Pages

Wednesday, October 17, 2018

AMUNIKE: MSIPOTEZE MATUMAINI NA TIMU YENU

Kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike akiongea na Waandishi wa Habari jana.

Baada ya Taifa Stars kufanikiwa kulipa kisasi dhidi ya Cape Verde uwanja wa Taifa Dar es Salaam kwa kuwafunga magoli 2-0, kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ambaye ni raia wa Nigeria Emmanuel Amunike alifunguka na kutoa ujumbe kwa watanzania.

“Ilikuwa ni mechi ngumu sana kwetu. Cape Verde ni timu ambayo naifahamu kwa miaka mingi, wameimarika sana na wana wachezaji wengi wanaocheza Ligi ya Ureno na wanaocheza Ufaransa."

Wachezaji wao wanajua nini cha kufanya wakiwa na mpira na wanajua nini cha kufanya wakiwa hawana mpira nimekuwa nikisema Tanzania imebarikiwa wachezaji wengi tunachotakiwa kufanya ni kuamini timu yetu,” amesema Amunike.

“Tumerudi nyumbani tukiwa tumefungwa magoli 3-0, kila mmoja akawa na mashaka na sisi, nataka mjue kitu kimoja hakuna safari isiyokuwa na changamoto.  Baada ya kufungwa magoli matatu mashabiki wengi hawakuja lakini nawataka wasipoteze matumaini katika timu yao.”

No comments: