Meneja wa bia ya Safari Lager Bw Oscar Shelukindo akiwaonyesha Waandishi wa Habari Hawapo pichani tovuti maalumu kwa ajili ya programu ya Safari Wezeshwa |
Oscar Shelukindo meneja wa bia ya Safari akizunguza na waandishi wa Habari hawapo pichani |
Oscar akionyesha mtando wa programe ya Safari wezeshwa (picha zote na IPSHA MEDIA) |
Hatimaye muda wa kurejesha
fomu za progmu ya SAFARI LAGER WEZESHWA umeongezwa mpaka kufiki tarehe 15 mwezi
wa 4 kutokana na maombi ya wajasiriamali wengi ambao hawakuweza kupata fomu
hizo kwa wakati.
Akizungumza na jijini Dar
es salaam leo meneja wa bia ya Safari lager Oscar Shelukindo amesema kuwa nia
hasa ya Safari Lagel ni kuhakikisha kuwa inawawezesha wajasiriamali kutimiza
ndoto zao.
Amesema milioni 200
zimetengwa kwa ajili ya kuwasaidia wajasiriamali kwa ajili ya kuwasaidia
vitendea kazi na kuongeza kuwa kutokana na maombi yao wameamua kusogeza mbele
siku za kurudisha fona na kuwataka wachangamkie nafasi hiyo.
Naye jaji mkuu wa program hiyo
Bw Joseph Migunda kutoka taasisi Ya TAPBDS amesema
kuwa sifa za kushiriki program hiyo ni sawa na mwaka jana na kuongeza kuwa
washiriki wana takiwa kuwa na sifa kuu nne ikiwemo wawe wachapakazi, biashara
zao ziwe halali, wawe na umri kati ya miaka 18 mpaka 40 na wawe na nia za
kukuza biashara zao.
No comments:
Post a Comment