Pages

Monday, January 30, 2017

TRENI YA DELUXE YAPATA AJALI, HAKUNA VIFO VILIVYORIPOTIWA

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) unatoa taarifa kuwa leo  Januari 29, 2017 mnamo  saa 9:40 alasiri treni ya abiria ya Deluxe ilipokuwa ikirejea Dar es Salaam kutoka Kigoma imepata matatizo kati ya vituo vya Ruvu na Ngeta ambapo mabehewa 9 yamepata ajali. Kati ya hayo manne yameanguka, mawili yametenguka na matatu yameacha njia.

Imeripotiwa watu kadhaa wamepata majeraha mepesi isipokuwa mmoja ndiye aliyepata majeraha makubwa ambaye amekimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi.

Hizi ni taarifa za awali baada ya Kikosi cha uokoaji kikimaliza kazi ya kuinua mabehewa ndio taarifa ya kamili ya ajali itakamilika.

Wakati taarifa hii ikipatikana Waziri wa  Ujenzi na Uchukuzi  Profesa Makame Mbarawa, Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Nd Masanja Kungu Kadogosa na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Mhandisi S. Chillery wako  katika eneo la ajali. 

Halikadhalika taarifa imefafanua kuwa sehemu ya treni ya Deluxe yenye mabehewa kumi na abiria wake iko njiani kuja Dar es Salaam na inatarajiwa kuwasili saa 2 usiku.

Aidha uongozi wa TRL umeuhakikishia umma na wateja wake kuwa njia ya reli kati ya Ruvu na Dar es Salaam itafunguliwa ndani ya saa 24 ili shughuli za usafirishaji  zirejee kama kawaida. 

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano.

Kny: Mkurugenzi Mtendaji wa TRL 
        Ndugu Masanja Kungu Kadogosa
        Januari 29, 2017
        DAR ES SALAAM 
Baadhi ya Mabehewa ya treni ya Delux ikitokea Kigoma kwenda  jijini Dar es Salaam  yakiwa yameanguka eneo la Ruvu mkoani Pwani jioni hii ya Januari 29, 2017. 
Baadhi ya Mabewa mengine yakiwa yameacha njia

No comments: