Pages

Sunday, July 12, 2015

MAGUFULI AIBUKA KIDEDEA KINYANG'ANYIRO CHA URAIS CCM

Dk John Pombe Joseph Magufuli, Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM.

Chama tawala nchini, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemtangaza rasmi Dk John Pombe Magufuli kuwa mgombea wake wa kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu wa ujao.

Dk John Magufuli, ameshinda kwa kura 2104 ambazo ni sawa na asilimia 87.1 ya kura zote zilizopigwa.

Balozi Mhe. Amina Salum Ali ameshika nafasi ya pili kwa kupata kura 253 ambazo ni sawa na asilimia 10.5 wakati Dk Asha-Rose Mtengeti Migiro amepata kura 59 ambazo ni sawa na asilimia 2.4.

Kufuatia ushindi huo Dk Magufuli ndiye atakaye kuwa mgombea urais wa chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa CCM Dk Jakaya Mrisho Kikwete katika mkutano huo alimtaja Dk Ali Mohamed Shein kuwa Mgombea urais kwa upande wa Visiwani (Zanzibar).

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjpTjGf0Nk-UIBj_qZWTphN8il-KfbWK_PoiwpKjMvx2ILez7e63OVn8XmekE1KkBUBot4qHQ8AqX9eYlPjE9Q1Q5R2e7GETVlvUWGngoR2JXWddmb-iMrY0-ynwr6NEMuQ2RpZoQk6OY4q/s1600/MMGL9670+copy.jpg
Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (kushoto) akimtangaza mgombea urais wa mwaka huu kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli.

No comments: