Pages

Wednesday, December 20, 2017

JB: KANUMBA ALIPOANZA KUFANYA VIZURI, MSHUMAA UKAZIMA

Msanii wa Bongo Movie, Jackob Steven a.k.a. JB.

MKALI wa Bongo Movie Tanzania Jocob Steven maarufu kama JB amesema kwamba marehemu Kanumba alikuwa mzuri katika kuigiza ‘Movie’  ila bado kuna watu wanafanya vizuri zaidi ya pale alipopaacha.

JB amesema hayo leo mchana kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio, kwamba kuifanya akili ya binadamu kusahau kitu alichokiacha msanii aliyekuwa juu sio kazi rahisi.

Marehemu Steven Kanumba, enzi za uhai wake.

Msanii huyo ametoa mfano wa aliyekuwa mkali wa Filamu za mapigano na Karate duniani Bluce Lee, ambaye alifariki wakati yupo katika kiwango cha hali ya juu, leo ukimueleza mtu kwamba Jackie Chan anafanya vizuri zaidi yake atakataa.

”Kanumba alifanya vizuri kwa muda mchache sana kisha Mungu akamchukua, wakati anafanya vizuri ndio hapo hapo mshumaa ukazima, sio rahisi kumuaminisha mtu kwa kiwango alichofanya Kanumba na alipoishia kuweza kufananisha na sasa kwakuwa alifanya vizuri zaidi ila bado waliopo wanafanya vizuri,” amesema JB.

JB ameongeza kuwa Kanumba alikifikisha Kiwanda cha Filamu pazuri kwa kiwango chake, ila kila ‘Industry’ kuna wakati inapanda wakati mwingine inashuka na anaamini sasa wunarudi vizuri.

No comments: