Pages

Thursday, April 11, 2013

FILAMU YA KANUMBA 'LOVE AND POWER' KUINGIA MTAANI KESHO


Ignatio Kambarage akizungumza katika mkutano huo.  Katikati ni Myovela Mfwaisa
akifuatiwa na Mosses Mwanyilu. 


Ile filamu ya Love & Power ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa hamu na wapenzi wengi wa filamu hatimaye mwisho wa wiki hii siku ya Ijumaa tarehe 12th April 2013 itazinduliwa na kuingia sokoni rasmi na kusambazwa nchi nzima na kampuni ya mahiri ya usambazaji wa filamu ya Steps Entertainment Ltd.

Akizingumza na waandishi wa wanahabari, Mratibu wa filamu ya Love & Power Bw. Myovela Mfwaisa amesema kuwa  “Filamu ya Love & Power ni filamu ya mwisho kutengenezwa na marehemu The Great Kanumba na inatarajiwa kuingia sokoni Ijumaa tarehe 12 Aprili.”

Hivyo basi hii itakuwa fursa pekee kwa wapenzi wa tasnia ya filamu na watanzania wote kwa ujumla na kuweza kujionea kazi bora iliyotengenezwa na gwiji la filamu na balozi aliyetangaza tasnia ya filamu ya Tanzania nje ya mipaka ya Tanzania.

Akizungumzia kwa ufupi juu ya filamu ya Love & Power Bwana Myovela amesema “Filamu ya Love & Power imetengenezwa na kampuni ya Kanumba the Great film kwa kushirikiana na Steps Entertainment Ltd ikiwa imeandikwa na Ally Yakuti."

Filamu hiyo imeshirikisha wasanii nyota katika tasnia ya filamu Tanzania kama marehemu Hussein Mkiety ‘Sharomilionea,’ Irene Paul, Patcho Mwamba, Grace Mapunda, Hartman, Rammy Galis pamoja Seth Bosco ambaye ni mdogo wa marehemu na kuongozwa na marehemu Steven Kanumba. Watayarishaji wakuu ni Steps Entertainment Ltd. na imetengenezwa hapa hapa jijini Dar es Salaam katika maeneo tofauti.

No comments: