Pages

Wednesday, August 24, 2016

SHULE BINAFSI ZACHIMBIWA KABURI


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe Prof. Joyce Ndalichako.
SOKO la shule binafsi za sekondari nchini liko hatarini kutokana na uamuzi wa serikali wa kuboresha shule zake 89 ili ziwe za mfano.

Akizungumza katika mahojiano maalumu jijini Dar es Salaam juzi, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako alisema kuwa shule hizo zitafanyiwa marekebisho makubwa ya kuanzia kujenga miundombinu upya ikiwa ni majengo yote pamoja na kuzipa walimu wengi na vifaa vya kutosha vya kujifunza na kufundishia.

Serikali imekuja na mpango huo wakati huu tayari inatekeleza sera ya kutoa elimu bura kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne.

Uamuzi wa serikali ni wazi utaua soko la shule binafsi ambazo katika miaka ya karibuni zimeanzishwa kwa wingi na zimekuwa zikilalamikiwa na wazazi kwa kutoza ada kubwa.

Chanzo: Nipashe

No comments: