Pages

Wednesday, November 1, 2017

LISSU AMPONGEZA NYALANDU, AZUNGUMZIA UCHAGUZI WA MADIWANI

DAR ES SALAAM.  Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amempongeza aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki (CCM), Lazaro Nyalandu kwa kupata ujasiri wa kuchukua hatua kubwa ambayo hata wabunge wengi waliopo ndani ya CCM wanashindwa kuichukua.

Lissu ambaye yuko kwenye matibabu jijini Nairobi amempongeza Nyalandu kwa kuwa alikuwa Mbunge jirani yake na kuwa ujasiri wa kufanya hivyo.

Mbali na kumpongeza Nyalandu pia Lissu amezungumzia uchaguzi wa madiwai katika kata 43 akieleza kuwa kuwapa CCM kura katika kata hizo ni sawa na kukubaliana na yanayoendelea nchini.

"Kuwapa CCM kura sasa hivi ni sawa na kuwapa CCM mamlaka ya kutapanya mali zetu kama wanavyotaka," amesema Lissu jana Jumanne akiwa jijini Nairobi.

Msikilize Mhe Lissu hapa chini akiongea kuhusiana na suala hilo:

No comments: