Pages

Saturday, June 21, 2014

LEO NDIO LEO!! MISS MSASANI 2014 KUPATIKANA LEO LE TASI LOUNGE (BUSINESS PARK), VICTORIA



Warembo wa Miss Msasani 2014 wakiwa katika pozi.


Warembo wa Miss Msasani 2014 wakiwa na Kamati ya Miss Tanzania.
Na Mwandishi wetu

BENDI ya muziki wa dansi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma', leo watapamba jukwaani katika shindano la kumtafuta mrembo wa Msasani (Miss Msasani 2014).

Mratibu wa mashindano hayo, Shabani Tolle amesema  taratibu zote zimekamilika ikiwa ni pamoja na warembo wote watakaopanda jukwaani kuwania taji hilo kuwa katika hali nzuri kiafya.

Tolle amesema mashindano hayo yatakayoshirikisha jumla ya walibwende 15 yatafanyikia kwenye ukumbi wa Le Tasi Lounge uliopo Moroco jijini Dar es Salaam kwa kudhaminiwa na Integrated Communications, CXC Africa, Merry Light, Tambaza Action Mart, Event Light, E Tatu Maliaga Interprises, Clouds FM na Le Tasi Lounge.

Ameongeza kwa kuwataja warembo watakaopanda jukwaani kuwania taji hilo kuwa ni Hidaya Mwendwa, Rahmath Thomas, Shufaa Omary, Lightnes Rajab, Glady Frank, Anaia Ally, Badra Karuta, Eunice Kilumbu, Felistecia Dioniz, Happy Johson, Fei Abdallah, Luciana Elias, Janeth Chris na Brandy Godwin.

Tolle amesema mbali ya warembo hao kupanda jukwaani kwa ajili ya kuwania taji hilo lakini kati hao warembo watano walioingia tano bora ya kumpata mrembo mwenye kipaji wa mashindano hayo (Miss Talent) nao watachuana kumpata bingwa.

Amesema katika shindano hilo la vipaji lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye ukumbi wa Club 71 Kibo Complex Tegeta, warembo tisa walipanda jukwaani kuwania nafasi ya mrembo mwenye kipaji na watano wakaingia tano bora.

Amewataja warembo watakaowania nafasi hiyo kuwa ni Hidaya Mwendwa, Rahmath Thomas, Shufaa Omary, Lightness Rajab na Glady Frank.

No comments: