Pages

Thursday, February 28, 2013

BODI YA TASAF YAZINDULIWA RASMI

 Bw. Ladislaus Mwamanga, Mkurugenzi wa TASAF, akizungumza na wajumbe
wa bodi (hawapo katika picha).

 Kaimu Mwenyekiti wa bodi ya TASAF, Abbas Kandoro akiwa pamoja
 na Bw. Ladislaus Mwamanga, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF.

  Wajumbe wa bodi ya TASAF wakiwa katika picha ya pamoja.
Picha zote na Julius Ngahyoma 

(Shabani Tolle)
Serikali imesema kuwa kasi ya kupungua kwa umasikini nchini bado ni ndogo na kwamba takwimu ya awamu ya pili ya MKUKUTA inaonyesha kuwa umasikini umepungua kwa asilimia mbili tu, jambo ambalo ni hatari kwa maendeleo ya taifa na jamii kiujumla.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-ikulu Bwana Peter Ilomo amezungumza  na wajumbe wa bodi ya mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF) ambayo imeteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe dakta Jakaya Mrisho Kikwete, amesema ni lazima bodi hiyo ifanye kazi kwa uadilifu mkubwa ili kuhakikisha kwamba changamoto za umasikini zinapungua kwa kusimamia ipasavyo miradi ya mfuko huo (TASAF) hususani katika maeneo ya vijijini ambako hali ya umasiki imekithiri.

Naye kaimu mwenyekiti wa bodi hiyo Alhaji Abbasi Kandoro amesema kuwa ili kufanikisha dhamana kubwa ambayo wamepewa na serikali ya kushughulikia matatizo ya wananchi, ushirikiano wa karibu kati yao na serikali unahitajika na wanatambua kuwa wana kazi kubwa ya kufanya, hasa katika utekelezaji wa mpango wa awamu ya tatu wa TASAF.

Bwana Ladislaus Mwamanga ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa mfuko huo amebainisha kuwa utekelezaji wa awamu ya tatu umeshaanza na tayari watendaji mbalimbali wameshaanza mafunzo ya utekelezaji wa mpango huo kwa vitendo.  Amesema mafunzo hayo yanafanyika katika vijiji 20 vilivyopo katika wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani na kwamba baadae utekelezaji wa mpango huo utafanyika kwa awamu katika halmashauri zote nchini.

No comments: