DAR ES SALAAM. Mbunge wa Songea Mjini (CCM), Leonidas Gama amefariki dunia katika hospitali ya Peramiho mkoani Ruvuma.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma, Ndugu Oddo Mwisho amethibitisha kutokea kwa kifo hicho ambapo amesema kuwa yeye alipata taarifa usiku wa kuamkia leo.
"Nimepata taarifa jana usiku kuwa Gama amefariki kwa kuugua shinikizo la damu. Tunawasiliana na familia ili kujua utaratibu wa mazishi." amesema Mwisho.
Marehemu Gama ameshawahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kabla ya kuwa Mbunge katika uchaguzi wa mwaka 2015.
Mungu ailaza mahali pema peponi roho ya marehemu Leonidas Gama. Amen.

No comments:
Post a Comment