Mke wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu wa madini jijini Arusha marehemu bilionea Erasto Msuya, bibi Miriam Msuya (katikati) akiingia katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana. |
MIRIAM Stephen Mrita maarufu kama Miriam Elisaria Msuya (41) ambaye ni mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam akikabiliwa na mashitaka ya mauaji ya dada wa marehemu bilionea huyo, Anath Elisaria Msuya.
Miriam ambaye ni mkazi wa Sakina kwa Iddi jijini Arusha, alisomewa jana mashitaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Magreth Bankika.
Wakili wa Serikali, Diana Lukondo alidai kuwa Mei 25 mwaka huu katika eneo la Kibada, wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam, mshitakiwa alimuua kwa makusudi bi Anath Msuya.
Kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji, mshitakiwa hakutakiwa kujibu chochote hadi upelelezi utakapokamilika na kesi hiyo itahamishiwa Mahakama Kuu Tanzania, kanda ya Dar es Salaam.
Lukondo alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba Mahakama kupanga tarehe nyingine ya kutajwa.
Hakimu alimuru mshitakiwa apelekwe mahabusu hadi Septemba 6 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
Miriam alikamatwa Agosti 4 mwaka huu jijini Arusha kabla ya kupandishwa mahakamani jana kwa tuhuma za mauaji ya dada wa aliyekuwa mmewe, marehemu Erasto Msuya.
Anath, ambaye ni dada wa marehemu bilionea Erasto Msuya, aliuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake Kibada, Kigamboni jijini Dar es Salaam usiku wa Mei 25 mwaka huu
Miriam ambaye ni mkazi wa Sakina kwa Iddi jijini Arusha, alisomewa jana mashitaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Magreth Bankika.
Wakili wa Serikali, Diana Lukondo alidai kuwa Mei 25 mwaka huu katika eneo la Kibada, wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam, mshitakiwa alimuua kwa makusudi bi Anath Msuya.
Kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji, mshitakiwa hakutakiwa kujibu chochote hadi upelelezi utakapokamilika na kesi hiyo itahamishiwa Mahakama Kuu Tanzania, kanda ya Dar es Salaam.
Lukondo alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba Mahakama kupanga tarehe nyingine ya kutajwa.
Hakimu alimuru mshitakiwa apelekwe mahabusu hadi Septemba 6 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
Miriam alikamatwa Agosti 4 mwaka huu jijini Arusha kabla ya kupandishwa mahakamani jana kwa tuhuma za mauaji ya dada wa aliyekuwa mmewe, marehemu Erasto Msuya.
Marehemu Anath Msuya, dada wa marehemu bilionea Erasto Msuya, enzi za uhai wake. |
Chanzo: Nipashe
No comments:
Post a Comment