Pages

Monday, May 9, 2016

JUMBA LA GHOROFA LAPOROMOKA MOMBASA

Jumba
Sehemu ya jumba kubwa la kibiashara mjini Mombasa imeporomoka siku chache baada ya jumba la makazi kuporomoka jijini Nairobi na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 40.

Sehemu ya jumba hilo la Nyali Centre, yenye ghorofa sita, iliporomoka usiku wa kuamkia leo.

Polisi, maafisa wa Shirika la Msalaba Mwekundu na maafisa wa Mamlaka ya Taifa ya Ujenzi (NCA) wamefika eneo hilo kufanya uchunguzi zaidi.
Chanzo: BBC Swahili

No comments: