Pages

Wednesday, August 24, 2016

WANAFUNZI 316 WAIGEUZIA KIBAO TCU; WAIDAI SHILINGI BIL. 5/-

Umati wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha St. Joseph.

WANAFUNZI 316 wa Chuo Kikuu cha St. Joseph ambao walikatishwa masomo yao, wameifikisha mahakamani Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) na chuo hicho wakitaka kulipwa zaidi ya shilingi bilioni 5.

Wanafunzi hao wameomba kulipwa fedha hizo ambazo ni ada walizolipa na fidia ya usumbufu walioupata kutokana na kusimamishwa kuendelea na masomo kwa madai ya kukosa sifa.

Kesi hiyo ya madai, imefunguliwa Mahakama Kuu, kanda ya Dar es Salaam na imepangwa kusikilizwa na Jaji Winfrida Korosso.

Walalamikaji hao wanawakilishwa na wanafunzi Ramadhani Kipenya, Innocent Peter, Faith Kyando na Mohammed Mtunguja, ambao wameifungua kesi hiyo kwa niaba ya wenzao 312.
Chanzo: Nipashe

No comments: