Pages

Monday, March 4, 2013

KENYA WAFANYA UCHAGUZI WA RAIS LEO

Mwananchi akipiga kura leo katika uchaguzi wa Rais nchini Kenya.  


 Watu wakiwa katika foleni ya kupiga kura katika eneo la Kibera, Nairobi.

Wananchi wakiwa katika foleni ya kupiga kura.
(Picha zote kutoka www.bbc.co.uk/swahili)

Kauli mbiu ni "PIGA KURA USIPIGE MTU, CHOMA NYAMA USICHOME NYUMBA"

SIFA ZA WAGOMBEA URAIS - KENYA
 RAILA AMOLLO ODINGA
Amezaliwa tarehe 7 Januari 1945, anagombea kupitia ushirika wa CORD. Mgombea mwenza ni Kalonzo Musyoka.  Ameahidi kusaidia kuwapatia vijana kazi na elimu zaidi.
 UHURU MUIGAI KENYATTA
Amezaliwa Octoba 1961.  Ni mtoto wa Rais wa kwanza wa Kenya, hayati Jomo Kenyatta aliyeongoza Kenya kutoka 1964 mpaka 1978.  Anagombea kupitia Jubilee Alliance, uliyoundwa kwa ushirikiano wa chama cha The National Alliance cha Kenyatta na United Republican cha William Ruto.  Katika ushirika wao, Kenyatta anasema anasimamia Kenya iliyoungana chini ya “ndoto moja ya kujenga Kenya bora”.
MOHAMUD ABDUBA DIDA
Amezaliwa mwaka 1975.  Anagombea urais kupitia Alliance for Real Change. Mgombea wake mwenza ni Joshua Odongo Onono. Ni mwanasiasa mpya, ameahidi kutilia mkazo masikini kama rais. Anasema elimu ni budi iwe bure kwa Wakenya. Alisifiwa kwa kufanya vizuri sana katika midahalo yote miwili ya urais iliyofanyika kwa mara ya kwanza Kenya katika matayarisho ya uchaguzi.
 MARTHA KARUA
Ni mgombea pekee mwanamke katika uchaguzi huu, amezaliwa Septemba 1957.  Anagombea kupitia ushirika wa National Rainbow Coalition akifuatana na mbunge wa zamani wa bunge la Afrika Mashariki, Augustine Lotodo kama mgombea mwenza. Karua ameahidi kuwakilisha Kenya iliyoungana na maswala ya mageuzi ya uchumi na ya kijamii, ikiwa ni pamoja na afya kwa wote. Anasema atatumia asilimia 10 ya bajeti ya Kenya kuboresha uzalishaji katika kilimo, kuongeza uzalishaji nishati na kuhakikisha asilimia 50 ya nyumba za Kenya zinapata huduma wa mtandao katika muda wa miaka mitano.
 PETER KENNETH
Amezaliwa Novemba 1965.  Anagombea urais kupitia chama cha Kenya National Congress, na mgombea mwenza wake ni Ronald Osumba.  Ametilia mkazo kupunguza ukosefu wa kazi na kukosekana kwa chakula.
 JAMES OLE KIYIAPI
Amezaliwa Mei 1961 huko. Mgombea mwenza ni Winnie Kaburu chini ya chama cha Restore and Build Kenya.  Ametilia mkazo wa nguvu ya swala la kuondoa ukabila katika siasa za Kenya. Anasema kipaumbele chake cha kwanza kama akichaguliwa itakuwa kutilia mkazo vijana na ukosefu wa kazi. Anasema serikali yake itaanzisha mpango wa kupata ufumbuzi wa matatizo ya ardhi kwa uangalifu na uwazi, na kuboresha uzalishaji kilimo nchini.
 WYCLIFFE MUSALIA MUDAVADI
Amezaliwa September 1960.  Anagombea chini ya chama cha United Democratic Forum Party katika ushirika wa Amani alliance.  Mgombea mwenza ni Jeremiah Kioni.  Ameahidi kuleta ukuaji wa kweli wa uchumi Kenya kwa kutilia mkazi utawala bora na kupunguza umasikini.
 PAUL KIBUGI MUITE
Amezaliwa Aprili 1945. Ni mmoja wa waanzilisha wa chama cha Safina. Anashirikiana na Shem Ochuodho kama mgombea mwenza. Ameahidi kushughulikia suala la ukosefu wa kazi na kuboresha hali ya utendaji kazi kwa kuongeza mishahara na kutekeleza sheria za kazi ambazo zitaweka kiwango cha masaa ya kazi kuwa manane pekee kwa siku. Anasema anaamini umoja wa wananchi wa Kenya, bila kujali ukabia, na atashughulika kuboresha hali ya watu wote.

No comments: