Pages

Thursday, April 11, 2013

MDAHALO WA KITAIFA WA WANAWAKE WAFANYIKA MJINI DODOMA

Mhe. Sophia Simba akipewa maelezo na Bill Marwa kuhusiana na  tovuti rasmi iliyotengenezwa maalumu
kwa ajili ya kupaza sauti ya mwanamke (www.sautiyamwanamke.org) baada ya kuizinduwa kwenye
uzinduzi wa Mdahalo wa Kitaifa wa Wanawake unaofanyika Dodoma.  Waliosimama kushoto
kwa Waziri ni Teresa Yates na Hilda Mashauri viongozi wa mtandao wa jinsia wa asasi za kiraia
(CSO Gender Coalition) waandaaji wa mdahalo huo. Tovuti hiyo itatumika kutoa
taarifa za kila siku za mdahalo na kuendelea kupaza sauti ya mwanamke baada ya
mdahalo kwa kuandika habari mbalimbali zinazohusu mwanamke.
                           

Mwanahamisi Salim, Meneja wa Kampeni, Ushawishi na Utekelezaji wa Haki za Kiuchumi kutoka
shirika la Oxfam akiendesha zoezi la ufunguzi wa Mdahalo wa Kitaifa wa Wanawake
unaofanyika katika ukumbi wa Chimwaga Mjini Dodoma.


Teresa Yates, Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania akikabidhi zawadi kwa
Mhe. Sophia Simba (MB), Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake, Jinsia na Watoto
na kwa Dr. Rose Nchimbi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma. 


No comments: