![]() |
Baadhi ya Wajumbe wa YUNA wakiwa katika picha ya pamoja katika mkutano na Wandishi wa habari uliofanyika idara ya habari Maelezo jijini Dar es Salaam. |
Baadhi ya sehemu ya waandishi wa Habari ambao wamehudhuria mkutano wa YUNA na Waandishi wa HAbari |
|
Du unaona tumemaliza una la kuongeza Mwenyekiti wa YUNA na TIMUN mara baada ya kumaliza mkutano na Wandishi wa Habari. |
Mwaka huu, mkutano wa Baraza
Kuu Kivuli La Kimataifa la Umoja wa Mataifa litafanyika Dodoma katika ukumbi wa
bunge wa Pius Msekwa kuanzia tarehe 2 hadi 6 Aprili 2013 ikiwa na mada isemayo,
“Malengo ya Maendeleo ya Kimilenia, kutazama mikakati ya maendeleo ya kijamii
na kiuchumi baada ya 2015”.
Mkutano huu utashirikisha
vijana 160 waliochaguliwa kutoka Tanzania bara na visiwani pamoja na vijana
kutoka nchi mbalimbali duniani. Lengo letu kuu ni kuhakikisha kwamba sauti ya
vijana inahusishwa katika ajenda za mashauriano ya Malengo ya Maendeleo ya
Kimilenia na kuandaa ripoti ambayo itajumuishwa katika taarifa ya taifa
itakayopelekwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Mkutano huu wa kimataifa
utakuwa majadiliano ya mwisho ya vijana kabla ya kutayarisha taarifa ya mwisho.
Asasi ya Vijana wa Umoja wa
Mataifa Tanzania inayofuraha kuwajulisha kwamba, mwaka huu Tanzania itakuwa
mwenyeji wa mkutano wa Baraza Kuu Kivuli La Kimataifa la Umoja wa Mataifa. Kwa
miaka kumi na tano, Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa imekuwa ikiandaa
mkutano wa Baraza Kuu Kivuli la Umoja wa Mataifa, ambapo washiriki hupata fursa
ya kufanya kazi kama wanadiplomasia na hushiriki katika vipindi sawa na vile
vya mashirika ya kiserikali. Washiriki hufanya utafiti kuhusu nchi fulani,
hupata majukumu kama yale ya wanadiplomasia, hufanya utafiti wa masuala ya
kimataifa, hujadili, huelimishana, hushauriana na hatimaye kupendekeza
masuluhisho ya matatizo mbalimbali ya dunia.
Asasi ya Vijana wa Umoja wa
Mataifa Tanzania inapenda kutumia fursa hii kukaribisha Watanzania wote
kuungana mkono na vijana wa Tanzania watakavyokuwa wanatoa michango na mitazamo
yao mikubwa na ya kimataifa katika suala la ajenda ya malengo ya maendeleo ya
kimilenia baada ya 2015.
Asasi ya Vijana wa Umoja wa
Mataifa Tanzania pia inachukua nafasi hii kuwaomba mashirika ya
kiserikali na yasiyo ya kiserikali kuwa kipaombele katika kuwasaidia vijana
wanaposhiriki katika nafasi hii ya pekee inayokusudia kuwaleta vijana wa
Tanzania karibu na Umoja wa Mataifa pamoja na dunia kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment