Pages

Sunday, June 8, 2014

MUIGIZAJI MKONGWE NCHINI, MZEE SMALL AFARIKI DUNIA: Kuzikwa kesho saa 10 Jioni Segerea, DSM

Marehemu mzee Small Wangamba, enzi za uhai wake.
 Muigizaji mkongwe nchini, Said Ngamba almaarufu 'mzee Small Wangamba' amefariki dunia usiku wa kuamkia leo akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili akipatiwa matibabu.

Mzee Small amefariki kwa ugonjwa wa presha na kiharusi baada ya kuugua kwa muda mrefu kabla ya kuzidiwa jana na kupelekwa Muhimbili.

Mtoto wa marehemu aitwaye, Muhidin amethibitisha kifo cha baba yake (Mzee Small).

Taarifa za zaidi kutoka kwa ndugu wa marehemu zinasema kuwa, marehemu Small atazikwa kesho saa 10 jioni katika makaburi ya Segerea jijini Dar es Salaam.

Mungu  alizale  Roho  ya  Marehemu  Mahali  pema  Peponi- Amina.

No comments: