![]() | ||
Afisa
Mtendaji Mkuu wa benki ya TPB Sabasaba Moshingi (kulia) pamoja na
Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande (kushoto)
wakibadilishana nyaraka za makubaliano mara baada ya kusaini.![]() Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya TPB Sabasaba Moshingi (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande (kushoto) wakisaini makubaliano ya ushirikiano, ambapo kwa sasa wafanyakazi umma, wateja na hata wale wasio wateja wanaweza kupata ving’amuzi vya DStv kwa mkopo na kisha kulipia kidogo kidogo. Nyuma yao ni mashahidi kutoka pambe zote mbili. |
BENKI ya TPB imeingia kwenye makubaliano rasmi na kampuni
ya Multichoice Tanzania inayotoa huduma za DStv ambapo wafanyakazi umma,
wateja na hata wale wasio wateja sasa wanaweza kupata ving’amuzi vya
DStv kwa mkopo na kisha kulipia kidogo kidogo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Bw. Sabasaba Moshingi alisema kwa sasa Watanzania wanaotaka kumiliki ving’amuzi vya DStv, wataweza kupata mkopo maalum kutoka TPB utakaowawezesha kufungiwa huduma za DStv na kisha kulipa kwa awamu kwa kati ya miezi mitatu hadi mwaka mmoja.
Alisema kuwa benki yake siku zote imekuwa ikijitahidi kubuni huduma mbalimbali kwa ajili ya kuwawezesha Watanzania wengi zaidi kupata huduma muhimu na pia katika kuboresha hali zao kiuchumi na kijamii.


No comments:
Post a Comment