Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,
Paul Makonda (wa pili kulia), akinena jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa
Clouds Media Group, Joseph Kusaga (kushoto).
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Paul Makonda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama
Mkoa wa Dar es Salaam mapema leo ametembelea Ofisi za Clouds Media Group
kutoa pole ikiwa ni siku moja baada ya ofisi hizo kukumbwa na janga la
moto uliotokea hapo jana majira ya saa nne asubuhi.
Makonda akiongea na maofisa wa vikosi vya usalama.
Viongozi wengine wa serikali
waliofika ofisini hapo ni Mkuu wa Wilaya wa Kinondoni, Ally Hapi na Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta.
Hata hivyo, tayari matangazo
ya vituo vya Clouds FM na Clouds TV yamerejea hewani baada ya kupotea
siku nzima jana kutokana na hitilafu ya iliyosababishwa na moto huo
ambao chanzo chake hadi sasa hakijajulikana.


No comments:
Post a Comment