| Marehemu Ramadhani Masanja (Banza Stone) enzi za uhai wake. |
Na I.A.Mwaipaja
MWANAMUZIKI mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Ramadhani Masanja almaarufu kama Banza Stone amefariki dunia leo mchana nyumbani kwao Sinza Kijiweni baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Kupitia redio ya Clouds FM, Shabani Ally Masanja ambae ni kaka wa Banza amethibitisha kutokea kifo hicho na kwamba msiba upo hapo nyumbani kwao Sinza, njia panda ya Lion Hotel.

Shabani amesema kuwa taratibu za mazishi bado zinafanywa hapo nyumbani na kwamba marehemu anaweza kuzikwa kesho; muda kamili utafahamika baadae baada ya majadiliano ya wanafamilia.
Banza Stone aliyezaliwa mwaka 1972 na kufanikiwa kumaliza elimu ya msingi katika shule ya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam mwaka 1987, alianza taratibu kujihusisha na masuala ya muziki akiwa angali mdogo.

Banza alianza muziki miaka 25 iliyopita, mara tu baada ya kumaliza elimu yake ya msingi kwa kujihusisha na muziki wa Hip Hop, enzi hizo walikuwa wakisikiliza katika redio. Wakati huo alikuwa na wenzake kama kina K One na Scoz Man.
Mwaka 1990 Banza aliamua kuwa mcheza dansi ambapo alicheza dansi kwenye maharusi na baadae alikwenda shule kusomea masuala ya muziki kwenye chuo cha utamaduni cha Korea (Korea Cultural Music Centre) mwaka 1990 mpaka 1991.
Baada ya kuhitimu cheti alianza kuimba katika bendi mbalimbali zikiwemo The Heart Strings, Twiga Band, Achigo Band, Afri-Swez na bendi nyingine ndogo ndogo. Ameuwa akikaa muda mfupi kwenye bendi hizo hadi alipohamia katika bendi ya African Stars (Twanga Pepeta) ambako alidumu kwa muda mrefu.
Alijiunga na chuo cha Sanaa Bagamoyo mwaka 2000 ambapo alipata mafunzo kwa miaka miwili, alipomaliza alitoka Twanga Pepeta na kwenda bendi ya Tanzania One Theatre (TOT) na huko alijulikana zaidi kwa jina la Mwalimu wa Walimu. Huko nako hakukaa sana na kuamua kuanzisha bendi yake iliyokuwa ikiitwa Bambino Sound ambayo ilidumu kwa miezi kadhaa tu.

Baadaye Banza Stone alirudi tena African Stars Band ambako alikaa kwa muda mfupi na kuhamia bendi ya Extra Bongo.
Mwaka 2013 msanii wa muziki wa kizazi kipya, Hamisi Ramadhani almaarufu kama H-Baba alimshirikisha Banza kurekodi wimbo wake mpya wa "Sina Raha."
Banza Stone amewahi kutamba na nyimbo kadhaa zikiwemo: Mtaji wa Maskini, Kumekucha, Elimu ya Mjinga, Angurumapo Simba na Falsafa ya Maisha. Amewahi pia kuimba vibao kadhaa vya taarabu ukiwamo Kuzaliwa Mjini na ule wa Play Boy.

Marehemu Banza Stone amekuwa akiripotiwa mara kadhaa kukabiliwa na ugonjwa wa kifua na fangasi ya kichwa ambao ameendelea kuwa nao hadi mauti ilipomfika leo mchana.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Banza Stone. Amina.
Chanzo: Clouds Radio & Jamii Forums
No comments:
Post a Comment