Pages

Wednesday, July 27, 2016

MTU MMOJA AFARIKI KATIKA AJALI YA KICHWA TRENI KUGONGANA NA BASI LA UDA JANA USIKU

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjPDh-Rz79UQ8EF2T-RAf0p4h57dJcWt707v-pEqV0vVGPpgx2q9ezhivcxKfMmqJDq3C2FF03Di3MaLmyImiFI_H0zhLs0YkaGnZEd6vqhl64WLnNgfGddCQEVEZIQO-sFe2NPLdWHfyE/s1600/New+Picture+%25282%2529.png
Mtu mmoja afariki dunia baada ya basi la UDA kukigonga kichwa cha treni cha Kampuni ya Reli Tanzania(TRL) katika makutano ya reli na barabara ya Kamata saa 3:20 usiku jana Julai 26, 2016. Marehemu ametambuliwa kwa jina la Omari Abdallah Nyumba mkazi wa Mbagala.

Aidha majeruhi 43 wa ajali hiyo walipelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo watatu kati yao ni mahututi.

Taarifa za awali za Kikosi cha Polisi Reli zinaeleza kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya dereva Majuto Hamis wa basi hilo la UDA aina ya Heicher lenye namba za usajili T969 CVP kukaidi amri ya kusimama iliotolewa na mfanyakazi wa TRL. Dereva huyo ni mmoja wa majeruhi ambaye amevunjika miguu na yuko chini ya ulinzi wa Polisi wa Reli akiwa wodini baada ya majeruhi wote kupatiwa huduma.

Kichwa cha treni kilichogongwa ni cha kazi za sogeza Namba 7317 kilikuwa kikitokea kituo kikuu cha treni cha Dar es Salaam.

Kikosi cha Polisi TRL wameahidi kutoa taarifa zaidi baadae hii leo kuhusu maendeleo ya majeruhi wa ajali hiyo.

Tokea uanze mwaka huu kumekuwepo na ukiukwaji mkubwa wa sheria za barabarani kwa watumiaji wa vyombo vya moto hasa madereva wa pikipiki za bodaboda kutokuwa makini katika kuzitii sheria hizo zinazosimamia makutano ya reli na barabara.

Tokea kuanza kwa mwaka huu wa 2016 ajali nyingi zimeripotiwa hapa jijini Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Manyoni mkoani Singida zikihusisha vyombo hivyo.

Wito unatolewa na Uongozi wa TRL kwa watumiaji wa vyombo vya moto, boda boda, magari mkubwa na mabasi na wananchi kwa jumla kuzingatia sheria ili kuepuka madhara makubwa ikiwemo kupoteza maisha, kupata ulemavu wa kudumu na pia upotevu wa rasilimali muhimu ambazo kama zikitumiwa vizuri zitaboresha maisha ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano:
Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL 
Ndugu Masanja Kungu Kadogosa
Julai 27, 2016.
DAR ES SALAAM.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgt2O7VwHvb8Y38hVuDmHbNQ1SARp-zYO2F_IZ7iN8E2yHkCrkU6PF9bbf9sDyuKfO_v0bciaR5gdeEa-h4GMWXM1A4b4DAT3eFYx0JhFPDEgUp0vA3Cij1gS8kTRezY2bLTPL_CR4v7_k/s1600/13679913_10208776905012998_7100227019259395107_o.jpg
Muonekano wa basi hilo baada ya kugonga treni.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgzF-fdLgR8iaez6sqqmesVSM9ZDDgsCS4fhI-3WmLwFVPn5TQDc-1qcuJZ9FfVnzGxTsSG-LHUwvqoPrg0Q-xsX_YD5MHI31Tu7Jchg7gvWjzugHa3ONwxPb-W4S6orf78HhZg5RUVq3s/s1600/13735599_10208776906933046_8958278858931461078_o.jpg

No comments: