Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani). |
Serikali imesema kuwa haitaruhusu vyombo vya nje kuingia nchini kwa
ajili ya kuchunguza sakata la kutekwa kwa bilionea Mohammed Dewji kwani
ni suala ambalo liko ndani ya uwezo wa vyombo vya ndani.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema kuwa Jeshi la Polisi lina wataalamu
ambao wana uwezo na weledi wa kuweza kushughulikia suala hilo.
“Kuna haja gani ya kuleta vyombo vya nje wakati tuna jeshi bora na
lenye uelewa mkubwa licha ya kukabiliwa na changamoto za hapa na pale,”
Masauni anakaririwa.
Kauli hiyo ya Masauni imekuja wakati ambapo Waziri kivuli wa Mambo ya Ndani, Godbless Lema amezungumza na waandishi wa habari ambapo pamoja
na mambo mengine aliitaka Serikali kuruhusu vyombo vya nje kuchunguza
sakata hilo.
No comments:
Post a Comment