Pages

Saturday, April 30, 2016

MBUNGE WA JIMBO LA VUNJO ,JAMES MBATIA AKABIDHI MSAADA WA CHAKULA KWA WAHANGA WA MAFURIKO.

Diwani wa kata ya Kahe ,Rodrick Mmanyi akizungumza baada ya Mkurugenzi wa Idara ya Maafa nchini,Brigedia Jenerali ,Mbazi Msuya kutembelea kata hiyo kutizama athari zilizotokana na mafuriko.
Baadhi ya wakazi wa kata ya Kahe wakiwa katika kikao na ujumbe wa Mbunge wa jimbo la Vunjo uliofika katika kata hiyo kwa ajili ya kutoa msaada wa chakula.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya  Moshi,Michael Kilawila akizungumza na kutoa pole kwa wakazi wa kata ya Kahe waliofikwa na maafa yaliyotokana na mafuriko.
Mkurugenzi wa Idara ya Maafa nchini,Brigedia Jenerali ,Mbazi Msuya akizungumza na wakazi wa kata ya Kahe baada kutembelea maeneo mbalimbali yaliyoathirika na mafuriko.
Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akizungumza katika kikao hicho kilicho fanyika ofisi ya kata ya Kahe ,kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Maafa nchini ,Brigedia Jenerali,Mbazi Msuya,kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila.

No comments: