Pages

CHEKA

******************************************************************

CHIZI NA BARUA

Jamaa alimkuta chizi anaandika barua, akamuuliza "unamwandikia nani hiyo barua?" Chizi akamjibu "najiandikia mwenyewe." 

Jamaa akamuuliza tena "inahusu nini?" Chizi akamjibu kwa mshangao, "wewe mwehu nini? sasa nitajuaje wakati barua bado haijanifikia?"

**********************************************************************************

MTOTO NA SALA

Watoto wa siku hizi tofauti na sisi tulivyokuwa zamani.  Hebu msikie huyu mtoto:
Mtoto alikuwa anapata shida kusali kila muda wa kulala sababu sala ilikuwa ndefu akaona aandike ile sala yote akaibandika ukutani.  Ikawa ikifika muda wa kulala anasema "ee Mungu, SOMA PALE. Amina."  ha ha haa chezeya watoto wa dotcom wewe............

*****************************************************************

JEURI

Ukiwa jeuri ujue kuna jeuri zaidi yako.  Daladala iliondoka Kariakoo kufika Manzese konda akauliza "kuna mtu anashuka?"  Dada mmoja akajibu "tumeziacha nyumbani, tuna mitandio tu!".  Kufika mbele yule dada aliyejibu kwa nyodo akawa anashukia Ubungo Maziwa akasema "Konda, nashuka Maziwa." Konda akamjibu "kayanunulie sidiria yasishuke." kwi kwi kwi........
*****************************************************************

Binti alisafiri kwenda China kwa miaka 20. Alipofika akawatumia wazazi wake kichupa cha dawa wanywe tone moja moja ili wasizeeke.

Baada ya miaka 20 mtoto aliporudi alimkuta mama yake kawa binti huku kabeba katoto ka kiume mgongoni, akafurahi sana kumkuta mama yake kawa binti, akamuuliza "mama, baba yuko wapi?", mama yake akamjibu "mwanangu, baba yako alivyoniona nimekuwa binti yeye akanywa kichupa chote ndio huyu nimembeba mgongoni."  Teh teh, chezea wachina wewe!

*****************************************************************

MLEVI

Mlevi mmoja alipita mtoni akakuta watu wanabatizwa.  Mlevi akajua kuna kitu wanatafuta kwa kuwa mchungaji alikuwa anawazamisha na kuwatoa kwenye maji.  Mlevi nae akaamua kupanga foleni, ilipofika zamu yake mchungaji akamzamisha alipomtoa akamuuliza, "umempokea Yesu?" mlevi akajibu "hapana."

Mchungaji akamzamisha tena alipomtoa akamuuliza tena "umempokea Yesu?", akajibu "hapana," mara ya tatu akamuuliza "umempokea Yesu?" mlevi akasema "mchungaji una uhakika alizama hapa au unanisumbua tu?"......


 

KUSOMA MUHIMU!!

Jamaa mmoja alikwenda kwenye hoteli moja ya kifahari, watu wote pale hotelini wanaongea kiingereza.  Basi jamaa alipokuwa chumbani akamuona panya, akapiga simu reception ili asaidiwe huku akiwa hajui panya anaitwaje kwa kiingereza.  Maongezi yao yalikuwa kama ifuatavyo:

MHUDUMU:  Thank you for calling reception, can I help you?
JAMAA:  Do you know Tom and Jerry?
MHUDUMU:  Yes, I know. 
JAMAA:  Ok, Jerry is here.
Mhudumu hana mbavuu...... ha ha haaaa

**********************************************************************************
MBUMBUMBU....!
Mwanafunzi mmoja wa kidato cha IV akiwa kwenye chumba cha mtihani wa hesabu, ghafla baada ya dakika 30 akatoka kwenye kiti akakaa sakafuni.  Msimamizi akamshangaa ikabidi amuulize "kwanini umekaa chini?"

Mwanafunzi akajibu, swali hili la 9 linasema 'SOLVE THIS QUESTION WITHOUT USING TABLES"
  Msimamizi hoooi kwa kicheko......... ha ha haaa, chezea shule za Kata wewe!

**********************************************************************************


UKIMWI

Bibi alikuwa anafua nguo za mjukuu wake aliekufa kwa ukimwi.  Katika fuafua akakutana na bikini, bibi akashangaa akajisemea mwenyewe "Khaa ugonjwa huu kweli mbaya sana, unakondesha mpaka chupi!" teh teh teh

******************************************************************
 
MBWA KOKO

Mbwa koko wawili walikuwa wanasaka chakula kwenye jalala, mara ikapita Land Rover ya FFU na ndani yake kuna mbwa wa polisi. Mbwa koko mmoja akaangalia kwa uchungu kisha akamwambia mwenzie "unaona wenzetu waliosoma walee wanaenda kazini."

******************************************************************
WANAUME NA SEMINA

Wanaume walikuwa kwenye semina wakaulizwa mara ya mwisho kumwambia mkeo kuwa unampenda ni lini?  wengine wakasema leo asubuhi na wengine wakasema muda sio mrefu.  Muwezeshaji akawaambia kila mmoja sasaivi amuandikie mkewe sms amwambie nakupenda mke wangu halafu badilishaneni simu kila mmoja asome majibu ya mwenzake.  Majibu yalikuwa hivi:
1.  Unaota au?
2.  Umekumbwa na nini?
3.  ?
4.  Utanieleze hii sms ulikuwa unatuma kwa nani.
5.  Leo sikusamehe, najua kuna kitu.
6.  Huyo uliye nae ndio kakwambia unitumie hii sms?
7.  Najua tu tayari kuna kitu.
8.  Wewe sema unachotaka!
9.  Leo hunipati ng'o!
10. Nani mwenzangu??

*******************************************************************

UMBEA NOMA


Binti kakaa kwenye daladala anaandika sms huku kashika kabegi kake.  Mzee mmoja pembeni akawa anakomaa kuangalia binti anaandika nini.  Binti akastukia, akaamua kuandika hivi: "yule nyoka utakuwa hujamtoa meno ya sumu, anasumbua kwenye begi anataka kutoka, sijui nifanyeje na alivyo mkubwa sijui itakuwaje?"

Mzee kuona vile akasogea pembeni, binti nae hakumchelewesha akamrushia begi! Mzee akakurupuka huku anapiga kelele "nyokaa nakufaa!" Binti akamwambia "ukome kusoma sms za watu" Teh teh teh.........

*****************************************************************
ARE YOU RELAXING?

Jamaa mmoja alikuwa ametulia beach, mzungu akapita akamuuliza "are you relaxing?", jamaa hakuelewa akamjibu tu "No" akapita mwingine akamuuliza tena vile vile, jamaa akajibu tena "no", akaona hapa nasumbuliwa sana akasogea mbele kidogo ufukweni akamuona mzungu ametulia akamuuliza "are you relaxing?" mzungu akamjibu "yes".  Jamaa akamkata makofi mawili na kumwambia "pumbavu, kumbe wewe ndio relaxing, inuka unatafutwa na wenzako.  Shenzi wewe mi naulizwaulizwa pale wewe unaangalia tu"...... kwi kwi kwi..........

*****************************************************************

SIMU MPYA

Dingi kanunua simu mpya akiwa na mwanae sebuleni akitest milio
Kwa bahati mbaya dingi akajamba "Pwiii.."
Katoto kakadakia: usiweke huo baba una harufu mbaya.

*****************************************************************


MIA TANO

Mjukuu kamnong'oneza babu yake sikio la kushoto kamwambia babu naomba mia tano. Kwa kuwa babu alikuwa hana pesa kaona mia tano kubwa kamwambia mjukuu wake sijasikia vizuri hebu njoo uninong'oneze kwenye sikio hili linguine.  Mjukuu akaenda sikio la pili akasema babu naomba sh elfu saba, babu akajibu mmh bora urudi kwenye sikio lile lile la mia tano!
*****************************************************************
JAMAA NA PAKA

Jamaa mmoja alimchukua paka wake na kwenda kumtupa mbali, aliporudi nyumbani alimkuta paka amekwisharudi.

Jamaa alikasirika sana! Siku ya pili akamchukua na kwenda naye mbali zaidi ya kilometa 50, akapita uchochoro nyingi asizozijua kisha akamtupa, akaanza safari ya kurudi nyumbani. Baada ya muda akampigia simu mkewe...

Jamaa: "vipi mke wangu huyo paka kaonekana hapo?"
Mke: “ndiyo mume wangu yuko hapa tena ametulia, kwani vipi imekuaje?”
Jamaa: “hebu mpe simu anielekeze njia ya kurudi!”

No comments: