![]() |
| Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akipokea kadi za Wanachama wa vyama mbalimbali vya upinzani na kujiunga na CCM,jioni hii katika viwanja vya mji mdogo wa Muganza,wilayani Chato Mkoani Geita, Mh Magufuli amezoa wanachama wapya waliorudisha kadi zao wapatao zaidi ya 150. |
![]() |
| Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akipokea kadi za Wanachama wa vyama mbalimbali vya upinzani na kujiunga na CCM, jioni hii katika viwanja vya mji mdogo wa Muganza, wilayani Chato Mkoani Geita,Mh Magufuli amezoa wanachama wapya waliorudisha kadi zao wapatao zaidi ya 150. Mh Magufuli yuko jimboni kwake Wilayani Chato kuwaaga na kuwashukuru Wananchi wake kwa kumpa ridhaa ya kuwaongoza kwa miaka 20 akiwa Mbunge. |
![]() |
| Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Ndugu Rajab Luhwavi akiwasalimia wanachama wa CCM pamoja na Wananchi waliofika kumlaki Dkt. Magufuli jioni ya leo katika viwanja vya mji mdogo wa Muganza wilayani Chato mkoa wa Geita. |
![]() |
| Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono pia na kuwashukuru Wananchi wake kwa kumpa ridhaa ya kuwaongoza kwa miaka 20 akiwa Mbunge wao. |
![]() |
| Baadhi ya Wananchi wa mji mdogo wa Muganza,Wilayani Chato na vitongoji vyake waliokuwa wamekusanyika kwenye viwanja vya mji mdogo wa Muganza jioni ya leo wakishangilia kwa furaha kubwa mara baada ya Mbunge wao na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM, Dkt John Pombe Magufuli kujitambulisha kwao. |
![]() |
| Mmoja wa Wafuasi wa chama cha Chadema Jumanne Majani akionekana kuwa na furaha ya kupitiliza mara baada kupewa ruhusa ya kusalimiana na Dkt. Magufuli, katika kijiji cha Kibehe alipokuwa akielekea Mji Mdogo wa Muganza kuwasalimia na kuwashukuru wananchi wa mji huo. |
![]() |
| Mmoja wa Wafuasi wa CCM akishangilia mara baada ya kumuona Dkt. Magufuli alipokuwa akipita kuwasalimia wananchi akielekea mji mdogo wa Muganza, wilayani Chato. |







No comments:
Post a Comment