Koffi Olomide. |
Baada ya kuwasiliana na maripota wa jijini Kinshasa ili kupata undani wa yanayomsibu mwanamuziki nguli wa Congo, Koffi Olomide 'Mopao' kufuatia tetesi za kutiwa mbaroni kwa kosa la kumshambulia mnenguaji wa bendi yake ya Quarter Latin aitwaye Pamela katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi, Kenya, imegundulika kuwa SIO KWELI kuwa Koffi Olomide tayari ameshahukumiwa kwenda jela miaka 18, bali UKWELI ni kwamba amepelekwa jela kwa siku tano kabla ya kufika tena mahakamani kujibu shitaka la kujeruhi kwa kukusudia (intentional injury) na kufanya fujo hadharani.
Koffi alikamatwa jana Jumanne asubuhi nyumbani kwake Kinshasa na kupelekwa mahakamani ambako amri ya kumweka jela kwa siku tano ilitolewa.
Shitaka kuu analokabiliwa nalo Mopao ni kumuumiza dansa wake wa kike na kufanya fujo hadharani.
Video zifuatazo zinaonesha Mopao alipokuwa akitolewa mahakamani na kupelekwa gereza kuu la Makala. Video ya chini ni wakili wake akieleza mambo yalivyo. Wanaojua Kifaransa kazi kwenu...

Chanzo: Michuzi Blog
No comments:
Post a Comment