Pages

Wednesday, February 21, 2018

JESHI LA POLISI KENYA LAMNASA MTANZANIA NA DHAHABU YA TSHS BILIONI 2.4


KENYA. Jeshi la Polisi nchini Kenya linamshikilia mwanaume wa miaka 48 anayesemekana kuwa Mtanzania ambaye ameshikwa akiwa anataka kusafirisha dhahabu kinyume na sheria.

Mwanaume huyo amekamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta akitaka kusafirisha dhahabu ya gharama ya Dola za Marekani Milioni 1 sawa na Tsh Bilioni 2.4 za Kitanzania.

Jina la mwanaume huyo bado halijawekwa wazi lakini inaelezwa kuwa anadaiwa kuwasili kutoka Mwanza, Tanzania kupitia Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro na alikuwa safarini kuelekea nchini Dubai.

No comments: