Pages

Monday, May 9, 2016

'MALKIA WA PEMBE' AFIKISHWA KORTINI TANZANIA

Yang Feng Glan, 'Malkia wa pembe' (katikati) akiwa chini ya ulinzi.


Kesi dhidi ya mwanamke mfanyabiashara raia wa China anayetuhumiwa na mashtaka ya kuendeleza mtandao wa kihalifu wa ulanguzi wa pembe barani Asia imeahirishwa kwa wiki mbili nchini Tanzania.

Mtuhumiwa amefikishwa Mahakamani leo asubuhi mjini Dar es Salaam kwa kosa la kuendeleza shughuli hiyo kwa takribani miaka 14.  Hata hivyo, mtuhumiwa huyo amekana mashtaka hayo.

Waendesha mashtaka wanasema Yang Feng Glan, anayejulikana kwa umaarufu pia kama 'Malkia wa pembe,' aliendesha biashara haramu ya kuwaua ndovu katika mbuga za wanyama ili kupata pembe zao ambazo wanazisafirisha na kuziuza katika mataifa ya bara Asia.

Mahakama imeambiwa kwamba faili ya kesi yake bado imo mikononi mwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma.

Maafisa wa serikali Tanzania walitaja kukamatwa kwa Yang Feng Glan mnamo Oktoba mwaka jana kama ufanisi mkubwa.

Taifa hilo la Afrika Mashariki limepoteza theluthi mbili za ndovu wake katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.

Chanzo: BBC Swahili

No comments: