![]() |
Mwili wa mwanamuziki Papaa Wemba ukiwasili nchini Congo. |
Mamia ya watu wamekongamana nje ya uwanja wa ndege wa Kinshasa kuupokea mwili wa mwanamuziki Papa Wemba uliowasili nchini humo kutoka Abidjan, Ivory Coast.
Mwanamuziki huyo ambaye ametajwa kuwa mmoja ya waanzilishi wa muziki wa kizazi kipya cha Soukous anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumanne baada ya mwili huo kuwekwa katika uwanja wa mpira kwa raia kutoa heshima zao za mwisho.
Maafisa wa serikali na wanadiplomasia watahudhuria ibada ya kumkumbuka mwanamuziki huyo katika uwanja wa ndege kabla ya mwili huo kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti.

Marehemu Papaa Wemba, enzi za uhai wake. |
Tamasha la bure la usiku kucha lilifanyika mjini Abidjan ambapo mwanamuziki huyo alianguka alipokuwa akiimba.Mwanahabari wa BBC Tamasin Ford anasema kuwa mashabiki wengi walivalia nguo nyeusi na kubeba mishumaa ili kutoa heshima kwa nguli huyo wa muziki.
Mkewe Papa Wemba na wasaidizi wake pia walikuwepo.
Mkewe Papa Wemba na wasaidizi wake pia walikuwepo.
![]() |
Mwanamuziki Fally Ipupa (mwenye kofia) akiwasili uwanja wa ndege kuulaki mwili wa marehemu Papaa Wemba. |
Baadhi ya watu maarufu waliowasili kuulaki mwili wa mawanamuziki nyota katika uwanja wa ndege nchini DRC ni pamoja na mwanamuziki mashuhuri Fally Ipupa pamoja na mtu anayemwigiza aliyekuwa Rais wa DRC Mobutu Seseseko.
Papa Wemba ambaye jina lake halisi ni Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba, alianguka na kufa jukwaani akiwatumbuiza maelfu kwa maelfu ya mashabiki wake waliojitokeza katika tamasha la muziki mjini Abidjan Ivory Coast.
Gwiji huyo wa muziki wa lingala alizaliwa mnamo Juni 14 mwaka 1949, katika eneo la Lubefu - Wilaya ya Sankuru nchini Congo.

Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment