PWANI. Mapigano makali yanaendelea kati ya Polisi na watu wanaosadikiwa kuwa ni magaidi ambao wapo katika nyumba moja maeneo ya Vikindu wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
Watu hao wanashukiwa kuhusika na tukio la juzi la uporaji wa silaha aina ya SMG kwa Polisi katika eneo la benki ya CRDB tawi la Mmbande ambapo polisi watatu waliuawa katika tukio hilo.
Hadi sasa bado Polisi wameizingira nyumba hiyo na inasemekana polisi mmoja ambaye alikuwa kiongozi wa kikosi cha kupambana na majambazi ambaye hivi karibuni alihamishiwa Dar es Salaam kutokea Manyara, Afande Njiku, ameuawa kwa kupigwa risasi ya kichwa katika mpambano huo.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu, Simon Sirro na wasaidizi wake wote wapo huko katika eneo la tukio.
Wakati huo huo, njia za magari yanayokwenda maeneo ya Vianzi, Mkuranga, Malela, Pemba Mnazi na Mfuru zimefungwa kutokana na mapambano hayo.

Tutawaletea taarifa zaidi baadae............
Chanzo: Radio One&Clouds FM
No comments:
Post a Comment