Pages

Friday, November 24, 2017

MPANGO WA MATIBABU BURE KUWAFIKIA WAZEE WA HANDENI



Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe amewahamasisha wazee wilayani humo wanaoanzia umri wa miaka 60 na kuendelea kujitokeza kwenye zoezi la upigwaji picha ili waweze kupatiwa kadi za bima ya afya zitakazowawezesha kupatiwa matibabu bure kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitali.

Hayo ameyazungumza jana wilayani humo mara baada kuwasili katika Ofisi za Mtendaji Kata ya Kabuku kuhamasisha huduma za afya.

Hatua hiyo ni muendelezo wa agizo la serikali ya awamu ya tano ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kuhakikisha wazee kuanzia umri wa miaka 60 na kuendelea wanapatiwa matibabu bure. 


Wazee wa wilaya ya Handeni wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa wilaya, Godwin Gondwe (hayupo pichani).
Diwani wa Kata ya Kabuku, Amina Mnegelo akizungumza machache mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe huku wazee wakimfuatilia kwa makini.

No comments: