| Modesta Joseph (kulia) mwananfunzi wa shule ya sekondari Kisutu ya DSM akipeana mkono wa pongezi na hati ya fedha na John Mngodo, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia baada ya kushinda tuzo ya ubunifu wa TEHAMA wa kuwawezesha wanafunzi kuwasilisha kero zao za usafiri kutumia TEHAMA kwa Taasisi ya EWURA. |
| Mgimba Faustine (kulia) akipokea tuzo ya fedha taslimu kutoka kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia baada ya kushinda Tuzo ya Wabunifu wa TEHAMA ya kuwawezesha wateja kutumia simu ya mkononi kubaini bidhaa feki. Anayeshuhudia katikati ni Naibu Balozi wa Finland nchini Tanzania Simo-Pekka Parviainen na wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Dkt. Hassan Mshinda. |
| Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia akimpatia Japhet Sekenya tuzo ya wabunifu wa TEHAMA kwa kutengeneza mtindi kwa kutumia karanga na unaoweza kutibu magonjwa mbali mbali ya binadamu kama vile vidonda vya tumbo, kuzuia saratani. Wa tatu kulia ni Naibu Balozi wa Finland nchini Tanzania Simo-Pekka Parviainen akishuhudia tukio hilo pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH (Wa pili kulia), Dkt. Hassan Mshinda. |
No comments:
Post a Comment