaka kuingilia kati maamuzi ya diwani huyo ambayo hayakushirikisha kiongozi wala mjumbe mwingine yeyote wa ngazi ya kijiji wala kata.
Bw Mwamoto alisema anasitisha uteuzi huo wa diwani kwa watendaji hao na yeye kama mbunge atawasiliana na ofisi ya mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo ili baada ya ajira mpya za watendaji kutolewa basi kata hiyo kupewa kipaumbele na kwa sasa wakati zoezi hilo bado kufanyika mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Ng'ang'ange ataendelea kukaimu nafasi ya utendaji wa kata pia.
Maamuzi hayo ya mbunge Mwamoto alionyesha kuwafurahisha wananchi hao wakiwemo wale wa upinzani kutoka chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema ) ambao walimpongeza mbunge kwea busara zake na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa mbunge huyo na mwenyekiti aliyeteuliwa kukaimu utendaji wa kata.

Mbunge wa Kilolo Bw Venance Mwamoto wa
kwanza kulia akicheza ngoma ya njuga na wasanii wa asili kijiji cha
Ng'ang'ange baada ya kufika katika mkutano wa hadhara.

No comments:
Post a Comment