Pages

Saturday, June 21, 2014

MEYA WA ILALA, JERRY SILAA ATEMBELEA BARABARA YA TABATA ST. MARY'S YENYE MGOGORO BAINA YA MKANDARASI NA DAWASA

Mwenyekiti wa Serikali za Mitaaa Bwana Hassan Chambuso akimuongoza Mh Meya wa manispaa ya Ilala Jerry Silaa kwenda kujionea eneo la kipande cha barabara ya St. Mary's Tabata ambacho kinaleta shida baina ya Mkandarasi na Dawasa.
Mkandarasi wa barabara ya Tabata-St Mary Bwana  George Lupia wa pili kutoka kushoto akitoa ufafanuzi kwa Meya Wa Ilala Mh Jery Silaa kuhusu kukwama kwake kuendelea na Ujenzi kutokana na Mabomba ya Dawasa kupita Katikati ya barabara Hiyo.
Meya wa Ilala Mh Jery Silaa akifafanua Jambo kwa Mwenyekiti wa mitaa ya Tabata Bwana Chambuso kuhusu yeye Kulifuatilia Swala hilo kwenye mamlaka husika haraka iwezekanavyo,Pembeni yake ni Diwani wa Kata ya  Tabata St Marys Bi Mtumwa Mohamed mwenye Dira.
Mkandarasi wa Manispaaa ya Ilala Bwana Kassim Muhinda Akimwelezea Meya Jerry Silaa kwamba washaongea na Dawasa lakini hawapewi ushirikiano wa kutosha na wa haraka katika kushughulikia utoaji wa Mabomba hayo.
Source: Fullshangwe blog

No comments: