Msanii Nasib Abdul maarufu Diamond Platinumz, amedai mahakamani kuwa hana uwezo wa kumlipa mwanamitindo Hamisa Mobeto, Sh milioni tano kama gharama za matunzo ya mtoto kwa mwezi.
Diamond amewasilisha majibu hayo katika Mahakama ya Watoto Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Devotha Kisoka baada ya Mobeto kumfungulia kesi ya madai katika Mahakama hiyo ya watoto akidai mambo mbalimbali ikiwamo matunzo ya mtoto.
Mobeto katika maombi yake kupitia mawakili wake Abdullah Lyana wa Walter Godluck wa kampuni ya Uwakili ya Century Attorney, anaiomba Mahakama imwamuru Diamond kutoa matunzo ya mtoto kila mwezi, mtoto huyo wa kiume aliyezaa na msanii huyo na kumuomba msamaha kwa umma kwa kumsababishia madhara yaliyoishtua familia yake.
Baada ya kupokea majibu hayo Mahakama iliahirisha kesi hiyo ya madai hadi Novemba 8, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Mobeto kupitia wakili wake walimpa notisi Diamond ya kutaka amwombe radhi na kupeleka matunzo ya mtoto ndani ya siku saba lakini notisi hiyo haikutekelezeka hivyo aliamua kulifikisha suala hilo mahakamani.

No comments:
Post a Comment