Pages

Tuesday, August 12, 2014

TOP LAND MABINGWA WA SAFARI POOL KINONDONI

Katibu Mkuu wa Chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga akimkabidhi Nahodha wa timu ya Top Land kitita cha fedha taslimu Shilingi 800,000/ = mara baada ya kuibuka mabingwa wa mashindano ya Safari Pool 2014 kwa Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Wachezaji wa timu ya Top Land wakishangilia kwa kucheza na kitita cha Shilingi 800,000/= mara baada ya kuibuka mabingwa wa mashindano ya Safari Pool 2014 kwa Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
MABINGWA watetezi klabu ya mchezo wa Pool ya Top Land ya mkoa wa kimichezo wa Kinondoni jijini Dar es Salaam imefanikiwa kutetea ubingwa wake katika fainali za mashindano ya mchezo huo yajulikanayo kama “Safari National Pool Competition 2014” kwa kuwafunga timu ya klabu ya Meeda kwa mabao 13 - 5, yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mkoani humo na kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 800,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa wa kimichezo wa Kinondoni kwenye fainali za kitaifa zinazotarajiwa kufanyika Mkoani Kilimanjaro.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na Meeda Pool Klabu na kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi 400,000/= na nafasi ya tatu ni Jaba Pool Klabu ambao walijinyakulia fedha taslimu Shilingi 250,000/= na nafasi ya nne ilichukuliwa na klabu ya JBS ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi 100,000/=.

Upande wa mchezaji mmoja mmoja wanaume Salum Yusuf alifanikiwa kutwaa ubingwa wa mkoa na kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi 400,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa wa Kinondoni kwenye fainali za Taifa upande wa wanaume na nafasi ya pili ilichukuliwa na Mohamed Idd ambaye alizawadiwa Shilingi 250,000/=.
Mchezaji mmoja mmoja Wanawake, Grace Thomas alifanikiwa kutwaa ubingwa huo na kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi 300,000/= pamoja na kuwakilisha mkoa katika fainali za kitaifa upande wa wanawake. Nafasi ya pili ilichukuliwa na Cecilia Kileo ambaye alizawadiwa fedha taslimu Shilingi 200,000/=.

Fainali za kitaifa za 2014 za “Safari National Pool Competion” zinatarajiwa kufanyika Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa kushirikisha mikoa 17 ambayo ni Tabora, Shinyanga, Dodoma, Mbeya, Iringa, Morogoro, Mwanza, Kagera, Manyara, Arusha, Tanga, Pwani, Ilala, Lindi, Temeke, Kinondoni na wenyeji wa mashindano kwa mwaka huu mkoa wa Kilimanjaro.

No comments: