Na.Catherine Sungura,WAF-DSM
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi amefanya ziara ya kushtukiza
Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) na kukagua mashine za MRI na
CT Scan na kubaini zimeharibika.
Hata
hivyo, uongozi licha ya kujua hali hiyo haukuwasilisha taarifa rasmi
kwa Wizara hiyo, kutokana na hali hiyo Prof. Makubi ameagiza ndani ya
siku 14 kuanzia sasa wahakikishe mashine hizo zilizonunuliwa kwa gharama
kubwa na Serikali, zitengenezwe na kuanza kutoa huduma.
Prof.
Makubi ameziagiza hospitali za Rufaa za Mikoa, Kanda na Taifa kuwa na
mpango mbadala (Plan B) kuhakikisha wagonjwa wanaendelea kupata matibabu
bila usumbufu pale mashine za Taasisi zao zinapoharibika.
"Kwa
mfano hapa MOI (Plan B) yenu ni Muhimbili, wagonjwa ambao wanahitaji CT
Scan na MRI wapate huduma bila kupata usumbufu na rafiki" ameagiza.
Aidha,
ameziagiza ziwe na 'plan B' kwa vipimo vyote vya radiolojia na vipimo
vya damu endapo itatokea changamoto wagonjwa waendelee kupata huduma.
Ameelekeza
pia hospitali zote za Taifa, Kanda, Mikoa na maalum zenye mashine za
kisasa kuhakikisha zinatenga asilimia kadhaa ya fedha kwa ajili ya
matengenezo yake kutoka kwenye makusanyo ya ndani
Hata
hivyo ameelekeza tena hospitali zote hizo kukaa na TANESCO na kufanya
tathmini ya mifumo ya umeme lakini pia ziweke 'backup' ya nishati
mbadala ili mifumo hiyo isiharibike pale inapotokea kukatika kwa umeme.
Vilevile
amewlekeza pia kutengwa bajeti mahususi ya matengenezo na kutoa miezi
mitatu (3) kuwa na mkataba wa matengenezo kwa mashine zote pamoja na
vifaa vya maabara kwa hospitali zote za Rufaa za Mikoa,Kanda,Maalumu ma
Taifa ili kuhakikisha zinafanyiwa matengenezo na ukarabati kwa wakati
No comments:
Post a Comment