Pages

Thursday, May 25, 2017

SERIKALI YANUSURU MAISHA YA MZEE NGOSHA


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema kuwa serikali itamhamisha Mzee Francis Ngosha kwenye makazi mapya kwenye kambi ya wazee wasiojiweza ya Nunge iliyopo Kigamboni jinini Dar es Salaam, huku hatua nyingine za kimatibabu zikiendelea.

Dkt. Kigwangalla ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati alipomtembelea mzee huyo katika hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam alipopelekwa na uongozi wa serikali ya mtaa, Buguruni.

Waziri Kigwangalla amesema mzee huyo hivi sasa atahamishwa kutoka hospitali hiyo na kupelekwa hospitali ya taifa, Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa afya yake.

Mzee Ngosha ndiye aliyebuni nembo ya taifa mwaka 1957 ambayo ina bibi na bwana, inayotumika na serikali katika shughuli rasmi ikiwemo bendera ya taifa.

Taarifa ya ugonjwa wa mzee Ngosha ziliripotiwa kwa mara ya kwanza na kituo cha runinga cha ITV kweney taarifa yake ya habari ya juzi saa mbili usiku.
Chanzo: Nipashe

No comments: