Papa Benedict XVI, mwenye nguo nyeupe.
Papa Benedict wa 16 ambaye ndio kiongozi mkuu wa kanisa la Katoliki Duniani anajiuzulu rasmi leo. Akizungumza katika misa yake maalumu aliyoifanya jana katika makao makuu ya kanisa hilo lililopo Vatican nchini Italia, Papa amesema kuwa ameamua kujiuzulu kutokana na maombi aliyoyafanya kwa Mwenyezi Mungu.
Papa Benedict ameliongoza kanisa hilo kwa muda wa miaka 8 toka achaguliwe rasmi ambapo amewaambia maelfu ya watu waliokusanyika katika viwanja vya Mtakatifu Petro huko Vatican kuwa anafahamu uzito wa maamuzi yake lakini anafarijika kutokana na imani yake kwa Mungu na kanisa hilo.
Aidha Papa akizungumza katika misa hiyo amesema kuwa alihisi kupotewa na nguvu katika miezi ya karibuni na kumuomba Mungu kumsaidia katika kufanya uamuzi huo.
“Nawaachieni Baraka zangu “ hayo ni baadhi ya maneno ya mwisho ambayo ameyaongea Papa huyo katika misa hiyo ambayo ilihudhuriwa na idadi kubwa ya waumini wa kanisa hilo lililopo Vatican.
No comments:
Post a Comment