![]() |
| Kamishina wa Polisi, ACP Suleiman Kova. |
Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kukamata bunduki 14 na risasi 28 zilizoporwa katika kituo cha polisi cha Stakshari.
Sambamba na silaha hizo ambazo ni bunduki za SMG 7, bunduki za SAR 7 zote zikiwa zimeibiwa Stakshari, jeshi hilo pia limekamata bunduki ya kichina aina ya Norinko na sanduku la chuma lililosheheni fedha za kitanzania milioni 170.
Kamishina wa Polisi, ACP Suleiman Kova amesema pamoja na kukamata silaha hizo, jeshi hilo linawashikilia watu wawili kati ya watano waliokamatwa wakijiandaa kufanya uhalifu eneo la Toangoma jijini Dar es Salaam.
Kova alisema watu watatu kati yao walifariki dunia baada ya kupambana na Polisi waliokuwa wakitaka kuwaweka nguvuni baada ya kubaini mpango wao wa kufanya uhalifu.

No comments:
Post a Comment