Pages

Wednesday, February 21, 2018

DIWANI WA CHADEMA ALIYEWEKWA NDANI NA MEYA WA CHADEMA KAHAMIA CCM


Diwani wa kata ya Daraja Mbili Arusha, Prosper Msofe katika jimbo la Arusha Mjini amejiuzulu nafasi yake na kuhamia CCM kwa madai ya kumuunga mkono Rais Magufuli.

Pamoja na mambo mengine Prosper Msofe amesema CHADEMA kimekuwa chama kinachoongozwa na Mbunge Lema katika mkoa wa Arusha na amedai kuwa Meya amekuwa akikataa kuambiwa ukweli.

Mkurugenzi wa jiji la Arusha, Athumani Kihamia amekiri kupokea barua hiyo pamoja na barua za madiwani wengine wa CHADEMA kujiuzulu nafasi zao hizo kwa madai wa kuhamia CCM.

No comments: